Tuendelee kujikumbusha kesi ya Ugaidi ya Mbowe baada ya Kibatala 'kumpelekea moto' Kingai

Tuendelee kujikumbusha kesi ya Ugaidi ya Mbowe baada ya Kibatala 'kumpelekea moto' Kingai

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
22,269
Reaction score
58,563
WAKILI PETER KIBATALA

Wakili Peter Kibatala: Utakasirika nikikuita kaka yangu?

Kingai: Ni sahihi, sababu nimekuzidi umri.

Wakili Peter Kibatala: Bila shaka hutakasirika nikitetea wateja wangu.

Wakili Peter Kibatala anamkabidhi Kingai Kitabu cha PGO.

Kingai: Ndiyo chenyewe.

Jaji: Angalia ndani vizuri ujiridhishe.

Wakili Peter Kibatala: Ni chenyewe?

Kingai: Ndiyo, ni chenyewe.

Wakili Peter Kibatala anamwonyesha Kingai ukurasa wa kwanza, ambapo IGP wa wakati huo, Said Mwema, alisema kila mshiriki aielewe na kuisoma PGO.

Anaeleza kwamba mshiriki ni polisi, ambaye anatakiwa kuwa na maadili na kujua miiko ya Polisi.

Kingai: (Anaitikia kwa kichwa.)

Jaji: Usitikise kichwa, sema kwa sauti.

Wakili Peter Kibatala: Kila mwanachama wa Polisi muda wote anatakiwa kuzingatia misingi ya haki za binadamu kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na watu wa Zanzibar.

Kingai: Sahihi.

Wakili Peter Kibatala: Sasa tuanze vizuri.

Wakili Peter Kibatala: Unapomkamata mtuhumiwa, unatakiwa pale pale umwambie wewe ni nani na unamkamata kwa makosa gani. Je, ni sahihi?

Kingai: Ni sahihi.

Wakili Peter Kibatala: Je, ni sahihi kwamba kwa mujibu wa PGO unatakiwa kuandika katika notebook, na kwa mujibu wa PGO notebook ni kifaa chako cha kazi?

Kingai: Ni sahihi.

Wakili Peter Kibatala: Ni sahihi, Kingai, kufunga safari kutoka Arusha mpaka Moshi, mkoa mwingine, ukiwa unajua mtuhumiwa Adamoo anatuhumiwa kwa ugaidi?

Kingai: Nilikuwa nafahamu.

Wakili Peter Kibatala: Na mawakili wa Serikali wameku-brief kuwa ushahidi wa sasa ni tofauti na ushahidi wa asubuhi. Hilo unafahamu?

Kingai: Ndiyo, nafahamu.

Wakili Peter Kibatala: Unafahamu bila shaka Mahakama haikuwepo wakati hayo yanatokea. Mahakama inatakiwa kuunganisha vidokezo vidogo vidogo kujua nini kilitokea.

Kingai: Sijaelewa.

Wakili Peter Kibatala: Unafahamu ushahidi mdogo mdogo ndiyo unaounda ufahamu kwa Mahakama kufanya maamuzi?

Jaji: Adamoo ni mshitakiwa wa kwanza au wa pili?

Wakili Peter Kibatala: Kibatala.

Wakili Peter Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kwamba ulipokuwa eneo la Rau huko Moshi, kama ulivyomwambia Mheshimiwa Jaji, ulifuata taratibu kwa mujibu wa PGO?

Kingai: PGO gani inasema hivyo?

Wakili Peter Kibatala: Huko tushatoka. Jibu ninalokuuliza.

Kingai: Hapo hakuniongoza.

Wakili Peter Kibatala: Ulizungumzia jibu la Adamoo kuwa uliliweka kwenye notebook, ambacho ni kifaa chako cha kazi?

Kingai: Hilo sikulisema.

Wakili Peter Kibatala: In fact, hiyo notebook hukuitoa Mahakamani, ambacho tumekubaliana ni kifaa cha kazi.

Kingai: Sikuitoa.

Wakili Peter Kibatala: Tutoke Rau Madukani, twende Police Station Moshi. Nilikusikia vizuri, kuna wadada mliwachukulia maelezo pale Moshi?

