Hoja ya kibatala ambayo nimeielewa ni kuwa walikuwa na mdadi wa kuionyesha mahakama kuwa yule "Inspekta John" siyo Askari.
Na wao walitaka waimalize kesi kwa kuonesha nwenye ushahidi wa msingi ni mtu anayetiliwa shaka utambulisho wake na uadilifu wake.
Leo wangemalizana na huyu shahidi, basi kungekuwa hakuna tena haja ya huyo "shahidi mtaalam" kuja mahakamani kutoa ushahidi.
Kwa hivyo waendesha mashitaka wameona Bora aje kwanza mtaalam halafu mwenye ushahidi wa msingi ndipo aje ahojiwe na kina kibatala.
Kwa mtazamo wangu ni kwamba upande wa mashitaka wanatumia "technicalities" kurefusha mashtaka bila ya sababu za msingi.