Tucheze michezo mipya

Stevutz92

New Member
Joined
Dec 31, 2021
Posts
0
Reaction score
1
Habarini jamani?

Naona Tanzania kuna fursa nyingi za kuanzisha klabu za michezo mingine, ukiachana na michezo kama football, boxing, basketball nk. Kuna michezo ambazo zinafaa kwa watu ambao labda football sio kipaji chao.

Na pia michezo hiyo inaweza kuchezwa katika jukwaa la kimataifa. Naongelea michezo kama lacrosse, water polo, handball, rowing nk.

Kwanini tusijaribu kuanzisha klabu za kuchezo michezo mingine kama hiyo na tuone tunaweza kuyafikisha wapi?

Nasubiri maoni yenu 🙏
 
Ni wazo zuri mkuu! Na hayupo wa kulipinga hili wazo lako zuri mkuu. Ila sisi wengine ngoja tuendelee na na football yetu mkuu!

Hayo masuala ya kupelekana usawa huu kwenye hiyo michezo mingine ya lacrosse, water polo, handball, rowing, nk. ni kuchoshana tu mkuu.
 
Sema Nini? Kuanzisha mchezo mpya Inahitaji uwekezaji wa halibya juu.
1.miundombinu.hapa Inahitaji viwanja na vifaa vya michezo
2.nguvukazi.Hapa TUNATAKA wachezaji na makocha.

Kuna michezo maarufu zaidi kama vile cricket,aRugby Tennis n.k.Michezo hii ni rais kupata makocha.pia tunaweza kuwa na mbionza pikipiki na magari,tukaweka viwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…