Kwanza kabisa; NINGEKUWA RAIS WA JMT (URT).
1.Ningepunguza idadi ya wabunge (Majimbo ya uchaguzi). Ningeondoa wabunge wa viti maalumu.
2. Ningepunguza mishahara ya wabunge, ningeondoa posho zao zote, ningewawekea kodi kwenye mishahara yao. Pia wangekatwa makato ya NSSSF ili wakimaliza miaka 5 wapewe kiinua mgongo kulingana na walivyochangia. Ningekata hela ya bima za afya kwenye mishahara yao.
3. Ningewapumzisha watendaji wazee wote kwenye wizara zinazohusiana na technology hasa ya mawasiliano na viwanda.
4. Ningefuta nafasi za wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa, ningebaki na DAS na RAS tu ndyo wawe top wa wilaya na mikoa.
5. Ningebadilisha mitaala na muhtasari wa elimu yetu ya Tanzania kwa kuzingatia mabadiliko na mahitaji ya dunia ya leo. Ningejikita kumfundisha mwanafunzi skills za vitendo zaidi kuliko knowledge based on theories.
6. Ningekahikisha tunafanya mega prohect moja moja kila mwaka au baada ya miaka miwili.
7. Ningewapa nguvu sekta binafsi kushiriki katika uwekezaji wa huduma za umma kama vile umeme, maji. Ningehamasisha uwekezaji kutoka nje kwa gharama nafuu sana ili baadae wawekezaji wakiwa wengi tatizo la ajira litapungua sana.
8. Ningepitisha sheria kama kiongozi wa umma amekula rushwa na ikathibitika basi adhabu yake ni kufirisiwa kila kitu na kwenda jela miaka 20.
9. Ningefanya mapinduzi ya kilimo (Agrarian revolution) kisha ningefanya mapinduzi ya viwanda kwasababu ningekuwa na uwezo wa raw materials za kutosha.
10. Nitafuata katiba na kuwaadabisha wote ambao watakaojiona hawawezekani.
11. Nitawatumia wafungwa wote nchini kuwa cheap labours ambao watafyatua matofari na kusaidia kujenga nyumba za watumishi wa umma (Walimu, Wanajeshi, Askari polisi na magereza, nk) nchi nzima. Ili kuondokana na tatizo la makazi duni kwa watumishi wa umma.
12. Ningeteua Waziri kulingana na ujuzi wa alichokisomea, uzoefu katika profession yake, weledi nk.
13. Ningehakikisha nakuwa na watumishi wa kutosha katika kila sekta (Afya, Elimu, Ujenzi, Technology, etc.)
14. Ningeweka wazi mikataba yote ya nchi inayoingia na wafadhili, wawekezaji, wahisani.
NAOMBA NIISHIE HAPA KWA LEO