Tubadilishe mwelekeo kidogo, can we also be a forum for something, not just against?

Tubadilishe mwelekeo kidogo, can we also be a forum for something, not just against?

Vipi na wewe una kiwanja ng'ambo? (Joke)

...nataka kukata foleni za ajabu ajabu mjini pale na sehemu ya mji kuhamia upande wa kigamboni,si unajua kama kuna daraja sisi wenye pesa tutajenga corporate office zetu kule maana huku kwingine ni vurugu tupu...nakuhakikishia likijengwa daraja viwanja kigamboni vitakuwa bei zaidi ya hapo mjini katikati au kariakoo,kuna beach kule mwanangu na tutaanza fresh kuupanga mji bila ujenzi wa ovyo ovyo....muhimu ni kukata foleni
 
Mimi nitakubaliana na wale wanaotaka maswala haya makubwa hasa rushwa na uhuumu uchumi yaendelee kuwa habari muhimu katika mjadala huu kwani nitarudia kusema kuwa pakacha la uchumi wetu linavuja kutokana na tobo zilizotokana na hayo mambo mawili hapo juu.

Hatuwezi kupuuza hata kidogo umuhimu wa haya maswala kwani elimu, kilimo, barabara, madaraja yote yatajengwa na fedha. Naamini kabisa Tanzania na pengine Afrika nzima hatuwezi kwenda mbele katika maendeleo ya aina yeyote ile ikiwa tunashindwa kuziba hizi tobo kwanza.

Guys, tuache ushabiki na kutazama swala hili kama vile ni jambo dogo sana ambalo linahitaji kusema kwa kiasi fulani kwani hizo nchi tunazozitazama kwa maendeleo yao wameweza kufika huko kutokana na kutokuwepo kwa maswala haya. Nimemsikia Dar sii Lamu kwanza akitoa agizo hilo la kutaka wakongwe tukate issue lakini sikuweza mjibu kwa sababu hakutaka kuelewa priority zangu. Tukiondokana na hawa mafisadi, fedha itakuwepo kuweza kujenga shule za maana, mishahara mizuri kwa walimu na vifaa bora vitapatikana, besides that tutakuwa tunajidanganya kuomba vitu hali mfuko mtupu.

Na hata ikitazama ranking ya nchi maskini duniani utakuta kwamba hujuma za uchumi wao ndio sababu kubwa ya kuwa katika umaskini.

Nilijaribu sana kubuni mfumo wa kiuchumi katika maendeleo ya Tanzania lakini nimekwama kutokana na tobo hizi ambazo nilizifanyia uchunguzi wa mtaani ili niweze kukamilisha jarida langu. Research yangu ndogo sana iliweza nifikisha katika kuamini kuwa hujuma za uchumi wetu ni kubwa sana kiasi kwamba maendeleo yetu yatasimama kama vile Nigeria pamoja na kwamba ni nchi tajiri sana kuliko Dubai na pengine nchi kubwa za magharibi. Hatutaki Nigeria kuwa mfano bora kwetu kwa sababu Ma Vogue yamejaa mitaani, tena wao wamezawadiwa sana katika elimu ambayo huitumia kuendeleza hujuma za uchumi wa nchi yao wenyewe.

Ndugu Kitila Mkumbo nakubaliana nawe sana tu kuwa tunahitaji kuzungumzia pia mapungufu katika sekta mbalimbali lakini kwanza inabidi tukubali kuwa mapungufu hayo yanatokana na hujuma za uchumi wetu. Fedha ikiwepo nadhani hayo yote yanaweza kufanyika kwa urahisi na muda unaotakiwa. First lets clean the house kabla hatujafikiria ni household gani zinatakiwa.

Tuendelee kumkoma nyani giledi.
 
Bandugu,

Niliposoma maelezo ya FD kutokea ddm kwenye uchaguzi, nilikata tamaa sana.

