kson m
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 6,672
- 3,055
Kabla hamjazungumza na serikali mjitambue kuwa ninyi vyama vya wafanyakazi ni vitanzi kwa watumishi. Serikali inapoongeza mishahara bila huruma mnamnyoa kila mfanyakazi 2%ya huo mshahara. Mmefanya hivi miaka mingi na wafanyakazi hawaoni msaada wenu kwao. Nyie ni sawa na viwavi jeshi kwenye shamba la maharage. Hamna chembe ya huruma. Fikiria kila mwezi unamfyeka kila mtumishi wastani wa shs 30,000/-mmeanzisha vitega uchumi lukuki lakini faida haijulikani ni ya nani. Wengine na mabenki wanayo lakini bado wanawafyeka wafanyakazi michango. Hamweleweki hata kidogo. Mngekuwa na akili angalao kidogo mngepunguza rate za makato kufikia 1% au mkaweka fixed amount ambayo kila mtumishi atachangia kwenye chama cha wafanyakazi. Wafanyakazi wote wana haki sawa lakini wengine wanalazimishwa kuchangia zaidi kupitia hiyo%.chakamwata walikuja na sera nzuri kea watumishi lakini mliwapiga vita kila mahali kama vile nyie mna haki miliki ya wafanyakazi(walimu)hili laihusu zaidi CWT. Ondoeni unyonyaji wenu kwa watumishi ndio muwe na uhalali wa kuzungumzia mshahara wa wafanyakazi.Kaimu Katibu Mkuu wa TUCTA amesema wamefanya tafiti kubaini kiwango cha mshahara ambacho kinaweza kumtosha mtumishi kuendesha maisha yake.
Kutokana na Tafiti yao wamependekeza kiwango cha chini mshahara kiwe Tsh. 970,000 kutokana na gharama za maisha za sasa.
Hayo yamesemwa siku ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ambayo kitaifa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
View attachment 1770128
Pia soma: LIVE - Mei Mosi Mwanza: Rais Samia ahutubia, aahidi kuongeza mishahara kuanzia mwakani