Tuendelee na Mambo ya Msingi Elimu inachezewa sana

Tuendelee na Mambo ya Msingi Elimu inachezewa sana

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
16,295
Reaction score
33,994
Kuhusu Ya endeleaayo kwenye kuiba mitihani na kubadili namba za watahiniwa

Baada ya shule husika kufungiwa kuwa kituo cha Mitihani ya Baraza, Nini Hatma ya Wanafunzi waliokuwa wanasoma shule hiyo?

Je, kuifungia shule husika ndiyo suluhisho la udanganyifu wa mitihani ya elimu nchini?, Je, Bila mwanafunzi kujitokeza na kutaja uonevu huo, Vyombo vinavyohusika na usimamizi wa mitihani hawakulibaini hilo mapema?

Je, Mchezo huo ulifanyika kwa shule hiyo tu?, Hali ikoje katika shule zingine?, Who is should be Accountable?, Ni lazima tuonyeshe hatua zilizochukuliwa kwa pande zote


Shule za Binafsi (Private schools), Tanzania zimepewa Uhuru mkubwa mno ndiyo maana madudu mengi ya kuvuja kwa mitihani au Wizi hufanyika mara nyingi katika shule hizi.

Sasa hivi kuna kukimbizana kutafuta shule ipi nzuri, hasa shule zenye majina makubwa, kuna idadi kubwa mno ya wanafunzi wanaenda kuchukua fomu za kujiunga, shule inaweza kupokea maombi ya wanafunzi 5000 huku uwezo wake ni wanafunzi 100 tu, watalipia hela fomu, watafanya mitihani, watachaguliwa wachache ambao nao wanatakiwa kwenda kusoma pre-form one kwa malipo fulani kisha wanaendelea na masomo yao baada ya muda wa kufungua shule kufika.

Hii inajikuta inaleta badala ya kuwa ni shule imekuwa ni BIASHARA, ndiyo maana shule nyingi za Binafsi zinapambana ili kufaulisha zaidi wanafunzi wake na kupata status kubwa Ili iwe inapokea maombi mengi ya wale wanaotaka kwenda. Huwezi kuamini mpaka sasa shule nzuri zote zimejaa.

Serikali inatakiwa kuongeza jicho zaidi hapa ili kuhakikisha wanadhibiti ubora wa elimu kwa mujibu wa misingi iliyopo
 
nimecheki matokeo ya darasa la 7 ya shule ya kata jirani ninapokaa mpaka nimeshangaa. miaka yote ya nyuma walikuwa wanafeli sana. lakini matokeo ya mwaka huu 90% wamefaulu.

siasa imeshaingia kwenye elimu, matokeo yatoke mazuri ili kuwafurahisha wanasiasa na wazazi. kwa mtindo huu titabaki kuwa wajinga.
 
Back
Top Bottom