Kwenye riadha na baadhi ya michezo mingine kuna kitu kinachoitwa 'False start". Hii inatokea pale ambapo kwa mfano mkimbiaji anaanza kukimbia kabla bastola haijapigwa (kutokana na papara au kitu kingine) au ameanza kinyume na taratibu nyingine. Hilo linapotokea wakimbiaji wote hurudishwa mstarini na kuanza moja.
Najiuliza kuwa yawezekana kama TAifa we had a false start and now we need to restart the building of our nation.
Kama tukiamua kuanza upya:
a. Tufute kesi zote za mafisadi
b. wenye kusahamewa ndiyo wasamehewe (kilichoenda kwa "mganga"! na iwe kama sandakalawe!
c. Panga upya vikosi vyote,
d. Pangua upya safi nzima ya uongozi na kupanga upya
e. andaa ajenda mpya ya taifa
n.k !
And then let see if we can start right!
Mkuu Mwanakijiji, natanguliza heshima nyingi. Mkuu matatizo yote ya kiutendaji tuliyonayo nchini yanatokana na mfumo usiokidhi mahitaji. Mfumo uliopo ambao kimsingi umejengwa na Katiba yetu, hauwezi kutuletea tija kubwa tunayoitarajia na ambayo wanasiasa wetu wamekuwa wakiizungumzia kwenye majukwaa ya siasa. Mfumo huu ni mgumu kuwa na mafanikio hata tukianza upya kila harakati kama ulivyoainisha.
Mimi naamini kuwa hatukuanza vibaya, ila tunaendelea vibaya. Ni sawa kabisa na mkimbiaji uliemtolea mfano, ambae ameanza mbio zake vizuri, halafu akasahau kuwa yuko mashindanoni na kuanza kuokoja maembe njiani au akaanza kuongea na simu huku akipoteza mwelekeo na muda bila kujali. Maana yake ni kuwa, sio tu kwamba mbio tunazokwenda nazo si za kimashindano, bali pia zinaelekea nje kabisa ya route inayotakiwa.
Nikirudi kwenye sababu za kimfumo zinazotufanya tushindwe kuendelea. Ukweli unabaki kuwa uzalendo kwa wananchi wote na hata viongozi wetu haupo tena, Ufisadi umeota mizizi, utendaji umeshuka sana (hasa kutokana na uoga wa kuthubutu walionao watendaji wa umma), na zaidi ushirikishwaji wa wananchi katika kujiletea maendeleo uko chini sana. Yote haya, ni matunda ya kuchezea au kuharibu misingi yetu ya uchumi ama kuweka misingi isiyoendana na hali halisi ya ukuaji wa Taifa huru.
Nahofia kuwa, kusamehe Mafisadi na hata watu wote waliopo magerezani hakutaweza kutatua tatizo lililopo. Kinachotakiwa sasa, ni kuunda Katiba mpya, yenye ushiriki wa wananchi wote na itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge (kama taratibu zilivyo). Katiba hii inatakiwa itoe nguvu zaidi kwa wananchi na sio kwa viongozi wachache kama ilivyo sasa. Iweke misingi imara ya kidemokrasia na utawala wa pamoja.
Katiba iweke bayana masuala ya uongozi ambapo kiongozi wa Taifa (Rais) asiwe ni mwenyekiti wa chama chochote cha siasa. Sababu ya hili ni kuwa, chama kilichomteua kuwa mgombea wake wa uRais kinatakiwa kiwe na uwezo wa kumhoji anapokwenda kinyume na ahadi za chama chake, na pia kiweze kumbadili kikiona hafai kugombea tena katika kipindi kinachofuata. Hali ilivyo sasa (inawezekana ni ya kimazoea zaidi, lakini haiko kisheria), inamfanya Rais awe na nguvu sana ndani ya chama chake, Taifa na taasisi zote nchini. Hii inayoweza kumfanya asiwe makini kiutendaji. Inawezekana hatujapata Rais alietumia vibaya madaraka yake kiasi hicho, lakini atakapotokea, itakuwa shida kumdhibiti.
Pili, ni vyema Mawaziri wote wanapoteuliwa na Rais, wajadiliwe na Bunge kuona kama wanakidhi mahitaji ya utekelezaji/utendaji unaokusudiwa katika agenda za nchi na walio na uwezo na maadili ya kuweza kulipeleka Taifa mbele. Imeshadhihirika sasa kuwa Mawaziri (ambao ni viongozi muhimu sana kitaifa) wamekuwa wakifanya mambo yasiyotegemewa na wenye maadili tata.
Azimio la Zanzibar (ambalo haliko kimaandishi hadi leo) linatakiwa lirekebishwe na kuweka misingi ya utawala bora. Mabadiliko yake yahusishe maazimio yaliyotangulia (hasa Azimio la Arusha) kwa kuyafanyia mabadiliko yaliyo ya lazima tu, badala ya kuyafuta maazimio hayo, ambayo yaliweka misingi mizuri ya kiutawala.