Elections 2010 TUCTA yajibu kauli ya JK

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
TUCTA lakebehi kauli ya JK
Monday, 23 August 2010 11:48
Na Job Ndomba,Jijini wa Dar Leo

SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limesema kwamba kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa ni matusi kudai kuwa hajali wafanyakazi shirikisho hilo limeibuka na kudai kuwa hizo ni kampeni.

Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.

"Siwezi kutoa maoni yoyote kuhusiana na kauli za kampeni alizozitoa Rais Kikwete na kwamba tumuache aendelee na kampeni zake nasi tunasubiri kupiga kura Oktoba 31, mwaka huu, " amesema katibu huyo.

Jana Rais Kikwete alisema kuwa ni matusi kuambiwa kuwa hajali maslahi ya wafanyakazi nchini wakati serikali yake imekuwa ikiboresha maslahi yao mwaka hadi mwaka.

Pia alisisitiza kwamba ataendelea kuwaheshimu wafanyakazi na serikali yake itaendelea kuboresha stahili zake na kuahidi kuboresha zaidi katika kipindi cha miaka mitano.

Sanjari na hayo Rais Kikwete alisema anataka kuweka rekodi ya kukumbukwa kwa mema yake katika uongozi wake na si vinginevyo.

Aidha akiendelea kuwaomba kura wananchi wa Jiji la Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba alisema hatendewi haki kuhusiana na maslahi ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani mwaka 2005 na Serikali yake ilikuwa ikifanya hivyo kulingana na nafasi.

Hata hivyo alisema serikali isingeweza kuwadanganya wafanyakazi kuwa kiwango walichokuwa wakikihitaji cha Sh.315,000 kuwa hakiwezekani lakini serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na uwezo wa bajeti yake.
 
Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.
Kauli hii ya TUCTA ndiyo niliyokuwa naisubiri wamwache tu aendelee kujikaanga mwenyewe kwa vile najua hatakuwa na majibu ya kuwaridhisha wafanyakazi, watakuwa wanamchekea tu kila apitapo. Watu wanadhani watanzania ni wajinga lakini si kiasi hicho, na mjinga akishaelimika humzidi hata mwalimu wake.
 
Swaafi...mwacheni ajichanganye mwenyewe kwanza...nataka staki
 
Heri wajikalie kimya maana vinginevyo, watakwenda mezani wakiwa na Plaster kichwani.

Hivi hili la Plaster na lenyewe kasingiziwa?
 
Hio nzuri, muacheni abwate sisi msimamo wetu uko pale pale, kuwa oktoba kisanduku cha kupigia kura ndicho kitasema.CHADEMA oyeeeeeeee.
 
Heri wajikalie kimya maana vinginevyo, watakwenda mezani wakiwa na Plaster kichwani.

Hivi hili la Plaster na lenyewe kasingiziwa?

Kama haya maneno yamechapwa vyema Mkuu alisema hivi kuhusu plasta:

"Sasa hata hatujazungumza wameanza kutangaza mgomo, sasa afadhali tuzungumze kwanza maana mgomo una kasheshe zake, mkigoma hamtaachwa, askari watawapiga virungu na hata wengine kuweza kupoteza maisha, mimi naweza kuwa rahim lakini polisi mkiwafanyia fujo watawatwanga na hata mkigoma baadaye mtarudi kwenye mazungumzo mkiwa na plasta midomoni"

Nimekuwa najiuliza alimaanisha wakirudi watakuwa wamenyamazishwa au?
 
Hata hivyo alisema serikali isingeweza kuwadanganya wafanyakazi kuwa kiwango walichokuwa wakikihitaji cha Sh.315,000 kuwa hakiwezekani lakini serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na uwezo wa bajeti yake.

Duu! Kumbe siku ile alitakiwa awe na akili kama ya leo?!! Kweli akili ya kuandikiwa hotuba bila kuipitia kabla na kuielewa,"CHANGANYA NA YA KWAKO"jamaa hakumbuki kabisa kama aliwahi kuongea na WAZEE wa Dar es salaam
 
tuje kufumbuka akili kwamba tupige kura kwa mtu binafsi kwa kumchuja na kumdadisi,na si chama!!
kazi ipo:confused2:
sisi tunasikiliza mawaidha ya kila mgombea wa vyama vyote,then Octoba 31 tunajua wapi tuweke kura zenu bila mtutu wa bunduki
 
Hongera Mgaya. Don' argue with a f.........l
 
the ccm presidential runner is somehow ignorant of thinking,
so we've to lieve him as idiot.
 
This is a series of loose and capture game...Akiingia ikulu atasahau tena kauli zake sa sasa!...Nadhani huyu tatizo lake si kuanguka-anguka tu majukwaani, bali hata kumbmukumbu zake zina mushkeli wa kutisha!
 
au kaasinngiziwa...kama alivyodai yule rafikie....." nimeonewa sana....nimenyanyaswa sana

Ndo hao hao
 
Plasta midomoni na plasta kichwani mimi naona ni kitu kimoja maana virungu vya FFU huwa havina macho, bora Mgaya ujinyamazie aliyelianzisha atalinywa mwenyewe.
 
Kiukweli babu kachoka hata ukiangalia picha za wakati anapokelewa mwanza anaonekana mchovu, ila piga ua maneno ktk kisanduku. Atawakumbuka mbayuwayu
 

Siyo kampeni tu, bali pia ni kutoa hongo pale alipoongeza mishahara kiduchu kimya kimya. Kwa nini asitangaze? Hiyo ni rushwa kwa wafanyakazi kwani amengojea hadi kampeni zinaanza ndiyo imejulikana kaongeza! NEC kazi kwenu, huyu mtu atakiwa kuwa disqualified!
 
"Siwezi kutoa maoni yoyote kuhusiana na kauli za kampeni alizozitoa Rais Kikwete na kwamba tumuache aendelee na kampeni zake nasi tunasubiri kupiga kura Oktoba 31, mwaka huu, " amesema katibu huyo.
To me this is a professional answer, aliposema 'siwezi kutoa maoni....tunasubiri Oct.31' unaweza fikiri hajatoa ujumbe kwa wafanyakazi kumbe ni ujumbe uliojitoshereza.
 
Mgaya umenifurahisha sana. ULISHASEMA mtu hataki pilau letu tumpe anaetaka!!! Si akili za kuambiwa tukichanganya na za kwetu tunawapata CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…