1. Kuambiwa madini kuchangia pato la taifa kwa asilimia 1.9.
2. Kama 10% tu ya Watanzania wana umeme.
3. Kuhusu 15% kwenye madini, bado negotiation zinaendelea! Mbona Karamagi alisema negotiations ziliisha?!

Mambo mengine ikabaki sentensi nzuri ya "Tunayafanyia kazi". Sentensi hii ndio ikazidi kunichefua. Hiyo naiita majibu rahisi kwa maswali ya msingi yanayohitaji majibu ya kina. Damn!

Kitila,

Tunashukuru kwa changamoto. Nafikiri tumekuwa sote toka enzi zile za BCS, tumekuwa tukimkoma nyani na pia humo humo kutoa mapendekezo ya utatuzi wa matatizo yetu. Tumeshuhudia mambo mengi yanafanyiwa kazi na mawazo yakitokea hapa hapa jamvi la JF, kama vile kuhusu usalama wa raia, utalii, n.k.

Kuhusu ajali barabarani, hilo pia limeshazungumziwa sana. Tazama ile mada ya Mar. Salome Mbatia (RIP). Watu wamezungumzia pia utendaji mbovu wa TRA na jinsi gani ya kuifanya TRA ifanye kazi kwa ufanisi.

Kuhusu madini, alikuwepo Dr. Khamisi hapa na mawazo yake safi kabisa. Kuhusu demokrasia, wapo akina MKJJ, GAMETHEORY (DrWHO). Kuhusu mambo ya uchumi na pato la taifa, namkumbuka Mzee Kamundu alikuwa anatoa mchango mzuri hapa.

Having said the above, nafikiri tundelee na kupigia kelele uovu huu, wakati huo huo tukitoa mawazo mbadala ya kutatua tatizo.

Of recent, kumekuwa na masuala ambayo, kwa maoni yangu, yamefanya hii JF yetu kuonekana kama ni sehemu ya watu tuliokosa mawazo mapya.

JF, tujitahidi kuvumiliana pale tunapokuwa na tofauti kifikra, kwani sisi binadamu hatuko sawa kiuezo.

Well, lets go back kukata ISHU kwa uhakika zaidi.

Mzee JASUSI uko wapi ndugu yangu?
 
Tuendelee kuchangia hoja kwa mtindo huu huu tunaochangia, ila tu, kila hoja iwe na Suggestion Box mahali ambapo mtu atamwaga shule yake kushauri juu ya utaribu fulani anaodhani ni tiba ya tatizo.
 
Well, mimi nafikiri tumeshakata sana issue za ufisadi hapa. Watu wameumbuliwa sana tu, na kwa kweli sisi tumeonyesha kwamba tunaweza sana kukemea na kuwaumbua mafisadi kuanzia wale waotuibia hela zetu kule BoT na kwenye taasisi zingine za umma hadi wale wenye tabia za kutokufunga suruali zao sawasawa. Yaani, kwa kifupi hii forum imefanikiwa kuwa a forum against ufisadi all other evils that befall our beloved country.

Nashauri tupige hatua kidogo. Can also be a forum for something?

Hebu tujiweke kidogo kama a policy review body. Ok, kuna hili tatizo la ajali, tutafanyeje kupunguza vifo vya wananchi wasio na hatia kiasi kile.

Kuna hili la shule. Tumeona mwenzetu JK shida yake ni wingi. Mashule mengi. Majengo mengi. Wanafunzi wengi. Walimu wengi hata kama hawaendi mashuleni. Yaani yeye ni mzee wa wingi, kwa sababu ni rahisi kupata sifa kwa kuangalia wingi wa kitu, ila ubora ni ngumu sana maana inachukua muda na wakati mwingine vigezo vya ubora ni controversial. Kwa hiyo kwa mtu anayependa sifa za sasa hivi itabidi akazania wingi, na ndio maana sisi wengine hatumshangai sana Rais wetu anavyokazania wingi wa vitu huku neno ubora likiwa mbali kabisa na midomo yake!

