Tuboresheje elimu ili kuzuia/kuondoa wimbi la kufeli wanafunzi?

Tuboresheje elimu ili kuzuia/kuondoa wimbi la kufeli wanafunzi?

Gaston Mbilinyi

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2010
Posts
296
Reaction score
51
Matokeo ya kidato cha nne 2012 yametoka hivi karibuni na yameleta gumzo miongoni mwa jamii ya ndani na nje ya Tanzania kutokana na namna wanafunzi walivyofeli. Achilia mbali kufeli, wanafunzi wengine badala ya kujibu maswali wakachora picha za watu, wengine wakatukana matusi na wengine kuandika beti za bongo fleva! Viongozi wetu wameweweseka na hata kupata kigugumizi maana inaonekana wana mchango mkubwa kwa watoto kufeli kiasi hicho! Hakika hii ni aibu ya taifa wala si ya watoto waliofeli tu.

Nimekuwa nikifuatilia sababu zinazotajwa kuwa zimechangia wanafunzi hao kufeli na wengi wanasema sababu zifuatazo kuwa ndio source ya sisi kama taifa kuaibika kiasi hiki.
1. Ukosefu wa walimu.
2. Ukosefu wa vitabu vya kiada na ziada ( kufundishia na kujifunzia)
3. Ukosefu wa maktaba
4. Ukosefu wa Maabara
5. Kukosekana kwa haki za walimu wanazopaswa kulipwa kisheria
6. Kukosekana kwa mitaala kumesababisha ufundishaji uwe shagalabaghala toka shule moja hadi nyingine
7. Kukosekana kwa motisha kwa walimu.
8. Upungufu wa vitabu na vifaa vya maabara.
9. Utandawazi ambao umechukua sehemu kubwa ya ubongo wa wanafunzi na hivyo kupuuza masomo.
10. Wazazi kutoshirikiana kwa ukaribu na walimu katika usimamizi wa wanafunzi.
11. Uwezo binafsi wa wanafunzi kuwa mdogo kwani wengine huchukuliwa wakiwa na alama za chini sana katika
kuingia kidato cha kwanza.
12. Uwezo mdogo kwa baadhi ya walimu.
13. Ualimu kuwa ni kimbilio la baadhi ya wakosa ajira ambao hawapo tayari kufundisha ila wapo tayari kwa mshahara.
14. Baadhi ya viongozi wa nchi kuona suala la elimu si muhimu ila siasa ndiyo muhimu kwao hivyo nguvu huelekezwa
katika siasa na hivyo elimu kutokuendeshwa kitaalamu bali kuongonzwa kisiasa.
15. NECTA wamejaa watu wa dini moja ambayo inakomoa watu wa dini nyingine
16. Masomo yanafundishwa kwa kiingereza badala ya Kiswahili
17. Watoto wanaanza form one wakiwa wadogo mno hivyo uelewa wao kuwa mdogo pia
18. Hali duni ya mazingira ya kufundishia mfano wanasema hakuna madawati na wengine chaki, umeme, n.k.
19. Watoto wa wakubwa/vigogo kutosoma katika shule hizi kunafanya vigogo kutojali kuboresha mazingira ya kufundishia
20. Shule nyingi za private ama ni za vigogo au vigogo wanahisa katika shule hizo hivyo hata huku kwa sisi walala hoi
kukiwapo kubovu hawajali, wao wanaangalia zaidi biashara yao ya hizo shule za private

Naamini na wengine yawezekana wamesikia sababu zingine wanaweza kuongezea hapo. Lakini najiuliza kujua sababu tu ya wanafunzi kufeli kunatosha? Kama ni kweli sababu ndio hizo, basi sasa tuchukue hatua nyingine ya kujadili namna tutakavyo weza kuondoka hapo kwaajili ya kuondoa tatizo.

Mimi nafikiri shule na vyuo vifungwe kwa japo mwaka mmoja na ndani ya mwaka huo yafuatayo yafanyike:
1. Sensa ya walimu ifanyike sambamba na shule tulizo nazo (ingawa shule zinajulikana)
2. Idadi ya walimu iliyopo igawiwe kwa shule zilizopo kwa kuzingatia nani anafundisha nini ili kuepuka walimu wanaofundisha
somo moja kulundikwa shule moja.
3. Walimu wafanyiwe semina au makongamano kwaajili ya kuwaweka sawa maana inaonekana wengine wanajisahau
4. Serikali iboreshe mazingira ya kufundishia kwa kuhakikisha inaweka vitabu na vifaa vingine pamoja na madawati
5. n.k.

Naomba michango yenu ya nini kifanyike ili kutatua tatizo la wanafunzi wetu aw sasa kufeli, kumbuka kila tatizo huwa na jibu.
 
>Kiboko kinasaidia kurekebisha tabia ya mtoto,hili lipo hata kwenye vitabu vitakatifu.
Kufuta adhabu ya viboko serikali ilikurupuka.
>Tatizo la uwing wa waalimu si sana, kwan mwaka jana waalimu walikuwa wachache kuliko mwaka huu lakn hawakufel namna hii?
>sababu yako no.5 yaweza kumata hapa kuwa yawezekana ni kisasi cha waalimu, lakn hii haitosh kwan wanafunz wameonekana wakichora had pcha licha ya matus wanayoyaandka.
KIKUBWA HAPA NI KUSHUKA KWA MAADILI, NA HILI HALIPASWI KUIACHIA GVT PEKEE,BALI KWA PAMOJA KAMA TAIFA TUSIMAME KIDETE NA KULITAFUTIA UFUMBUZI YAKINIFU. Hasa ktk ngaz ya familia na din.
 
>Kiboko kinasaidia kurekebisha tabia ya mtoto,hili lipo hata kwenye vitabu vitakatifu.
Kufuta adhabu ya viboko serikali ilikurupuka.
>Tatizo la uwing wa waalimu si sana, kwan mwaka jana waalimu walikuwa wachache kuliko mwaka huu lakn hawakufel namna hii?
>sababu yako no.5 yaweza kumata hapa kuwa yawezekana ni kisasi cha waalimu, lakn hii haitosh kwan wanafunz wameonekana wakichora had pcha licha ya matus wanayoyaandka.
KIKUBWA HAPA NI KUSHUKA KWA MAADILI, NA HILI HALIPASWI KUIACHIA GVT PEKEE,BALI KWA PAMOJA KAMA TAIFA TUSIMAME KIDETE NA KULITAFUTIA UFUMBUZI YAKINIFU. Hasa ktk ngaz ya familia na din.

Sababu No. 5 siyo yangu ila ni moja kati ya sababu nilizo zisikia. Hapa tunatafuta njia ya kutatua tatizo. Nashukuru kuwa unashauri kuwa wanafunzi wapewe haki yao ya fimbo inapobidi, nakubaliana nawe juu ya hili kwani hata mimi enzi hizo hakika nilitandikwa sana. Ingawa ni kweli kuwa walimu wa kizazi cha leo wanaweza kuhamisha hasira za ugomvi wa nyumbani kwa watoto shuleni. Pia nakubaliana kuwa wazazi tujitahidi kuwalea watoto katika maadili mazuri.
 
Back
Top Bottom