TUCTA, TUGHE waishangaa CWT kuhusu kikokotoo cha PSSSF

TUCTA, TUGHE waishangaa CWT kuhusu kikokotoo cha PSSSF

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Siku chache baada ya wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kutaka mjadala wa kikokotoo urudi upya, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) limesema utaratibu wote ulifuatwa na suala hilo lilishafikiwa mwisho.

Kauli hiyo imekuja baada mkutano ulioshirikisha CWT na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuvunjika baada ya kuibuka kutokuelewana katika kiwango cha kikokotoo.

Baadhi ya wajumbe walimnyooshea kidole Kaimu Rais wa CWT, Dinah Mathamani, wakidai ameshindwa kuendesha kikao hicho.

Rais wa Tucta, Tumaini Nyamhokya alisema yanayotokea CWT hawezi kufahamu mitazamo yao ni ipi lakini suala la kikokotoo lilishapita na ni sheria.

“Sijui tunajadili nini kwenye sheria, tulishafuata taratibu zote hadi likafika hapo lilipofika. Masuala mengine ni masuala ya mtu mmoja katika chama siwezi kuwazuia wasiwaze lakini kama ni suala la utaratibu ulifuatwa na suala la kikotoo likafikia mwisho,” alisema.

Msimamo wa Tucta uliungwa mkono na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (Tughe), Rugemalira Rutatina akisema kupitia shirikisho hilo, wameshamalizana na Serikali kuhusu suala la kikokotoo, tatizo lililopo ni mifuko ya hifadhi ya jamii kutotoa elimu kwa wafanyakazi.

“Sisi tulishamalizana nao (Serikali) ila hawatoi elimu, watoke nje wakatoe elimu, watu waweze kuelewa, huo ndio mgogoro tulio nao. Lakini mambo ya kikokitoo sisi huko tulishatoka,” alisema.

Alipoulizwa nini mkakati wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi (PSSSF) kutoa elimu juu ya kikokotoo hicho baada kugonga mwamba CWT juzi, Meneja Uhusiano na Elimu kwa wanachama wa mfuko huo, James Mlowe aliahidi kulitolea ufafanuzi suala hilo leo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (THTU), Dk Paul Loisulie, alisema hata kwao bado kuna vuguvugu halijapoa watu wametulia tu lakini iko siku wataibuka.

Alisema inahojiwa kwa nini wabunge wapewe mafao yote lakini wafanyakazi wapangiwe kiwango cha kupewa na kwanini mifuko ya hifadhi ibaki na fedha yao nyingi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Dk Joseph Mhagama alisema kabla ya Mei Mosi mwaka huu, Serikali iliieleza kamati hiyo kuwa wamekubaliana na wadau waliridhika na kikokotoo hicho kipya ambacho ni asilimia 33.

“Maoni yangu ni kwamba ieleweke uamuzi ulifanyika collectively (kwa ushirikiano), kwa maana kulikuwa na mashauriano, haukuwa uamuzi wa upande mmoja, maana yake Serikali ilikaa na wadau na kufikia mwafaka wa asilimia 33,” alisema.

Dk Mhagama alisema ni vyema kama hawajaridhika (CWT), Serikali ione umuhimu wa kufanya mashauriano na wadau ili kupata uelewa wa pamoja kuhusu hatua hizo zilizochukuliwa.

Kwa upande wake Dinah alisema kabla ya kukutana mwezi ujao katika Mkutano mkuu wa CWT, watamweleza Waziri mwenye dhamana hisia za wanachama kuhusu kikokotoo. Hata hivyo, alisema baada ya kutangazwa kwa kikokotoo hicho kipya Mei mwaka huu, jambo hilo limefanyiwa kazi kwa muda mrefu na wameshirikishana.

“Kwa upande wetu ambao kikokotoo kilikuwa asilimia 50 na kushushwa kuwa asilimia 33, nadhani tutapata mshtuko lakini hali ndivyo ilivyo kwa kuwa tumeelezwa kwanini tumefikia hapa na faida zake bila kujali waliokuwa asilimia 50 au asilimia 25 lakini kubwa ni mifuko kuwa endelevu,” alisema.

MWANANCHI
 
Inasikitisha sana.waalimu jiteteeni wenyewe.
 
Haiwezekani mtumishi astaafu umpe 33% ya mafao yake, kwa walimu ambao wana mishahara midogo 33% ya pensheni inaweza isifike hata milioni 15.
Hajazoea shika hela nyingi amezoea kupewa hela kidogo kidogo ya kula acha apewe ama awe na uhakika wa kula mpaka kaburini.

Security Ni kubwa kuliko kuchukua nyingi then ananunua fuso inapiga mweleka chini.
Kuna job game and business game hizi Ni two quite different battle field. Na huwezi zimasta zote mpaka zikafikia level ya kuwa Ile intuitively ama part of who you're,or second nature Ni ngumu mno.

Mastery of any craft takes massive and massive of time, energy, courage, warrior mindset, sweat, blood, dedication and deliberate practice,high commitment mpaka ufike level ambayo you're being admired as a role model of young peers.
 
Mifumo imewekwa kumnyonya mtumishi. Why unitunzie hela so Bora uninunulie nyumba nipangishe nakuwa nalipa kidogokidogo mpaka nakuja kustaafu nakuwa Nina nyumba zangu Kama tano napangisha nakula ama hapo serikali hainipendi.
 
Moja ya sheria za kipuuzi chini ya utawala wa ccm ni hii ya kikokotoo. Yaani hela ni ya kwangu, halafu unaipangia matumizi!

Katika hali ya kustaajabisha, Wabunge kila baada ya miaka 5 tu wanachukua mafao yao yote! Tena zaidi ya milioni 250!

Wakati huo huo mtumishi mwingine wa serikali aliyefanya kazi kwa miaka zaidi ya 30, unampa 33% ya mafao yake, huku 67% yake iliyobakia unakaa nayo kilazima!!

Kwa nini wasitoe option kwa watumishi? Kama kuna anayetaka hiyo 33% ya kikotoo angepewa! na kama kuna anayetaka 100% ya mafao yake naye apewe!

Ujinga wa ajabu kabisa huu.
 
Wasifanye watumishi hawana akili za kusimamia pesa zao wenyewe, kwa nini wabunge wanachukua zile milioni 200 zote baada tu ya miaka mitano na hakuna anayewapangia matumizi?

Huyu mtumishi aliyesota miaka 30 leo ashindwe kumudu kutumia mafao yake? afterall akishindwa ku-manage pesa zake wao linawauma nini.

Hii ni kuendelea kuwafanya watumishi kuendelea kuwa maskini na wanashindwa hata kuwekeza kwa ajili ya watoto wao, maana pesa wanayotegemea waifanye kama mtaji wa uwekezaji wanapewa kiduchu walimu simamieni hapohapo msiyumbishwe na hawa tucta, sijui tughe huenda wao wamelamba asali....​
 
Nyamhokya kashachukua chake mpumbavu yule..

Haiwezekani mtumishi astaafu umpe 33% ya mafao yake, kwa walimu ambao wana mishahara midogo 33% ya pensheni inaweza isifike hata milioni 15.
Nyamhokya ni likada la CCM linatetea tumbo lake. Naliombea lile lishibe, lipate ugonjwa moyo lidondoke ghafla life hata leo hii. Qumer ya mama yake!
 
Back
Top Bottom