Habari kaka.
Kuna dada nina shida nae, kuonesha nipo serious nimemwambia popote alipo niko tayari kumfata tuonane.
Mie nipo mitaa ya Ubungo.
Dada ameniambia anaishi Temeke Yombo. Amesema kama ni kuonana, basi isiwe mitaa ya mbali na Temeke. Yaani tusiende mbali. Anaishi kwao.
Mie Temeke sio mwenyeji, napajua Tandika kituo cha daladala na ile barabara ya kwenda Buza.
Naomba unielekeze Yombo iko pande gani. Yaani nafikaje.
Halafu kingine, maeneo ya huko Temeke kuna mahali tulivu naweza mpeleka mtu wangu tukakaa kwa ajili ya mazungumzo.
Wote hatunywi pombe.
Napenda sehem iwe na mandhari tulivu, romantic. Tuweze kuongea kwa utulivu, kisha giza likiingia nimrudishe kwao Yombo mie nirudi Ubungo.
Nisaidie mkuu. Nampenda sana huyu dada.
Kuhusu usafiri nina private car.