Nasikia kuanzia mwakani anakuja na sera ya dispensary kila kijiji! Yaleyale ya wingi, na hii wakiitekeleza itabidi dada zetu wanaomaliza la saba ndio wawe manesi na tusubiri watu kupata ulemavu wa miguu kwa kuchomwa sindano na watu wasio qualify!

Ok, nirudi kwenye issue ya elimu. Elimu yetu inaugua ugonjwa wa kutisha. Yote hii ya madaktari ya kumfanyia mtu operation ya mguu badala ya kichwa, inatoa taswira ya ugonjwa ambao elimu yetu inaugua. Hawa ni matunda ya elimu yetu mbovu.

Sasa sisi hapa kama policy review body, tunawezaje kuboresha elimu yetu? So far hapo juu, as usual, nimefanikiwa tu kuwa against something. Je, tunaweza ku-propose something?

Tukate issue hapa, nami nitashuka baadaye kidogo na mapendekezo yangu (something for).

PS: hii mada ikiwa misplaced, naomba nisamehewe bure na ipelekwe panapohusika kama sio mahala pake.

Kwa maoni yangu KIINI cha matatizo mengi ya nchi yetu ni ufisadi, rushwa, viongozi waroho wa utajiri walioweka mbele maslahi yao badala ya Tanzania na kusaini mikataba mibovu. Haya ndio KITOVU kikubwa cha matatizo yetu ya huduma mbovu mahospitalini, mashuleni, barabara mbovu, kilimo duni n.k. Mpaka hapo tutakapoweza kupambana na mafisadi, wala rushwa, wanaotumia nyadhifa zao kujitajirisha, wanaosaini mikataba mibovu na kushinda, kamwe Tanzania tunayoitaka itabakia kuwa ni ndoto tu. H
 
freedom of expression, people have the right to talk what they think is right at that particular time.

At this time Tanzania has many failure than succession, so there is no time to point out the construction of one bridge, while there are many bridges collapse. Our part is not to criticise government, but to challenge them.
 
Bandugu,

Mzee JASUSI uko wapi ndg yangu??

Tena umenikumbusha akina Sam, Kyoma, Eric Ongara, mgongomgongo, tafiti then jadili, n.k. wote hawa wamepotelea wapi siku hizi?
 
Naamini kuwa Kitila anachosema ni zaidi ya kuwa mahali pa ukosoaji bali pia pawe mahali pa mawazo mapya, mawazo ya utatuzi. Labda inawezekana tuwe na kasection ka "brain storming" ambapo mawazo yetu mbadala wa jinsi gani vitu viwe au vinapaswa kuwa yanaweza kutolewa na kuchambuliwa.

Section hiyo isiwe mahali pa kulalamika bali kugongana mawazo ya kuona nini kifanyike na hakuna mawazo yatakayopigwa marufuku isipokuwa yasiyohusiana na mawazo mbadala.

Iwe ni mahali pa brain storming for real, na kwa kufanya hivyo siyo tu tutashirikiana katika kuonesha mapungufu au makosa bali pia tutachangia akili zetu kutafuta suluhisho. Tunachoweza kufanya ni kuchagua mada za ku tackle that particular day or week..

Mawazo mbadala ni kitu cha msingi sana, lakini hata hivyo nina wasiwasi wa wahusika kuyachukua hayo mawazo na kuyafanyia kazi.

Wapinzani walikuja na bajeti mbadala, badala ya watawala kuipa uzito walikejeli juhudi hizo za wapinzani.

Labda tuutumie uwanja huo kujifurahisha!!!!!!!!!
 
