Tufanye nini ili vijana wengi waingie kwenye Ujasiriamali wa Kijamii?

Tufanye nini ili vijana wengi waingie kwenye Ujasiriamali wa Kijamii?

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira na wenye hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi.
Nadhani haujaelewa kuwa jamaa anazungumzia aina gani ya ujasiliamali.....

Sio normal Enterprise entrepreneurs..... Anazungumzia Social Entrepreneurs!
 
Hapo hajazungumzia profit oriented entrepreneurs, amezungumzia Social entrepreneurs.....

Nadhani unatakiwa kujieleimisha juu ya utofauti wa kada hizi mbili my brother!

Social entrepreneur ni nani
 
Sifahamu CBO na FBO ni nini.

Mtu yeyote anayeanzisha biashara au mradi kwa lengo la kutatua changamoto za kijamii huitwa Mjasiriamali wa Kijamii "Social Entrepreneur" Mfano, nikianzisha mradi wa kukusanya taka ili kuondokana na takataka maeneo yetu na kuepusha jamii na magonjwa kama Kipindupindu.
Nawasi wasi sana na mentality za vijana wa Tanzania.

Maana kukosa kwao ajira in the first place ni kwasababu si watu wa kujitoa kwaajiri ya jamii yao. Sasa uwaambie wajitolee kupambana kusolve matatizo ya jamio yao kwa gharama nafuu, hapo utachezea za uso.
 
  1. Wazo zuri sana;Kuna mambo mawili ya kufanya kwanza serikali itoe kitu kinaitwa TAX credits kwa watu watakaofanya shughuli ambazo ni positive kwa jamii.Hizi Tax credit mtu anaweza kutumia kuombea Tax waiver pale anapokuwa na profitable venture.
  2. Pili serikali ifanye utambuzi maeneo muhimu yanayohitaji entrepreneurs na kuyapa kipaumbele katika legislation na Taxation ila watu wengi wavutike huko.Nafikiri hili linawezekana kwani sehemu inayoleta shida ni jinsi ammbavyo serikali inakataa kutoa kipaumbelee kwa community centred intiatives na hivyo tunajikuta tunakwama kila tunapojaribu.
Hivi ni kwanini huwa tunachukulia ujasiriamali kuwa ni kitu cha kuhamasishana kama kwenda jumuiya ya maria imakulata?!

Ujasiriamali ni kitu cha mtu na wale atakaowashirikisha automatically. Leo utashangaa mtu anauwezo wa kiakili wa kufanya vitu vyake na kusimamisha biashara ya pekee yake ila ukienda serikalini kuomba msaada utaambiwa ujiunge katika vikundi......vikundi gani sasa vya watu ambao wao wenyewe hawana mission yoyote ya maisha wako negative na hawana matarajio yoyote ya kimaisha kwa siku zijazo.....?!

Me nadhani serikali wazingatie ya fuatayo katika kutoa fursa kwa both social entrepreneurs na business enterprise entrepreneurs;

1. Bank ziwekewe special fund zenye low interest rates kutoka BOT ili wale wenye idea ambazo ni realistic na sio hawa wantepreneurs wanaoota kurusha roketi mars wakati maisha yao ni mtihani mtupu.

Hawa wenye realistic ideas waweze andikia business plan na proposals zake, wapate ushirikiano wa kutosha kutoka kwa ma' offecer biashara wa halimashauri wa kisasa ( sio hawa wa sasa uchwara na wajuaji ambao wanaamini kila kitu ni hadi ilani ya chama iseme).

2. Serikali iamue moja katika kubadili falsafa ya kiuchumi, maana kwasasa hatueleweki kama ni socialism au ni free market economy. Na ili ujasiriamali uwe active then best option ni kuadopt free market economy na serikali iwe na mashiko kidogo sana katika maamuzi ya kiuchumi.

Nitarudi kuongezea.
 
Ndugu yangu kila mtu ni mjasiriamali ila sio kila mjasiriamali ni mtengeneza fursa au mtatuaji wa changamoto.Ukirejea maelezo ya mleta uzi tunazungumzia watu wanaoitwa social entrepreneur amba ni wale ambao ventures zao zina impact kwa life style ya jamii.ni wale ambao wanaanzisha miradi kutatua kero specific za jamii.Hawa inabidi wape hamasa kwa sababu mitaji huwa ni midogo na zaidi huwa na mazingira magumu
 
Social entrepreneur ni nani
Huyu ni aina ya mjasiria mali ambaye anatatua changamoto za jamii yake bila kupata faida kwake ila faida inaenda kwa jamii husika.

Mfano, wewe umeumiza kichwa ukabuni bembea ambayo imeunganishwa na pampu inayovuta maji ardhini na kuyajaza katika karo kuuuubwa ambalo linasupply maji kwa jamii yako yenye shida ya ukosefu wa maji kwaajiri ya matumizi ya nyumbani.

So wakati watoto wanashinda kutwa nzima wanacheza na zile bembea, maji yanakuwa yakivutwa na hizi pampu za aina yake na yakijazwa katika matenki na kusupply kwa watu na hatimaye tatizo la maji katika jamii hii kutoweka kabisa.

Na watu wakalipa kiasi kidogo sana cha pesa ambacho kikikusanywa hutumika tena kulipia gharama za kumantain hizi pampu ili ziendelee kuwapo na kufanya kazi na pia kulipa mishahara ya wasimamizi wa huo mradi nafuu.