Kingai: Ndiyo.

Wakili Peter Kibatala: Tukumbushe kwamba investigation file lipo Dar es Salaam.

Kingai: Ndiyo, lilikuwa Dar es Salaam.

Wakili Peter Kibatala: Jaji akiandika, sema kwamba hukusema kwa nini ulichukua maelezo ya wale wadada pale Moshi wakati investigation file lipo Dar es Salaam.

Kingai: Sikuulizwa hilo.

Wakili Peter Kibatala: Jibu ninachokuuliza.

Wakili Peter Kibatala: Kwa ushahidi wako, kuna upekuzi wa Adamoo ulifanyika mbele ya mashahidi pale RAO Moshi?

Jaji: Naomba tunyamaze kupisha hadhana kidogo.

Mahakama kimyaaaaa.

Tunaendelea...

Wakili Peter Kibatala: Kuna mashahidi wawili walihojiwa Moshi wakati IR 5 imefunguliwa Dar es Salaam. Sasa mweleze Jaji kama ulifafanua kuwa kuna mazingira yoyote yaliyosababisha watoe maelezo Moshi na si Dar es Salaam.

Kingai: Nilieleza mazingira hayakuwa rafiki, ndiyo maana tukaenda kurekodia pale Polisi.

Wakili Peter Kibatala: Maelezo kuwa shahidi anaweza kuhojiwa popote kwa mujibu wa kiapo chako hapa Mahakamani, ulitoa hapa leo?

Kingai: Hiyo sikusema.

Wakili Peter Kibatala: Ndicho nilichokuwa nataka. Muda mwingine pay attention.

Wakili Peter Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni kifungu gani cha PGO kinachosema kwamba IR 5 ikifunguliwa Dar es Salaam, mshitakiwa anatakiwa asafirishwe kutoka Moshi hadi Dar es Salaam.

Kingai: Hiyo ni manifesto ya CPA, sikumbuki kifungu gani.

Wakili Peter Kibatala: Ngoja nikupe CPA, unitajie kifungu gani.

Wakili Peter Kibatala: Hutaki tena CPA?

Kingai: Nisisumbue Mahakama. Nilisema mazingira gani yaliyosababisha niwalete Dar es Salaam.

Wakili Peter Kibatala: Tuambie kifungu cha sheria chochote.

Kingai: Sikumbuki kifungu cha sheria.

Wakili Peter Kibatala: Pale Moshi palikuwa na facility zote za kuwawezesha kuwahoji watuhumiwa pale Moshi, kweli au si kweli?

Kingai: Kweli

Wakili kibatala: Mliwashwa nini kuwapeleka Dae es Salaam ?

Kingai: waheshimiwa majaji KIBATALA ananidharirisha

WEKA EMOJI KAMA UNATAKA TUENDELEE KUKUMBUSHANA.
 
Afu ndio baada ya hii case, akapandishwa cheo?

Huyu huwa anajitoaga fahamu siku zote.
Ilikuwa ni “Pole” na “Kifuta jasho”, wakati huyo akipandishwa cheo, mshitakiwa akapelekwa Ikulu.
 
Kumbe uko napo kulikuaga na matusi ya nguoni yaliyofichwa kwa mf wa tusi uliwashwa nini?
 
Hii kesi mbowe alikuwa anaenda jela.
Kwenda Jela hakumfanyi kuwa na hatia.
Kama kwa Lissu ushahidi mama ulitupiliwa mbali na Mahakama na bado Mahakama hiyo ikamkuta ma kesi ya kujibu wakati ishahidi wa hicho cha kujibu kimeshatupwa unatarajia nini?
 
Kwenda Jela hakumfanyi kuwa na hatia.
Kama kwa Lissu ushahidi mama ulitupiliwa mbali na Mahakama na bado Mahakama hiyo ikamkuta ma kesi ya kujibu wakati ishahidi wa hicho cha kujibu kimeshatupwa unatarajia nini?
Lissu sio rahisi ushahidi haumtii hatiani kwa uhaini ila mwamba ni kweli wale makomandoo alikuwa na jambo lake
 
Back
Top Bottom