Tufanye nini ili maziwa yakauke na yasitoke?

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
237
Mke wangu alijifungua yapata wiki ya tatu sasa. Bahati mbaya, mtoto hakuwa riziki.

Sasa maziwa yamekuwa yanajaa na kumwagika. Afanyaje ili yakauke na yasiendelee kutoka?
 
KAUMZA

Kuna dawa ya kuyakausha, nenda hospital watakupatia. Ukiachia hiyo hali iendelee atapata homa kutokana na vitu kama majipu kwapani, hii itatokana na maziwa kujaa kupitiliza kwenye matiti hivyo kutafuta sehemu dhaifu.
 
Last edited by a moderator:
mshana jr
Asante sana kwa ushauri. Tena homa imemuanza.
 
Last edited by a moderator:
Mi kama daktari mzoefu, nakushauri umwambie awe anayakamua kila mara yanapotokea ila akinywa dawa ya kuyakausha yasitoke atapata kansa ya titi hivyo kupelekea kukatwa titi, hivyo awe anayakamua tu yatakoma yenyewe.
 
Poleni sana,
Mama ajitahidi asile vyakula vya mama mjamzito, ikiwa ni pamoja na ile ulaji wa kutaka kuurejesha mwili ktk hali ya awali kabla ya ujauzito. In short, ale chakula cha kawaida kabisa kwa sasa.
 
Mi kama daktari mzoefu nakushauri umwambie awe anayakamua kila mara yanapotokea ila akinywa dawa ya kuyakausha yasitoke atapata kansa ya titi hivyo kupelekea kukatwa titi, hivyo awe anayakamua tu yatakoma yenyewe.

Dr MZOEFU, sikubaliani nawe kwenye kansa ya titi kuwa inasababishwa na dawa za kukata maziwa yasiendelee kutoka HALAFU ishu ya kukamua sio rahisi kihivyo hasa kama mama ana maziwa mengi.

Labda ungemshauri ayakamue huku akitumia dawa sahihi za kuyakausha.
 
Strictly prohibit kutumia dawa za kukaushia, utampeleka katika matatizo sugu.

Atafute chombo awe anayakamua kila anapohisi yamejaa katika titi maana yanatakiwa yatolewe mwilini siyo kuyazuia yasitoke, ukifanya hivyo basi breast cancer hiyoni ni moja ya risk factor yake.

Pole kwa kupoteza kichanga mkuu.
 
OK.. nashukuruni kwa ushauri wenu wenye kufaa
 
Poleni sana. Kila yanapoaza kutoka awe anayakamua.
 
Yaan asikamue kabisaa awe anayakanda na maji ya uvuguvugu tena huku kwenye makwapa ili yasitengeneze mitoki.Maana mechanism inayofanya maziwa yaendelee wakati mtoto ananyonya ni ile hali ya mtoto kuwa anavuta sasa ukiyakamua yanaendelea kujaa kwa kufuata same mechanism.Dawa labda ya kupunguza maumivu kama paracetamol mimi ni shuhuda wa nikisemacho.
 
Mke wangu alijifungua yapata wiki ya tatu sasa. Bahati mbaya, mtoto hakuwa riziki.

Sasa maziwa yamekuwa yanajaa na kumwagika.. Afanyaje ili yakauke na yasiendelee kutoka?

Pole sana mkuu. Mimi ni shuhuda kwa hili.

Nilishauriwa niache hivyo hivyo. USIKAMUE MAZIWA, maana uzalishaji wa maziwa utaendelea pia awe anakula chakula cha kawaida. Nilikuwa natumia panadol kupunguza maumivu ya homa ingawa matiti yalivimba hadi kwapani siku ya kumi nikashangaa yamerudi kama nilikuwa sinyonyeshi.
 
​Poleni sana Mkuu.
 
Asanteni sana ndugu zangu. Nashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…