Tuelimishane: Mapinduzi ya kijeshi hupangwa na kufanyika vipi ili hali majeshi huwa na vikosi vingi tena sehemu tofautitofautoi za nchi?

Status
Not open for further replies.

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wote ni mashuhuda wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Afrika kwa nyakati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikiamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaidi huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua Serikali?

Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant tena akiwa na askari 17 tu.

Mwenye uelewa atusaidie.
 
Swali zuri sana. Mapinduzi hufanikiwa kama anayefanya mapinduzi huwa anakubalika na vikosi vingi kama siyo vyote ie awe na COMMANDING HEIGHTS IN THE ARMY.

Anaweza asiwe Mkuu wa Majeshi akawa mtu mwingine mwenye influence kubwa na bahati ya kupendwa na wanajeshi.

Mfano Lisu hana mamlaka lkn ametokea watu kumkubali, kwenye nchi ya tume huru, Lisu kesho anakuwa Rais!.....
 
Swali zuri sana. Mapinduzi hufanikiwa kama anayefanya mapinduzi huwa anakubalika na vikosi vingi kama siyo vyote ie awe na COMMANDING HEIGHTS IN THE ARMY. Anaweza asiwe Mkuu wa Majeshi akawa mtu mwingine mwenye influence kubwa na bahati ya kupendwa na wanajeshi. Mfano Lisu hana mamlaka lkn ametokea watu kumkubali, kwenye nchi ya tume huru, Lisu kesho anakuwa Rais!.....
Anaanzaje kukubalika na wenye madaraka wanamuona tuu? Kwamba huko hakuna inteligenjia?
 
Swali zuri sana. Mapinduzi hufanikiwa kama anayefanya mapinduzi huwa anakubalika na vikosi vingi kama siyo vyote ie awe na COMMANDING HEIGHTS IN THE ARMY. Anaweza asiwe Mkuu wa Majeshi akawa mtu mwingine mwenye influence kubwa na bahati ya kupendwa na wanajeshi. Mfano Lisu hana mamlaka lkn ametokea watu kumkubali, kwenye nchi ya tume huru, Lisu kesho anakuwa Rais!.....
Kwahiyo kiongozi wa kiraia anaweza kupanga mapinduzi ya kijeshi?
 
Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?

Kwa mfano, Samweli Doo aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.

Mwenye uelewa atusaidie.
Subiri Rushwa ishike kila idara, kila mtu afanye analotaka fanya, Rais awe na makundi ya wapigaji na mwisho Rais awe na ushirikiano binafsi na viongozi wa mataifa fulani hapo ndipo utajuwa hujuwi kama jeshi linawezaje.
Ila nikukumbushe jeshi ndio hutawala nchi wakati wote na ndio maana Kuna yule jamaa nyuma ya Rais. Kwaheri
 
Kwa kifupi

Mapinduzi ya Kijeshi mara nyingi huwa na mazingira ambayo asilimia kubwa ya Jeshi huwa wapo tayari kuyaunga mkono.
Ikiwa sivyo lazma jaribio lifail.
Nchi nyingi tu majaribio hufail,au likifanikiwa na hakuna consensus ndo inakuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Mfano wakati wa Magufuli majaribio yamefeli Mara 2 japo haikujulikan sana
 
Ngoja mimi nichangie in my point of view. Nadhani ni kitu hupangwa kwa maana wakuu wa vikosi hujua nini kinaendelea hivyo anatafutwa yule most trusted na loyal mjeda ambaye huwa hana cheo kikubwa sana na asiyedhaniwa ndio anakuwa kama ignition ya ku initiate coup akiwa anapewa full back up na ma big boys ndani ya jeshi .Na pia anayeanzisha coup anakuwa kama chambo ili when things goes wrong wale big boys walio ndani ya jeshi wawe katika safe haven kuepuka kushtakiwa na kutiwa hatiani.
 
Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?

Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.

Mwenye uelewa atusaidie.
Kama unaonegelea mapinduzi ya Afrika magharibi, yanasabishwa na ubaguzi wa ukabila tu. Hakuna zaidi.

Na mapinduzi yote ya Afrika ukiyatazama utaona yamesababishwa na ubaguzi tu, hakuna zaidi.

"Divide and rule" inatumika na tunaotumika kupinduwana kuuwana na kuchukiana ni Waafrika wenyewe kwa ujinga wetu.
 
Kwa kifupi

Mapinduzi ya Kijeshi mara nyingi huwa na mazingira ambayo asilimia kubwinea ya Jeshi huwa wapo tayari kuyaunga mkono.
Ikiwa sivyo lazma jaribio lifail.
Nnchi jingi tu majaribio hufail,au likifanikiwa na hakuna consensus ndo inakuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Kwakweli ni lazima sehemu kubwa ya Jeshi kama sio Jeshi lote liunge mkono mapinduzi vinginenyo civil war haikwepeki.

Mpaka kufikia hatua kama hii, ni wazi watawala wa kiraia watakuwa wamefanya madudu mengi sana kiasi kwamba wanajeshi nao wanakuwa wamechoka hivyo akitokea Jasiri wa kuanzisha mapinduzi inakuwa rahisi kuungwq mkono na jeshi lote au sehemu kubwa ya jeshi.
 
