Matokeo ya kidato cha nne yamesikisha wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wameyasemea kwa uchungu sana na wengine kufikia hata hatua ya kudai tukio hilo litangazwe kama janga la kitaifa. Kati ya wanaonyesha kusikitishwa na kufadhaishwa na matokeo hayo kuna baadhi wanaongea ukweli wa kile wanachokifeel from the bottom of their hearts lakini kuna wengine wanaonyesha kusikitika wakati tukijaribu kuwaangalia kwa undani kiukweli ni kwamba wanatucheka na kutubeza. Nasema hivyo kwa sababu shule nyingi zilizofanya vizuri yaani Div 1-3 ni zile za private. Kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo ni watoto wa viongozi na watoto wa watu wenye vipato vikubwa ndani ya jamii. kwa upande mwingine shule za kata ambazo ni za serikali zilizotoa division ziro kwa kiasi kikubwa ndizo wanaosoma watoto wa wananchi wa kawaida amabao wengi ni masikini. Tukifanaya uchambuzi wa kimantiki kutokana na matokeo haya tunaona kuwa kuna mkakati mahsusi wa kuhakikisha kuwa tabaka la wenye nacho wengi wao wakiwa ni viongozi wetu wanawaandalia watoto wao kuwa watawala wa mambumbu waliowandaa kwa makusudi. Hivyo basi, tunaiomba serkali yetu ijirudi na kuungalia mfumo wa elimu ili kuirekebisha hali hii inayonekana kuanza kuwa na mizizi.