kalipeni
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 1,571
- 1,328
Hebu tuongee ukweli tu; umetoka kwenye mkesha flani wa aina yoyote ile, asubuhi ukaamua kulala chumbani kwako ili kupunguza uchovu na usingizi.
Ukaandaa maji ya kuoga kwenye beseni pindi utakapoamka uoge na kuendelea na mambo mengine ya ujenzi wa taifa; wakati umelala usingizi mnono ulioambatana na ndoto tamu tamu; mara ukasikia mlango unagongwa kwa nguvu; "ngo ngo ngo, hodi".
Ile unakurupuka kwenda kufungua mlango, mara ukajikwaa kwenye beseni la maji yakamwagika sakafuni, mara ukateleza na kuangukia meza ya Tv ikaanguka chini na kupasuka, king'amzi, deck na bufa vyote chali.
Ukaamua ufungue mlango kwanza uone nani anabisha hodi, mara unakutana na wakala amevalia mavazi yake ya kikazi anakwambia; "TUNAKAMILISHA USAJILI WA LAIN KWA KUTUMIA ALAMA ZA VIDOLE KWA GHARAMA YA SH. 1,000/= TU".
Je, utamjibuje?