Ngoja mimi nichangie in my point of view. Nadhani ni kitu hupangwa kwa maana wakuu wa vikosi hujua nini kinaendelea hivyo anatafutwa yule most trusted na loyal mjeda ambaye huwa hana cheo kikubwa sana na asiyedhaniwa ndio anakuwa kama ignition ya ku initiate coup akiwa anapewa full back up na ma big boys ndani ya jeshi .Na pia anayeanzisha coup anakuwa kama chambo ili when things goes wrong wale big boys walio ndani ya jeshi wawe katika safe haven kuepuka kushtakiwa na kutiwa hatiani.
Ndio maana ukimsikiliza Traore anasema eti waliyokubaliana na kina Daniba hakuyafanya inavyotakiwa Kwa hiyo hupangwa.

Ila ni Nchi Zenye intelligence dhaifu ndio haya mambo Huwa rahisi.
 
Mapinduzi mengi kama sio yote yana backup ya mageneral wa vikosi kadhaa kama sio vyote.

Mapinduzi anaweza fanya askari yoyote as long as yana backup gani nyuma ?!.
 
Kwahiyo kiongozi wa kiraia anaweza kupanga mapinduzi ya kijeshi?
Wanapanga sana tuu ila kama ana uungwaji mkono mkubwa wa jeshi eg Venezuela,Argentina,Turkey kule Majaribio ya Wapinzani yalifeli japo yalikaribia ila ni lazima kuwe na external Support.

Hakuna mapinduzi ya Afrika yakawa hayana uungwaji mkono wa Nje,hayapo.
 
Mapinduzi yana options mbili tu ya faulu uunde serikali au ya fail uunde kundi la uasi au uwe executed wewe na kikosi chako.

Nchi za kijamaa au zenye chembechembe za ujamaa kihistoria zimeweka jeshi ndani ya chama, chini ya chama au katika uangalizi kamili wa chama kuna nchi ipo Afrika imefanya hivi😄.
 
Wote nii mashuhudaa wa taarifa za mapinduzi ya kijeshi sehemu mbalimbali duniani hasa Africa kwa nyalati za sasa.

Binafsi nimekuwa najiuliza haya mapinduzi huwa yanafanyikaje ili hali Jeshi huwa lina askari wengi tena katika sehemu mbalimbali za nchi.

Kwa mfano, kikosi au vikosi katika mji mkuu wa nchi vikoamua kuasi, vikosi katika maeneo mengine ya nchi vina nafasi gani katika kuzima uasi?

Kwa maneno mengine, inawzekana vipi uasi ufanywe na kikosi au vikosi vichache then Jeshi lote mara moja liwe chini ya kiongozi mmoja wa haya mapinduzi?

Na zaid huwa inawezekana vipi wanajeshi wa vyeo vidogo tu kupindua serikali?

Kwa mfano, Samweli Doe aliongoza uasi akiwa na cheo kidogo to tu cha Sergeant.

Mwenye uelewa atusaidie.
Kila nchi kuna Mzee, huyo mzee ndiyo kila kitu, yeye ni zaidi ya rais, yaani yeye ndiye mamlaka! Hata Tz yupo hata Kenya yupo. Yaani akisema kitu fulani kifanyike basi lazima.
 
Wanapanga sana tuu ila kama ana uungwaji mkono mkubwa wa jeshi eg Venezuela,Argentina,Turkey kule Majaribio ya Wapinzani yalifeli japo yalikaribia ila ni lazima kuwe na external Support.

Hakuna mapinduzi ya Afrika yakawa hayana uungwaji mkono wa Nje,hayapo.
Mapinduzi yanaweza kuwa yana support ya ndani bila support ya nje Kama jeshi lipo kwenye ulaji mkubwa.

Pia michezo michafu ndani ya vyama tawala wanaweza tengenezeana mapinduzi hasa wale walio tolewa nje ya mfumo hii michezo ipo sana Afrika
 
Ndio maana ukimsikiliza Traore anasema eti waliyokubaliana na kina Daniba hakuyafanya inavyotakiwa Kwa hiyo hupangwa.

Ila ni Nchi Zenye intelligence dhaifu ndio haya mambo Huwa rahisi.
Yeap nakubaliana nawe . Intelligence ikiwa weak lazima liwakute jambo . Na pia moles ni changamoto sana .
 
Mapinduzi yanaweza kuwa yana support ya ndani bila support ya nje Kama jeshi lipo kwenye ulaji mkubwa.

Pia michezo michafu ndani ya vyama tawala wanaweza tengenezeana mapinduzi hasa wale walio tolewa nje ya mfumo hii michezo ipo sana Afrika
Mapinduzi ya Africa Huwa ni upuuzi kuliko faida Wala hawapindui Kwa maslahi ya Nchi Bali ya kwao.

Mfano hapo Niger huyu Kiongozi wa Mapinduzi alimegewa ubuyu kwamba Rais anapanga kumpiga Chini kumbe akamuwahi Sasa huu ni upuuzi wanaoshangilia Huwa ni manyumbu wasioelewa wanachoshangilia.

Kiufupi Wanasiasa wanaweza furahia hasa wa upinzani wakidhani kwamba wanaweza pata fursa ila ni ngumu.

Pia angalia Egypt baada ya Upinzani kushinda na Jeshi haliwataki wakaipundua hivyo hivyo na MynMar.

Ndio maana Huwa napinga mapinduzi ya Afrika mama nafahamu Huwa ni upuuzi wa kugombea vyeo Wala sio Kwa maslahi ya Nchi na matokeo yake watu wataanza ku suffer.

Hatari ya jeshi ni kwamba wao wanaamini kwenye matumizi ya Nguvu na hakuna wa kuwauliza ndio maana Huwa sitaki hata kidogo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom