Tuanzishe Kampeni Google watuambie kwanini wamempa Mo Dewji umiliki wa Tanzania

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Kwenye mada "Nani anamiliki Tanzania..." Mwana JF Kinyungu akagugo kwa kutumia neno " Who is the owner of Tanzania" na jibu likaja Mo Dewji. Alipoweka hilo jibu kwenye ile mada nikadhani ni maskhara ama utani, lakini na mimi jibu likaja hilo hilo, nikashangaa sana.

Imekuwaje Google waseme Mo Dewji ndiye mmliki wa Tanzania? Je, Serikali inajua kuwa inasemwa na Google kwamba Mo Dewji ndiye mmiliki wa Tanzania?

Je, haina athari kwenye mambo mengi kimataifa, jee imeshatokea watu kuwasiliana na Mo kwa kudhani yeye ndiye anayeimiliki Tanzania?

Na wewe Gugo kwa kutumia sentesi hii "Who the owner of Tanzania" uone jibu litakuja lipi.

Tuipambanie Tanzania yetu.
 
Unajua huu muda ukiandika Nani anamiliki Tanzania linakuja uliloandika Wewe?
 
Jibu hili Nani mwenye Mkwanja Mrefu Tz ndiyo maana ya Google.halafu kumbuka source ya hiyo Information
 
Google sio site inayoaminika asilimia 100 kwa literature review, hasa wikipedia
 
Google hawa chapishi habari yoyote.
Kazi ya Google ni kutafuta tu
Habari imechapishwa Wikipedia
Na Wikipedia kila mtu anauwezo wa kuweka taarifa kama vile JF
 
Google sio site inayoaminika asilimia 100 kwa literature review,
Sawa. Hapa tunazungumza kwa wale wanaoiamini na hayo majibu, " kama wanavyosema hao wenye "Literature review" kwamba "We shall not take things for Granted"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…