Tuchukulie umepata nafasi ya kuwa Rais kwenye nchi hii, Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, n.k. Je, ungewafanya nini?

Tuchukulie umepata nafasi ya kuwa Rais kwenye nchi hii, Waziri, Katibu Mkuu wa Wizara, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, n.k. Je, ungewafanya nini?

Capitrait

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2013
Posts
228
Reaction score
328
Hebu kulalamika na kulaumu tu pause kidogo.

Chukulia umepata nafasi ya kuwa Rais wa JMT, Waziri Mkuu, Waziri, Katibu Mkuu kwenye wizara, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Mbunge, Diwani, na kadhalika na kadhalika.

Ki ujumla we ni mtu uliyepo kwenye system na kuwa sehemu ya maamuzi kwa ajili ya nchi hii.

Je, ni kitu gani hasa ungefanya kwa ajili ya Tanzania na watanzania katika kukabiliana na changamoto mbali mbali zilizopo?

NB:
Maswali yanaruhusiwa kum challenge yeyote aliyejiweka kwenye nafasi tajwa hapo juu au nafasi yeyote ile yenye chain ya maamuzi kwa ajili ya nchi.
 
  1. Kama ningekuwa Rais ningetanguliza haki kwanza nisingeendekeza upendeleo wala nisingekubali kuendeshwa na mtangulizi wangu, ningesimamia zaidi haki, ningejali utu, ningezingatia matakwa ya katiba, ningemwomba Mungu anipe busara na hekima katika kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi.
  2. Waziri Mkuu - Ningetimiza majukumu yangu kwa kufuata kiapo changu, utendaji wangu ungekuwa kwa kuzingatia katiba
  3. Waziri - Ningefuata kiapo changu, nisingeendekeza rushwa wala upendeleo wa aina yoyote, nisingeiba fedha wala mali ya umma
  4. Katibu Mkuu kwenye wizara - Ningeridhika na stahiki zangu, tamaa kwangu ingekuwa mwiko
  5. Spika wa Bunge - Nisingetumia Katiba ya nchi kujisafishia chooni, ningejisafisha kwa karatasi ya kawaida au maji
  6. Jaji Mkuu - Haki
  7. Mbunge - Ningefanya mikutano na wapiga kura wangu ili kuchukua mawazo yao kila wakati kabla ya kwenda bungeni
  8. Diwani - Ningefanya mikutano na wapiga kura wangu ili kuchukua mawazo yao kila wakati kabla ya kwenda kwenye vikao vya madiwani
 
Spika wa Bunge ambae ni Job ndugai, ningemfilisi kila kitu, akawa kama alivyo zaliwa mtupu.. na ningeweka alama atae msaidia atakiona cha mtema kuni.. ningepiga pigo kama ambalo MfalmeNebukadneza alipigwa na Mungu kwa kushushwa chini hadi kula majani kama mnyama
 
Spika wa Bunge ambae ni Job ndugai, ningemfilisi kila kitu, akawa kama alivyo zaliwa mtupu.. na ningeweka alama atae msaidia atakiona cha mtema kuni.. ningepiga pigo kama ambalo MfalmeNebukadneza alipigwa na Mungu kwa kushushwa chini hadi kula majani kama mnyama
E buana eeehhhh kisa nini hasa?
 
  1. Kama ningekuwa Rais ningetanguliza haki kwanza nisingeendekeza upendeleo wala nisingekubali kuendeshwa na mtangulizi wangu, ningesimamia zaidi haki, ningejali utu, ningezingatia matakwa ya katiba, ningemwomba Mungu anipe busara na hekima katika kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi...
Duuuuu si mchezo yaani?
 
Kutawala kwa haki na demokrasia....mwaka watu wa 9....nawapa katiba mpya ...
 
Cha kwanza kabisa ningelivunja bunge.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
Hujielewi, uchaguzi mkuu hujumuisha kuchagua rais, wabunge na madiwani. Ukishinda unakuwa rais, Sasa ungevunja bunge gani? Au ukiwa rais wabunge hawataapishwa? Kumbuka bunge huvunjwa kila baada ya miaka mitano na kuitishwa uchaguzi mkuu.
Naona wewe unaongelea kufanya mapinduzi.
Nyumbu hovyo kabisa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Hujielewi, uchaguzi mkuu hujumuisha kuchagua rais, wabunge na madiwani. Ukishinda unakuwa rais, Sasa ungevunja bunge gani? Au ukiwa rais wabunge hawataapishwa? Kumbuka bunge huvunjwa kila baada ya miaka mitano na kuitishwa uchaguzi mkuu.
Naona wewe unaongelea kufanya mapinduzi.
Nyumbu hovyo kabisa.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Nyumbu ni matako ya mama yako

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza kabisa; NINGEKUWA RAIS WA JMT (URT).

1.Ningepunguza idadi ya wabunge (Majimbo ya uchaguzi). Ningeondoa wabunge wa viti maalumu.

2. Ningepunguza mishahara ya wabunge, ningeondoa posho zao zote, ningewawekea kodi kwenye mishahara yao. Pia wangekatwa makato ya NSSSF ili wakimaliza miaka 5 wapewe kiinua mgongo kulingana na walivyochangia. Ningekata hela ya bima za afya kwenye mishahara yao.

3. Ningewapumzisha watendaji wazee wote kwenye wizara zinazohusiana na technology hasa ya mawasiliano na viwanda.

4. Ningefuta nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, ningebaki na DAS na RAS tu ndyo wawe top wa wilaya na mikoa.

5. Ningebadilisha mitaala na muhtasari wa elimu yetu ya Tanzania kwa kuzingatia mabadiliko na mahitaji ya dunia ya leo. Ningejikita kumfundisha mwanafunzi skills za vitendo zaidi kuliko knowledge based on theories.

6. Ningekahikisha tunafanya mega prohect moja moja kila mwaka au baada ya miaka miwili.

7. Ningewapa nguvu sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji wa huduma za umma kama vile umeme, maji. Ningehamasisha uwekezaji kutoka nje kwa gharama nafuu sana ili baadae wawekezaji wakiwa wengi tatizo la ajira litapungua sana.

8. Ningepitisha sheria kama kiongozi wa umma amekula rushwa na ikathibitika basi adhabu yake ni kufirisiwa kila kitu na kwenda jela miaka 20.

9. Ningefanya mapinduzi ya kilimo (Agrarian revolution) kisha ningefanya mapinduzi ya viwanda kwasababu ningekuwa na uwezo wa raw materials za kutosha.

10. Nitafuata katiba na kuwaadabisha wote ambao watakaojiona hawawezekani.

11. Nitawatumia wafungwa wote nchini kuwa cheap labours ambao watafyatua matofari na kusaidia kujenga nyumba za watumishi wa umma (Walimu, Wanajeshi, Askari polisi na magereza, nk) nchi nzima. Ili kuondokana na tatizo la makazi duni kwa watumishi wa umma.

12. Ningeteua Waziri kulingana na ujuzi wa alichokisomea, uzoefu katika profession yake, weledi nk.

13. Ningehakikisha nakuwa na watumishi wa kutosha katika kila sekta (Afya, Elimu, Ujenzi, Technology, etc.)

14. Ningeweka wazi mikataba yote ya nchi inayoingia na wafadhili, wawekezaji, wahisani.

NAOMBA NIISHIE HAPA KWA LEO
 
Back
Top Bottom