PostGE2025 Tuanze kuyaita majengo na miundombinu kwa majina ya mashujaa wetu

PostGE2025 Tuanze kuyaita majengo na miundombinu kwa majina ya mashujaa wetu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
Tanzania imeingia zama mpya. Na zama mpya zinahitaji mitazamo mipya. Hili nililisema humu ndani kama siyo October 27 basi 28.

Tutahitaji kufanya resistance ya kila namna dhidi ya udhalimu, ikiwemo kutumia njia za kibunifu ambazo ni salama lakini zenye maana kubwa.

Mojawapo ya jambo nililowaza ni huku mitaani na mitandaoni kuanza kuyaita majengo ya serikali na miundombinu mingine majina ya mashujaa wetu wa kupambania demokrasia na wahanga wengine wa udhalimu.

Kwa mfano, tunaweza kuamua kuita stand ya SGR ya Dodoma "Mdude Nyagali Train Station". Tukikubaliana jina na eneo husika na likapita, tutaanza kulitumia katika maongezi yetu ya kila siku.

Tufanye hivyo katika maeneo yote waliyopeana majina bila kuzingatia uzalendo wa kweli wa wahusika. Siku yaja ambayo majina hayo ya mashujaa wetu na wahanga yatasimikwa rasmi.
 
Back
Top Bottom