Tuchague kwa busara, Mbwa watulinde au tuwalinde mbwa?

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Posts
7,359
Reaction score
5,837
Anaandika Askofu Bagonza

Mbwa hubweka. Asiyebweka hata akipigwa jiwe ni “mdoli “ wa mbwa. Mbwa halisi ukimzuia kubweka, utabweka wewe.
Mbwa akibweka usiku humwamsha mwenye nyumba toka usingizini ili aione hatari iliyopo. Asipobweka, mwenye nyumba huamka kumwangalia mbwa kwa nini habweki. Kwa tendo hilo, mwenye nyumba hugeuka kuwa mlinzi wa mbwa

Tuchague kwa busara; Mbwa watulinde au tuwalinde mbwa?
 
Huyu Askofu ana maneno ya busara sana.

"Tuchague mbwa watulinde, au tuwalinde mbwa"

Mimi napenda mbwa anilinde, kwasababu mbwa hawezi kuwa bosi wangu. Ila yupo mwingine anapenda kumlinda mbwa, nina mashaka kama yupo vizuri kichwani.
 
Gwaji boy kamshauri mwenye nyumba awaache mbwa wabweke.
Naona hapo maaskofu toka ktk makundi kinzani kifikra wafanana kwenye wazo la busara... Let them bark and rejoice.....
 
Mzee wa what is wrong is wrong regardless who did that!!
 
Thanks mods kwa kuweka heading nzuri
 
Spana za Gwajima naona zimewatoa watu mafichoni! JPM kaza mwendo! ,wacha waendelee kubweka
 
Magufuli kasajili bunduki, anasema hahitaji mbwa, style ya zamani hiyo.
 
Hii sasa ni hatari sana, Yaani Askofu Bagonza hakumuelewa Waziri Winston Churchill alikuwa ana maanisha nini kwenye mfano huo wa kubweka kwa mbwa!? Au ndiyo anataka ku'rig' maelezo ya askofu mwenzake!?
 
Anaandika Askofu Bagonza

Mbwa hubweka. Asiyebweka hata akipigwa jiwe ni “mdoli “ wa mbwa. Mbwa halisi ukimzuia kubweka, utabweka wewe.
Mbwa akibweka usiku humwamsha mwenye nyumba toka usingizini ili aione hatari iliyopo. Asipobweka, mwenye nyumba huamka kumwangalia mbwa kwa nini habweki. Kwa tendo hilo, mwenye nyumba hugeuka kuwa mlinzi wa mbwa

Tuchague kwa busara; Mbwa watulinde au tuwalinde mbwa?
Good analysis, kwa mantiki hiyo ndiyo maana unatakiwa kumuacha aendelee kubweka na wala haina haja ya kumpiga mawe ili asiendelee kukupigia kelele ya kubweka, hivyo mwenye nyumba mwache aendelee kufanya yale aliyokusudia. WAACHE MBWA WAENDELEE KUBWEKA... huku mwenyenyumba akisomga mbele. NIMEIPENDA HIYOO
 
Hii sasa ni hatari sana, Yaani Askofu Bagonza hakumuelewa Waziri Winston Churchill alikuwa ana maanisha nini kwenye mfano huo wa kubweka kwa mbwa!? Au ndiyo anataka ku'rig' maelezo ya askofu mwenzake!?
Baba Askofu ana kinyongo mgombea wake kapigwa chini mazima.
 
Good analysis, kwa mantiki hiyo ndiyo maana unatakiwa kumuacha aendelee kubweka na wala haina haja ya kumpiga mawe ili asiendelee kukupigia kelele ya kubweka, hivyo mwenye nyumba mwache aendelee kufanya yale aliyokusudia. WAACHE MBWA WAENDELEE KUBWEKA... huku mwenyenyumba akisomga mbele. NIMEIPENDA HIYOO
Hujamuelewa na hutamuelewa
 
Back
Top Bottom