Mangaline
JF-Expert Member
- May 19, 2012
- 1,045
- 221
Katika mchakato unaoendelea wa uteuzi wa wajumbe wa kamati ya kata ya katiba mpya, tumehamasishwa vya kutosha, na bahati nzuri au mbaya tumechaguliwa katika ngazi za Vijiji kuwa miongoni mwa watakao kwenda katani kugombea ujumbe wa kamati ya katiba ya kata. Kwa bahati mbaya zaidi, misukumo ya kugombea kuwa mjumbe, ilikuwa zaidi kiitikadi za vyama na pengine dini. Ninachofahamu, yako mengi zaidi ya itikadi za vyama na udini. sasa yapi mengine ambayo ni muhimu zaidi katika mchakato wa kupata katiba tunayoitaka, ili tujiandae na kujielimisha ili tuyatetee kwa nguvu zote??? Nahitaji constructive comments tafadhali.