Kitila una wazo zuri ila mie nahisi unajaribu kuukimbia ukweli ili ujiliwaze kidogo baada ya kuchoka na hiyo maada.Tatizo ni kuwa tutazunguka na kurudi palepale.Matatizo yote yanayotukabili watanzania yanasababishwa na Uongozi.
Uduni wa elimu tatizo nini?
moja ya sababu itakuwa waalimu duni(mtu wa division IV anasomea ualimu miezi 6) wasio na motivation.Sababu:Waliofaulu vizuri hawataki kuwa waalimu kutoka na mishahara midogo,kutothaminiwa na hakuna motivation.Sababu wizara inatengewa pesa kidogo.Sababu tunaambiwa sirikali haina pesa.Sababu viongozi wanaiba pesa na kuingia mikataba mibovu.
Kilimo duni.Sababu: Kipaumbele hakuna na bajeti ndogo-Hakuna pesa-Zinaibiwa na hazikusanywi ipasavyo.

Ukiangalia katika issue nyingi watu wamejaribu kutoa solution.Mfano ya Wizi wa mali ya Watanzania na mikataba mibovu:Watu wamesema😛CCB ipewe meno,Bunge lisiwe sehemu ya serikali,Sheria na katiba zirekebihswe,Waliohusika na ubadhilifu wafikishwe mahakanani na kufilisiwa wengine wafukuzwe kazi.

Ninaloliona tatizo ni kuwa tumekuwa na vijihabari vya kijinga jinga vinawekwa hapa kwenye siasa ili mradi tu mtu aonekane kaleta topic mpya au kamjibu mtu au kwa makusudi ahamishe attention za watu toka mada muhimu au kwa ajili ya kulipiza kisasi kutokana na dongo alilojenga kwa mtu au kikundi, kutokana na kuchangia au kuanzisha topic fulani.Mengi nimeona yamekuwa yakichangiwa kwa ushabiki tu na si mada yenyewe.
 
Nyangumi et al., mimi nakubali kabisa. Unajua hapo karibuni tulianza kutoka kwenye mstari. Tulikuwa obsessed sana na issue ya uchaguzi wa CCM na zile picha fake za JK na mambo yake ya US. Lengo la mada yangu hii ilikuwa ni kujaribu kuwarudisha watu kwenye mstari, nafikiri kwa kiasi fulani lengo limefanikiwa maana sasa watu naona wanakata issue hasa kwenye kila mada, no matusi no what safi kabisa.

Nimefurahishwa na hoja yako ya uongozi kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu. Ningeeda mbele zaidi ni kusema uongozi wa CCM ndio hasa chanzo kutokana na kuchakaa na kuwa nje ya wakati. Yaani kukubali kutawaliwa na CCM kwa kipindi hiki ni sawa na kuvaa t-shirt wakati wa winter ya mwezi wa 12 au 1, lazima tuchanganyikiwe. Siku watanzania tukielewa hili itakuwa ndio itakuwa mwanzo wa kupata ufumbuzi wa matatizo yetu lukuki.
 
Kitila Mkumbo,
Waziri Membe ameomba Bungeni Tsh Billioni 8 kwa ajili ya matumizi ya safari za viongozi wakuu. Inamaana Kikwete, Lowassa, na Shein, watatugharimu Tsh. zaidi ya Billlioni 80 assuming wana-serve miaka 10.

Hivi haiwezekani kuchota atleast Tsh. Billioni 30 kati ya hizo, wakakopeshwa a few INDIGINOUS INDUSTRIAL CAPTAINS tukawa na wawekezaji/wazalishaji wa ndani? Hatuwezi kuendelea kwa kutegemea makampuni yaliyoandikishwa nje.

Kila nchi iliyoendelea uchumi wake unaendeshwa na makampuni ya ndani ya kizalendo.
 
Fedha kila siku siyo tatizo,tatizo ni namna ya kuzitumia.

MTZ akiambiwa fedha siyo tatizo, atakuuliza ziko wapi mbona mimi sizioni?
Fedha siyo tatizo msemo huo unamaana kwamba kiasi chochote ulicho nacho ni fedha muhimu ya kukuondoa hapo ulipo.

kijana mtaani utamsikia akisema " kila siku napata fedha ya kula tu" fedha ya kula ndo Tshs ngapi?

