Nikweli kabisa mkuu mimi nadhani watu hawafikirii adha na kejeli tunazokutana nazo kwa hawa wake zetu..
Just imagine umeoa then tangu uoe mwanamke hajawahi kufurahia mchezo unafikiri aibu gani unapata...
Aaa aaaaa aaaa, Mkuu @Bwanamisitu pole sana, unatia huruma yaani nakuona vile unavyopata maumivu moyoni, pole mtu wangu. Nilikua nasoma tuu comment na kupita ila niliposoma hii comment ya kwako nimehuzinika sana.
Ngoja tupeana ushauri kidogo, kabla sijakwambia kitu gani ufanye; ngoja nijaribu kuweka ama kuuliza masuala yatakayosaidia kufahamu kiini cha tatizo lako. Utajijibu kimoyomoyo mwenyewe huko.
Jiangalie kama tatizo lako liko la kitabia, yaani uliwahi kujihusisha kupiga puu ama kujichua siku za nyuma kabla ya kuoa? Kama ni hivyo maana yake tatizo lako ni la kisaikolojia na kimwili hivyo utadeal nalo katika kujibiidiisha kuachana na hiyo tabia kama bado unayo na kuweka fiti kwa mazoezi ya mwili jumla na mazoezi ya kuukanda uume ili uindoe ulegevu wake na hatimae kuwa imara wakati wa kufanya tendo. Aidha, unatakiwa kula vyema na kupumzika vya kutosha. Ondoa wasiwasi na wahaka wakati ukijiandaa katika kufanya mapenzi na mwenzio.
Hapa panapo kula vizuri nataka nikutajie walau aina fulani fulani za vyakula ambavyo mm binafsi huwa natumia kama chakula na sio kama dawa, (yaani nakula kiasi kidogo kila siku) lozi ama almound, aina hii ya njugu imefanyiwa utafiti sana na watafiti duniani na imegundukllika kuwa huwa inaweka sawa na kuimarisha uimara wa mbegu za kiume na kumfanya mtumiaji awe na "sexual stamina" ambapo humuwezesha awe muamuzi wa muda gani anataka kuwaruhusu wagiriki kushuka.
Kwa utafiti wanapendekeza ule kiasi cha kigao kimoja cha mkono, yaani walau upate punje za lozi 10 hadi 15 kwa siku kwa matokeo mazuri. Kwa sababu sijajiandaa sitaweka rejea za hizi tafiti kwa sasa. Naweka tuu hii link unaweza kujisomea kidogo, kama unataka kusoma tafiti za kisayansi unaweza ukagoogle zipo za kutosha huko mjtandaoni. Naamini utafanikiwa inshaalah.
Eating a handful of almonds daily can reduce belly fat, waist circumference, leg fat and improve a man's sperm count and quality..
Chakula chengine ni mronge, ule mti wenye vijani vidogovidogo ambao huwa unakuwa mkubwa kiasi. Huu nitajuwekea faida zake tu maana unatumika katika namna tofautitofauti.
Wengine hutumia kama mboga, chai na tunda zake huliwa, mm binafsi nilkshawahi kutumia kwa kunywa chai ya majani ya mronge na wakati mwengine huwa najikuta natafuna zile mbegu zake na kunywa na maji yabkutosha kama masihara tuu na si kwa lengo hasa ya kurudisha hamasa ya tendo ila faida huiyona baada ya muda mdogo sana.
Nenda kajifunze kuhusiana na matumizi mazuri ya mronge katika kuimarisha afya ya uzazi kwa mwanaume.
Jichunguze kama tatizo lako linasababishwa na shida za kijini ama mapepo, ukijijua uko hivyo jitafutie tiba haraka kupitia mrengo wa imani yako, maana haya mapepo yanachangia kwa kiasi kikubwa binaadamu kuharibikiwa katika mambo yake ya kimapenzi.
Pole sana mtu wangu, Mungu yuko pamoja nasi. Tusikate tamaa na maisha ya duniani, Mungu katuwekea starehe ile ili tutulize nafsi na miili yetu kupitia viumbe wenzetu wa kike nao kutuliza hisia zao kupitia sisi, sasa inapofika wakati ikiwa mwanaume ama mwanamke hapati kitulizo cha aina ile binafai huwa napata huzuni sana. Maana ndio starehe pekee ambayo maskini na matajiri hupata namna moja ya utamu kutegemeana na jinsi utavyojitahidi kuweka sanaa utakayo.
Ooohhhhh pole sana mtu wangu.
Sent using
Jamii Forums mobile app