Paul malale
New Member
- Aug 30, 2022
- 1
- 0
Maendeleo ya nchi yetu yamekuwa ya polepole sana sababu kuu ni matumizi makubwa ya pesa kwa watu wachache yasiyo ya lazima,vnchi yetu inakadiriwa kuwa na watu 60M. Nni nchi inayokabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ajira, umeme, maji, hospitali, elimu bora na vitu vingine vingi ambavyo kuvitatua inahitaji kutumia pesa
Pamoja na kuhitaji pesa kufanya vitu hivi bado kuna matumizi mabaya mno ya pesa, twende bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wabunge 393, kila mbunge kwa mwezi hujipatia pesa inayokadiriwa kuwa 12M ,kwa wabunge 393 kwa mwezi mmoja wanaigharimu nchi 4.7B, fikiria kwenye nchi ya watu 60M inatumia 4.7B kwa watu 393?
Ubunge ni kazi ambayo haihitaji taaluma yoyote hakuna sababu ya kulipwa pesa yote hiyo, hiyo pesa wanayogawana hao watu 393 kwa mwezi ina uwezo wa kulipa walimu 6700 kwa mshahara wa 700,000 kwa mwezi au madaktari 4700 kwa mshahara wa 1,000,000 kwa mwezi
Kwenye nchi yetu hii inayokabiliwa na tatizo la ajira, je kuna kijana hapa Tanzania ukimwambia umpeleke bungeni akawe mbunge ummpe nyumba ya kuishi na umlipe mshahara wa 500,000 kwa mwezi akakataa? Maana yangu ni kwamba tuna uwezo wa kuwa na wabunge na tukawalipa 500,000 kwa mwezi na kazi ikafanyika, kwa mshahara huo wa 500,000 ukilinganisha na wanaopata sasa tutakuwa tumeokoa 4.5B kwa mwezi kama taifa, kwa pesa hio 4.5B kila mwezi tuna uwezo wa kujenga hospolitali mbili mpaka tatu
Hapo ni Bungeni tu ila kuna sehemu nyingi ambazo kuna matumizi makubwa ya pesa kwa watu wachache
KUHUSU TATIZO LA AJIRA
Vyuo vyetu vimekuwa vikizalisha wahitimu wengi mno kila mwaka ila tatizo la ajira nalo ni kubwa mno kutatua changamoto hii tufanye kitu kimoja kama taifa, kila mtu anayo haki ya kuajiriwa hivyo basi chochote kinachopatikana tujitahidi kugawana wote ili tupunguze ukali wa maisha
Nashauri muda wa kustaafu upunguzwe mfano tunaweza kuweka mwalimu aweze kustaafu baada ya miaka 10 ili kuweza kuwapa nafasi wengine ambao wamesoma ualimu na hawajaajiriwa ili nao wapate ajira, linakuwa ni jukumu la mwalimu aliyeko kazini kujua kwamba atafanya kazi kwa muda mfupi hivyo suala la kutunza pesa anayopata ni la kwake, atakachopata ndani ya hiyo miaka 10 itakuwa ni mtaji kwake atarudi mtaani akafanye hata biashara, tugawane umasikini, inaumiza lakini hamna namna inatakiwa tuchukue maamuzi magumu tutumie njia hii
Kwenye kustaafu tunaweza tukawa tunabakiza baadhi ya walimu wenye uzoefu ili kuja kuwaongoza wengine, ukishastaafu hakuna kupewa hela ya kustaafia, inakuaje wewe pamoja na kulipwa mshahara uendelee kupewa hela nyingine wakati kuna watu wamesoma wako mtaani na wana haki kama wewe
Ualimu ilikuwa ni mfano tu itungwe sheria kwa sehemu zote iwe hivi, kama uko Serikalini hiki kiti kinaumiza lakini hamna namna kuna mamillioni ya walimu, madaktari, wahandisi nk wako mtaani na hawana mtaji wa kujiajiri
MAENDELEO NI FIKRA, AHSANTENI

Upvote
0