"Tatizo ni namna ya kuzitumia" sentensi hii ina maana kwamba siku zote sisi watu wa dunia ya 3 tunatumia fedha katika mambo yasiyo tusaidia kwanza kisha tunang'aa macho na kupanga bajeti hewa juu ya mambo muhimu.

Labda niseme hivi; Fedha ziibiwazo serikalini au zitumikazo kwa mambo ya ovyo ndiyo fedha ziwafaazo wajanja daraja la pili na la tatu pale tanzania ambao wengi ni kundi la wafanya biashara na waunganishaji wa misheni hapa na pale.

Kwa vile wajajnja hawa huonekana matajiri mbele za wananchi wa kawaida au wanasiri ya maendeleo wasemacho kwa wananchi mitaani huchukuliwa kama ukweli usio pingika.

kampeni za kisiasa mara zote huimarishwa kupitia mkondo wa kundi hili la watu wafaidikao na ubadhirifu hadi kuwafikia wale wasiofaidika na kuwashawishi kuunga mkono utaratibu uliopo.
 
Kuna mwana-forum mmoja amesema kuwa kumbi na nafasi za kujadili matatizo mengine yanayoikabili nchi yetu zipo bwelele,kwa mfano section ya hoja nzito.Tunaweza kutaka kubadili mwelekeo kwenye section hii YA SIASA lakini tukumbuke kuwa matatizo yanayoikabili sekta ya huduma za jamii (elimu,afya,barabara,umeme,maji,nk) yanachangiwa kwa asilimia kubwa na wana-SIASA wetu ambao tunawasuta na kuwakemea hapa kila siku.Let's be honest,kujadili elimu ni jambo la muhimu,lakini tunategemea mijadala ya namna hiyo itazaa nini iwapo viongozi wetu ndio hawa ambao kauli yao ya kuridhisha ni ile ya "tanafanyia kazi".Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,kamwe hatacheza.

Idea ya kuwa na mijadala ni nzuri,lakini ingekuwa nzuri zaidi iwapo watawala wetu wangekuwa wameshabadilika na wako tayari kushauriwa.Kam wameweza kupuuza bajeti mbadala ya wawakilishi halali wa wananchi (wapinzani walio bungeni) sasa hapa si tutakuwa tunapoteza muda wetu bure tu.Focus ya kuwaumbua,kuwasuta na kuwasakama ni mwafaka zaidi kwa sasa kwani iwapo mkakati huo utafanikiwa,then tutakuwa na uhakika kwamba ushauri unaopatikana hapa utafanyiwa kazi.

JK na wapambe wake hawatembelei JF kufuata ushauri bali kuangalia skandali gani zimemwagwa hapa.Hawa sio viziwi bali wanajifanya tu kuwa hawasikii na ni wabishi,na dawa ya viumbe kama hao sio kuwafanyia diplomasia bali kuwapigia kelele zaidi na zaidi mpaka hapo watakapoona aibu na kubadilika.Naamini hata hayo "mazingaombwe ya Dodoma" sio matokeo ya ushauri mzuri bali ni matunda ya kelele za akina Kabwe,Slaa na wananchi kwa ujumla (wale wenye machungu na nchi yao) hususan wale walioamua kuwazomea mafisadi.

Moreover,sidhani kama kuna ubaya iwapo mie nitamlaumu Karamagi kwa kutuingiza kwenye mikataba ya kilevi kuliko ya machifu wetu wa zamani,halafu member mwingine aka-brainstorm kwa kushauri marekebisho yanayohitajika kwenye sekta nzima ya madini na raslimali nyingine.Ni suala la approach tu....

