Tucheke na mama zetu leo

Tucheke na mama zetu leo

Hii ni mamazetu wote .hapo utafikiri walimuona mamaangu huuh!r.i.p mama
Kuna ile unachapwa alafu anakwambia kimyaa..
Nilikua sijui kwa nini wanafanya hivyo..
Ila nimekuja kutambua mama anakua anaumia akimuona mwanae analia.

love thé love or hâte thé love.....
 
Huyu atakuwa Mmama wa bongo movie kwani mimi Mama yangu hajawahi kuniambia haya hata siku moja, ni mke wangu tu huwa anakuwa na maneno machache uliyo andika humu so I guess katoa kwak au huko mitaani. Nikichelewa kurudi nyumbani utamsikia kakulisha nini leo? Simjibu kwani najuwa anamaanisha nani n nini lengo lake. Akiona sina jibu ananifuata chumbani na kunisachi change, akikuta hakuna utamsikia yaani baba wewe huna hata huruma, hela zote umemuachia yeye? Yaani ni full vituko....nikila na kuita watoto tule wote utamsikia, unawaitia watoto ili ukale kule? Yaani hapa sina hata hawara na sijafikiria kuwa naye kwani nampenda sana mke wangu ila vituko vyake tu ni muziki shinda Twanga Pepeta na ndicho kitakachonikimbiza kwake.
Huna haja ya kukimbia...ichukulie poaitive...akiongea wee cheka tu..
Siku nyingine jivike ukauzu na umtolee uvivu umpe makavu live
Umenishangaza kusema hao wamama wa bongo movie!!!!
Hao ni mama zetu huku mtaani my mom was exactly like that japo anazeeka amepoa sasa.

love thé love or hâte thé love.....
 
Ni pale unapokuwa wa kwanza kiwilaya au kimkoa unampa taarifa anaishia kuitikia Aaha.

Post sent using JamiiForums mobile app
Niliwahi kuwa wa 20 kile kipigo sijawahi kukisahau..

love thé love or hâte thé love.....
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38] haaaa wazazi wetu walitufundisha vizuri kwa alama za ishara du walikuwa safi hao duu, je nasi hata robo ya hayo tunayafanya kwa watoto wetu au nikukenua tu? Au ni b kulaumu watoto wasiku hizi wakati walezi ni siye hawa hawa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii huwa inabore sana unakuta mtoto anafanya mambo ya kijinga mbele ya wageni na mzazi wake anaona sawa tuu wala hamkemei mtoto eti madai yao wanawapenda watoto wao ndio maana watoto wanawazalilisha mbele za watu hayo ni malezi ya kipuuzi mno.
Unafika ugenini unapew Soda mtt anaiwahi anapiga tarumbeta mzazi unakenua tu loh ni shida hiki kizazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!!!sisi watoto wa zamani tulikuwa watiifu sana hata kwa mambo hayawezekani.
kuna siku nilijaribu hili zoezi kwa mtoto wangu lkn nilifeli kwa maswali niliyopata.
1.aliuliza kwa sababu gani?
nikamjibu ili uende haraka na urudi haraka.
2.kwani mama mate huwa yanakauza muda gani?
nikamjibu baada ya dakika 10.
Akasema mama siyo mbona mimi nikitema mate yanakauka saa hiyohiyo.

Alienda nilikomtuma lkn siyo kwa masharti ya kutema mate.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kwa leo mkuu unahojiwa maswali kama hayo, zamani unapata wapi ujasili/mda wa kuuliza hivyo!!!

mimi hiyo ya kutema mate iliniumiza sana aisee kuna siku nakumbuka niliagizwa dukani akatema mate chini mbio zikaanza harafu mvua ilikuwa imenyesha tope kibao si nikateleza nikapoteza hela ewaaaaa!! mkuu acha kabisa kwanza nyumbani nilirudi saa 20pm nikachezea kichapo kitakatifu harafu hakuna kula.
 
Iiuu88u ii
[emoji68]‍[emoji65]‍[emoji65][emoji68]‍[emoji66]‍[emoji65][emoji68]‍[emoji66]‍[emoji65] Nani kama mama ??

Utajuaje kama mama ako ni mtanzania.........

