Tuepushe kipi kati ya uhai na siasa, utekaji na mauaji ya kisiasa? Ni heri kukaa bila vyama vingi ili tusiuane au tubebe yote?

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Kwa masikitiko makubwa, nashangaa kuona eti maisha na uhai wa watu unaweza kukatishwa kwa sababu zinazoitwa ni Siasa!

Ni ujasiri uliopita kiwango cha Rehema za Mungu, mtu anapoamua kumdhuru mtu, kumtesa na kumwaga damu yake kwa madai ya kuendelea kubaki kwenye nafasi za kisiasa huku akijua dhahiri naye ni yule yule mwanadamu mwenye nyama na uhai ndani uleule wa mtu anayemwaga damu yake, na kwa namna nyingine, yeye pekee ndiye mwenye kujihesabia haki juu ya uhai aliotugawia bule Muumbaji wetu.

Je, uhai ni zaidi ya siasa au Siasa ni zaidi ya uhai?

Je, tuepushe kipi kati ya UHAI na SIASA?

Au iko mbinu mpya ambayo hatujawahi kuitumia ili kwa hiyo, siasa tuione ni rafiki wa Uhai wetu?

Siasa za Tanzania na Afrika kwa ujumla, nimezinyoshea mkono!

Pia soma:Maandamano kupinga mauaji na watu wasiyojulikana yanatakiwa kuwa ya wananchi wote bila kujali dini wala chama cha siasa
 
Huu upuuzi alianzisha yule Dhalimu aliyeondoshwa, Sasa huyu chura kiziwi ndio anaendeleza baada ya kushindwa kuongoza nchi ili abaki madarakani.
 
Huu upuuzi alianzisha yule Dhalimu aliyeondoshwa, Sasa huyu chura kiziwi ndio anaendeleza baada ya kushindwa kuongoza nchi ili abaki madarakani.
Hapana mkuu, umesahau, kina mwangosi vipi
 
Acha tu ,tambua wanadamu wote hatufanani ndio maana haya yote yanatokea
 
Hapana mkuu, umesahau, kina mwangosi vipi
Naweza sema Mwangosi ilikuwa bahati mbaya sana katika kutekeleza majukumu ya Kazi ,Tena ilikuwa mchana kabisa. Tofauti na hii ya magenge ya kutekana na kuua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…