Tufanye biashara hii, yenye hela

Sisi binafsi tubapenda mtu akipinga jambo atoe solution yake sio unalalama tu na bila kuwambia watu wafanye nini hilo ni tatizo natumai komando utakuja na majibu ya tuache nini tufanye sio kuegemea upande mmoja tu.
 
nimepata mada ila mkosoaji bado hajathbitisha kwamba anataka kusaidia.biashara ya mkaa imebezwa afanye nini.
 


Hata kuandika neno consultancy huwezi, kazi yenyewe utaweza wapi?
 
Wazo lake ni zuri, na kwa kuanza inafaa.. Let's back to the point, maana ya biashara ni kuwa na mfumo mpya wa kipekee na endelevu. Imetosha. Lakini si watu wote watakuwa wafanya biashara.. Waajiriwa, waliojiajiri, wafanyabiashara, na wawekezaji(haya ndiyo makundi manne hasimu duniani kifikra na kiakili, chagua ulipo na songa mbele) usikatishwe tamaa na mtu pia ukiambiwa ukweli kubali hata kama hujui jifunze
 
Contact pse
 
Tafadhari orodhesha hata tatu hizo sustainable biashara ni zipi?
 
Chasha Poultry Farm unapoint nzuri sana, na unachokisema kinatugharimu kama taiga, lakini hiyo mipango yote inahatua mkuu. Michael Dell hakuanzia hapo alipo japo alikua na vision ya kukua kwa biashara yake. Hata hivyo nafikiri unafaham ni kitu gani kimemkumba hivi karibuni pale alipoanza kuacha kazi yake kuu kufanywa na makampuni mengine.

Pili, naomba nikukosoe kukejeli waajiriwa, huenda wewe binafsi ukawa na mtizamo tofauti kuhusu kuajiriwa lakini haimaanishi kuajiriwa ni utumwa na aibu kama unavyodai. Nimeshuhudia ajira zikiwawezesha watu kujikwamua na kupiga hatua kimaendeleo sana.

Hata Huyo Dell anahitaji wataalam wakusimamia na kutumia ujuzi na maarifa ndio maana unaweza kuitolea mfano Dell kama miongoni mwa makampuni yaliyofanikiwa.
 
Moja ya biashara ambayo inaniumiza kabisa kwasababu najua kuwa inaharibu mazingira na si endelevu
 
komandoo naona unapata taabu ya kuwajibu watu wewe si ufanye lako mkuu maana utateseka kujibu hapa
 
Msichukulie jazba wakuu lengo ni kujifunza na kubadilishana mawazo na uzoefu nasio kutambiana ujuzi wa economic stabilities zetu.
 
Tusichukulie jazba wakuu lengo ni kubadilishana mawazo na uzoefu n' not otherwise!!
 
Wew
Wewe lazima utakua ni jamaa wa fursa forever living etc. Mnazarau biashara ambazo ndio zimetulea mnataka wote tuuze virutubisho na sabuni
 

Mkuu hivi kuingiza mkaa mijini inatakiwa niwe na kibali gani kwa uelewa wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…