-Ni pale unapo mkopa hela alafu uki mdai.... Ana kuuliza chakula unacho kulaga humu ndani uwa unalipia..?
Huyo mbongo

-Ni anapo kuachia kazi alafu anaenda na remote kazin.......usisubir kuambiwa

-nipale unapo aga kwenda kwa rafik ako kupiga story alafu anakuuliza iv Lin uyo rafik ako amewah kuja kwenu....... Huyo hajahamia bongo

Nipale anapo kuuliza kama chakula alicho kupakulia kinatosha ukisema hapana ana kwambia kapike mwenyewe...... Huyo wakwetu

Ni pale unapo wekewa nguo za Aina mbili za jumapil na zakushindia sasa jikute nunda ushindie za jumapil utajuta kwa hayo makofi.......mama huyo wahapahapa

Nipale unapo sahau kumsalimia asubuh alafu ana kusalimia yeye shkamoo.... Ohoo kaa mbali kwa mda huo..... Huyu haina haja ya kuulizia anatokea wapi

Nipale anaposinzia huku mnaangalia tv na hatak mbadilishe channel.....huyu wahapahapa......

Nipale unapo kuwa store alafu anakuita jikoni alafu anakwambia nenda kanichukilie mwiko store..... Na huyu niwaambie anatokea wapi..

Kuna Vyombo vingine anavitoa tuu wakija wageni..... Haaahaa ni mama usimuulize utaifa huyu unakosea

Ni pale unavo rud kwenu unamwambia umeshika nafasi ya pili darasan anakuuliza wa kwanza anavichwa vi wili??..... Yupo kweny list ya wamama wabongo...

Sasa unataka kujua serikali ina mkono mrefu @Dokoa nyama udakwee!!!!!!!!!
Utamuona trump kwenye mwembe .....

a tunawapenda mama zetu wakitanzania.........
.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni pale unapokosea wakati wageni wapo, halafu asubiri wageni waondoke upate kichapo
 
Huna haja ya kukimbia...ichukulie poaitive...akiongea wee cheka tu..
Siku nyingine jivike ukauzu na umtolee uvivu umpe makavu live
Umenishangaza kusema hao wamama wa bongo movie!!!!
Hao ni mama zetu huku mtaani my mom was exactly like that japo anazeeka amepoa sasa.

love thé love or hâte thé love.....

Ahsante ila wakati mwingine mtu unalazimika kutoka nje ya ndoa hata kama hauna nia ili tu upate mtu wa kukufariji. Maana unafikiria muziki unaopigwa na mkeo nyumbani ni Zaidi ya disco la watts 10000, sasa hapa utafanyaje? Kina Mama kwa kweli ndiyo wanaotufanya sie wanaume tuwakimbie na kutafuta nyumba ndogo.
 
Kukimbia kutafuta nyumba ndogo ni justification tu...
Ika haiwezi kubadili uhalisia uliopo katika ndoa yako.
Zaidi utaongeza stress na kuchochea moto.
Wanandoa wengi hawana mawasiliano mazuri.
Pia wanandoa wengi wanaishi kwa mazoea.

love thé love or hâte thé love.....
 
Huyu atakuwa Mmama wa bongo movie kwani mimi Mama yangu hajawahi kuniambia haya hata siku moja, ni mke wangu tu huwa anakuwa na maneno machache uliyo andika humu so I guess katoa kwak au huko mitaani. Nikichelewa kurudi nyumbani utamsikia kakulisha nini leo? Simjibu kwani najuwa anamaanisha nani n nini lengo lake. Akiona sina jibu ananifuata chumbani na kunisachi change, akikuta hakuna utamsikia yaani baba wewe huna hata huruma, hela zote umemuachia yeye? Yaani ni full vituko....nikila na kuita watoto tule wote utamsikia, unawaitia watoto ili ukale kule? Yaani hapa sina hata hawara na sijafikiria kuwa naye kwani nampenda sana mke wangu ila vituko vyake tu ni muziki shinda Twanga Pepeta na ndicho kitakachonikimbiza kwake.
Utakuwa wa ubalozini wewe 99% ulilelewa na hausugeli
Karibia yote hayo yashanitokeaga pindi naishi na maza.
 
Nimechezea kichapo cha bi mkubwa mpaka basi. Nimekua mtu mzima sasa. Huwa akija kwangu namkumbusha alivyokua ananitwanga [emoji23]
 
Back
Top Bottom