Tuelimishane: Malengo ya kuteua balozi bila kumpa nchi ya Ubalozi ni nini hasa

Tuelimishane: Malengo ya kuteua balozi bila kumpa nchi ya Ubalozi ni nini hasa

Ngwanakilala

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
774
Reaction score
1,467
Wakuu

Waasalam. Naomba tujaribu kuelimishana kidogo hasa kwa wale wajuzi wa masuala ya kidiplomasia. Malengo ya Kuteua Balozi Bila Kumpa Nchi ya Ubalozi ni Nini Hasa? na majukumu yake yanakua yepi? na je anakua na mshahara wa ziada kwa kazi hiyo na boss mwengine pia wizara ya mambo ya nje?

Nimejaribu kuangalia definition ya Ambassador lakini haikunipa mwanga wa kutosha

a diplomatic official of the highest rank, sent by one sovereign or state to another as its resident representative (ambassador extraordinary and plenipotentiary).

a diplomatic official of the highest rank sent by a government to represent it on a temporary mission, as for negotiating a treaty.

a diplomatic official serving as permanent head of a country's mission to the United Nations or some other international organization.


an authorized messenger or representative. Abbreviation: Amb., amb.
 
Nchi fulani [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kupata hadhi ya kibalozi akiwa nchni,pia kubaki kwenye utumishi wa serikali.Ila natamani Rais aniteuwe ujue !hivi mwananchi wa kawaida Msomi rais hawezi kumteua ?au lazima uwe mtumishi au mwanasiasa.Rais uje mtaani basi ututeue na sisi
 
Nadhani aliyemteua anakuwa anajua anaenda nchi Fulani ila hawezi kuambiwa au taarifa kuwekwa wazi kwakua taarifa zake zinatumwa kwanza nchi anayokwenda kwa ajili ya vetting wakimkubalia ndio anapelekwa

Tusubiri mawazo ya wengine.
 
Wapo watu hua wanateuliwa kua mabalozi lakini wanabaki hapa nchini kwamfano wakurugenzi wengi wizara ya mambo ya nje wanateuliwa kua mabalozi hata wakuu wa itifaki ni hivyo hivyo lakini wao hawapangiwi nchi. I wonder why is it necessary kwao kua mabalozi
 
Nadhani aliyemteua anakuwa anajua anaenda nchi Fulani ila hawezi kuambiwa au taarifa kuwekwa wazi kwakua taarifa zake zinatumwa kwanza nchi anayokwenda kwa ajili ya vetting wakimkubalia ndio anapelekwa

Tusubiri mawazo ya wengine.
Nchi anayokwenda ndiyo inafanya vetting?! Sasa sisi tuna waapishaje kabla ya vetting huko waendako?! Na huwa inamfanyia vetting peke yake, na kwanini sisi ndio tuwachagulie mtu ikiwa wao ndio huchukua qualified candidates?!
 
Nchi anayokwenda ndiyo inafanya vetting?! Sasa sisi tuna waapishaje kabla ya vetting huko waendako?! Na huwa inamfanyia vetting peke yake, na kwanini sisi ndio tuwachagulie mtu ikiwa wao ndio huchukua qualified candidates?!
Sijajua kwanini inakuwa hivyo lakini balozi alieyeteuliwa jina lake lazima liende huko na wao ndio wataleta jibu kama wamemkubali au la na hawalazimishwi kutoa sababu za kumkataa.

Kuna Uzi humu umeelezea kwa kina,nimechukua baadhi ya maelezo.

''Ndiyo maana ibara ya 4 (1) imesisitiza kuwa, "Nchi iliyomtuma balozi ni muhimu ijiridhishe kuwa nchi iliyotarajiwa kumpokea balozi imemkubali mteule huyo." Kitendo hiki kwa lugha ya kidiplomasia huitwa agremo/a.

Ibara hiyo hiyo ya 4 (2) imeweka onyo kuwa, "Nchi inayompokea Balozi haipaswi kueleza sababu za kumkataa mteule tajwa (Persona non grata)."
 
Baadaye utasikia tunatuma mabalozi kwenye vyama vya upinzani tukibaini wale wanaotupinga wamefanya maamuzi ya kutuunga mkono maana kwa uchumi huu lazima kila mzalendo aonje keki
 
Back
Top Bottom