TUCTA lakebehi kauli ya JK
Monday, 23 August 2010 11:48
Na Job Ndomba,Jijini wa Dar Leo
SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) limesema kwamba kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuwa ni matusi kudai kuwa hajali wafanyakazi shirikisho hilo limeibuka na kudai kuwa hizo ni kampeni.
Akizugumza na gazeti hili leo asubuhi Katibu wa shirikisho hilo Nicholaus Mgaya amesema kuwa hivi sasa hawatatoa maoni yoyote zaidi ya kumwacha aendelee na kampeni zake.
"Siwezi kutoa maoni yoyote kuhusiana na kauli za kampeni alizozitoa Rais Kikwete na kwamba tumuache aendelee na kampeni zake nasi tunasubiri kupiga kura Oktoba 31, mwaka huu, " amesema katibu huyo.
Jana Rais Kikwete alisema kuwa ni matusi kuambiwa kuwa hajali maslahi ya wafanyakazi nchini wakati serikali yake imekuwa ikiboresha maslahi yao mwaka hadi mwaka.
Pia alisisitiza kwamba ataendelea kuwaheshimu wafanyakazi na serikali yake itaendelea kuboresha stahili zake na kuahidi kuboresha zaidi katika kipindi cha miaka mitano.
Sanjari na hayo Rais Kikwete alisema anataka kuweka rekodi ya kukumbukwa kwa mema yake katika uongozi wake na si vinginevyo.
Aidha akiendelea kuwaomba kura wananchi wa Jiji la Mwanza katika Uwanja wa CCM Kirumba alisema hatendewi haki kuhusiana na maslahi ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani mwaka 2005 na Serikali yake ilikuwa ikifanya hivyo kulingana na nafasi.
Hata hivyo alisema serikali isingeweza kuwadanganya wafanyakazi kuwa kiwango walichokuwa wakikihitaji cha Sh.315,000 kuwa hakiwezekani lakini serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na uwezo wa bajeti yake.