Nieleweke kuwa sipingani na hoja ya Bwana Kitila bali nadhani anachoshauri ni sehemu ya tunachokifanya kila siku
 
Hi Guys, honestly i think kitila is right there are many things which need to be addressed especially in education, equality, peoples rights etc.

So it will be better if something for example education can be discussed here in details from the class rooms and everything.

It'll be better to discuss things which are more constructive.

Nawakilisha
 
Mlalahoi,
Kule kwenye hoja nzito watu hawatoi michango sana- hapo nyuma niliweka hoja ya "Plight of Disabled in Tanzania-" we got very few contributions! Nafurahi kwa hii hoja ya ajali!
Unajua huku kwenye siasa- na haya mambo ya udaku naona ndiyo watu wengi wanapenda! Sijui ni kwa nini! Fikiri iliposemwa kuna picha za ngono za JK- so much attention! Sasa unadhani ukileta hoja "njito" watu kweli watatoa the sema attention?
 
Well, mimi nafikiri tumeshakata sana issue za ufisadi hapa. Watu wameumbuliwa sana tu, na kwa kweli sisi tumeonyesha kwamba tunaweza sana kukemea na kuwaumbua mafisadi kuanzia wale waotuibia hela zetu kule BoT na kwenye taasisi zingine za umma hadi wale wenye tabia za kutokufunga suruali zao sawasawa. Yaani, kwa kifupi hii forum imefanikiwa kuwa a forum against ufisadi all other evils that befall our beloved country.

Nashauri tupige hatua kidogo. Can also be a forum for something?

Hebu tujiweke kidogo kama a policy review body. Ok, kuna hili tatizo la ajali, tutafanyeje kupunguza vifo vya wananchi wasio na hatia kiasi kile.

Kuna hili la shule. Tumeona mwenzetu JK shida yake ni wingi. Mashule mengi. Majengo mengi. Wanafunzi wengi. Walimu wengi hata kama hawaendi mashuleni. Yaani yeye ni mzee wa wingi, kwa sababu ni rahisi kupata sifa kwa kuangalia wingi wa kitu, ila ubora ni ngumu sana maana inachukua muda na wakati mwingine vigezo vya ubora ni controversial. Kwa hiyo kwa mtu anayependa sifa za sasa hivi itabidi akazania wingi, na ndio maana sisi wengine hatumshangai sana Rais wetu anavyokazania wingi wa vitu huku neno ubora likiwa mbali kabisa na midomo yake!

Nasikia kuanzia mwakani anakuja na sera ya dispensary kila kijiji! Yaleyale ya wingi, na hii wakiitekeleza itabidi dada zetu wanaomaliza la saba ndio wawe manesi na tusubiri watu kupata ulemavu wa miguu kwa kuchomwa sindano na watu wasio qualify!

Ok, nirudi kwenye issue ya elimu. Elimu yetu inaugua ugonjwa wa kutisha. Yote hii ya madaktari ya kumfanyia mtu operation ya mguu badala ya kichwa, inatoa taswira ya ugonjwa ambao elimu yetu inaugua. Hawa ni matunda ya elimu yetu mbovu.

Sasa sisi hapa kama policy review body, tunawezaje kuboresha elimu yetu? So far hapo juu, as usual, nimefanikiwa tu kuwa against something. Je, tunaweza ku-propose something?

Tukate issue hapa, nami nitashuka baadaye kidogo na mapendekezo yangu (something for).

PS: hii mada ikiwa misplaced, naomba nisamehewe bure na ipelekwe panapohusika kama sio mahala pake.

It is too late for Tanzanians to speak something for mbona tutakuja kugundua tembo kabaki mkia mkianza kusifia hawa watu wanapenda sana sifa huku wanaendelea kudokoa kidogo kidogo. Let us be against ndipo tutapunguza kasi ya kila kitu kama rushwa wizi wa mali za serikali matumizi mabaya ya mali za serikali kama vile unakuta boss mzima yuko na gari la serikali kwenye bar nk.
 
Back
Top Bottom