Tucheke kidogo maoni ya ndugu yetu alipokuwa akiulizwa maswali.

Ukaridayo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Posts
515
Reaction score
476
Mimi kama Mtanzania nina haki ya kutoa maoni kuhusu mambo yanayoendelea hapa nchini

Nitatoa maoni yangu kuhusu Makontena na Mgambo aliyetoa kipigo

1:KUHUSU MAKONTENA
Kwa mtazamo wangu Mimi nashauri maeneo yote ya mabondeni na kwenye misitu mikubwa swala la kuku na tairi za guta tuwaachie wanariadha ambao kwakweli wanaimba Kwaya kwa kiwango cha Stigilazi Goji

2:KUHUSU MGAMBO
Sitaki kuingia deep sana kwenye swala hili kwasababu timu kama Arsenal na Chelsea hazipo kwenye mashindano ya UEFA lakini pia barabara kuu ya Songea Masasi ambayo ni kivutio cha maji inapaswa kujengwa uzio

Ni maoni yangu jamani, sijui wengine mnaonaje.
ngoja nikatoe maoni mengine kwenye group lingine maana hapa tayari..
🤣🤣🤣
 
Hii imekaa vizuri sana hasa pale waandishi wanapokuuliza maswali ya kukutega/kuchonganisha.
Mfano kuna wanafunzi walikuwa wakiingia kny mtihani akikuta swali halijui anajibu kitu alichokisoma ili mradi ajaze answer sheet.
 
Hii imekaa vizuri sana hasa pale waandishi wanapokuuliza maswali ya kukutega/kuchonganisha.
Mfano kuna wanafunzi walikuwa wakiingia kny mtihani akikuta swali halijui anajibu kitu alichokisoma ili mradi ajaze answer sheet.
Mkuu hayo maoni utawezaje kuyajibu mbele ya kamera za waandishi wa hbr.. ikiwa kichwa hakina maruhani ujue unatakiwa uwe na moyo kweli..
 
Hii ungeiweka kule joke/utani tungekuelewa. Sio kila jukwaa unaposti ukiwa umevuta.
 
Reactions: Paw
Tucheke au tulie maana huu ni msiba
 
Nimerudia kusoma Kama mara 5 nikatoka na 0

Ametisha huyo jamaa
 
Ngoja na mimi nisiingie deep sana,,

"SAWA"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…