Hiyo ndio social entrepreneurship......kama uonavyo katika mfano huo, hakuna sehemu nimesema huyu aliyebuni huo mradi atajilipa mamilioni wala senti tano isipokuwa amesolve tatizo la jamii yake completely ambalo huwenda angekuwa business enterprise entrepreneur angeweka bei za juu na kuchaji pesa kufidia gharama lakini pia kupata faida katika huu mradi kwaajiri ya matumizi yake binafsi......!
 
Are you familiar with the term "Bricolage" ?!

Kama unafahamu maana ya hilo neno, then hapo ndipo msingi wa neno "social entrepreneurship" ulipo.

Otherwise naomba unifahamishe if unauelewa mpana katika kada ya ujasiriamali.......ni eneo langu kitaaluma so sibabaishi wala sisemi nisichokifahamu mkuu.
 
Ndugu yangu kila mtu ni mjasiriamali ila sio kila mjasiriamali ni mtengeneza fursa au mtatuaji wa changamoto.Ukirejea maelezo ya mleta uzi tunazungumzia watu wanaoitwa social entrepreneur amba ni wale ambao ventures zao zina impact kwa life style ya jamii.ni wale ambao wanaanzisha miradi kutatua kero specific za jamii.Hawa inabidi wape hamasa kwa sababu mitaji huwa ni midogo na zaidi huwa na mazingira magumu
Na katika kukutoa vumbi katika kioo chako cha maarifa. Si kweli kuwa kila mtu ni mjasiria mali ingawa anaweza kuwa.....

Ukiona mtu anafuata fursa baada ya kuona inalipa huyu huitwa mfanya biashara (ingawa imezoeleka kuwaita ni wajasiria mali)....

Ila mtu ambaye huwa anaanza na kitu yeye kama yeye katika eneo fulani na kukifanya kwa mara ya kwanza na kukigeuza hicho kitu kuwa fursa ya kupata faida ya kibishara then huyo tunamwita mjasiria mali.

Naomba usinichokoze nikumwagie hadi aina za wajasiria mali hapa maana utakimbia....

Ila kwa kifupi nikupe kanuni hii ikusaidie kutofautisha wajasiria mali na wafanyabishara.

Ujasiria mali unakwenda sambamba kabisa na hasara na hakunaga ujasiria mali bila hasara. Hasara ndio mbolea ya kuimarisha na kurutubisha shughuli yoyote ya ujasiriamali.

On the other hand, biashara na hasara ni vitu viwili tofauti, yaani maji na mafuta, ccm na chadema. Palipo na hasara biashara haitakuwapo ila ujasiria mali utakuwapo.

For deper learning nitafute....nijaze ubongo wako na nondo mpya.
 
[QUOTE="ukh

Tatizo linaanzia katika mfumo wa elimu.

Elimu ni jambo la kwanza kwa umuhimu katika taifa lolote; lakini, inasikitisha kwamba, mitaala ya elimu haikidhi mahitaji ya mazingira, na vile vile elimu inachangia uoga na ajinga kwa kiasi kikubwa.

Vijana wengi sana wanaamini katika kusoma ili waajiriwe, na hawana wazo la kuanzisha biashara zao wenyewe.

Mfano, utakuta mtu ana masters ila kaajiriwa na mtu asiye soma au aliyesoma kidogo. Hapa maana yake ni kwamba, huyu mwajiri hana elimu ila ni jasiri kuliko mwenye elimu ya masters.

Kwa hiyo elimu na mtaala wake kwa ujumla, unaua ubunifu kwa vijana.

Siasa nazo si rafiki kwa vijana.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 70+ ya Watanzania wanategemea kilimo.

Lakini cha ajabu ni kwamba, bajeti katika kilimo ni ndogo sana ukilinganisha na sekta nyingine.

Vile vile, mitaala ya elimu haijakipa kilimo kipaumbele cha kutosha.

Masoko ya mazao si rafiki na sera za kupiga marufuku usafirishaji wa mazao nje ya nchi unawaumiza sana wakulima, na inafifisha kilimo biashara.

Mimi binafsi ni mhitimu wa shahada, lakini nimejikita katika ujasiriamali wa kilimo biashara

Ni hayo tu ukhuty
Tatizo wala sio elimu, tatizo ni mindset zetu iliyojengwa toka tukiwa wadogo kabisa majumbani mwetu.
 
Huyu ni aina ya mjasiria mali ambaye anatatua changamoto za jamii yake bila kupata faida kwake ila faida inaenda kwa jamii husika.

Mfano, wewe umeumiza kichwa ukabuni bembea ambayo imeunganishwa na pampu inayovuta maji ardhini na kuyajaza katika karo kuuuubwa ambalo linasupply maji kwa jamii yako yenye shida ya ukosefu wa maji kwaajiri ya matumizi ya nyumbani.

So wakati watoto wanashinda kutwa nzima wanacheza na zile bembea, maji yanakuwa yakivutwa na hizi pampu za aina yake na yakijazwa katika matenki na kusupply kwa watu na hatimaye tatizo la maji katika jamii hii kutoweka kabisa.

Na watu wakalipa kiasi kidogo sana cha pesa ambacho kikikusanywa hutumika tena kulipia gharama za kumantain hizi pampu ili ziendelee kuwapo na kufanya kazi na pia kulipa mishahara ya wasimamizi wa huo mradi nafuu.

Hiyo ndio social entrepreneurship......kama uonavyo katika mfano huo, hakuna sehemu nimesema huyu aliyebuni huo mradi atajilipa mamilioni wala senti tano isipokuwa amesolve tatizo la jamii yake completely ambalo huwenda angekuwa business enterprise entrepreneur angeweka bei za juu na kuchaji pesa kufidia gharama lakini pia kupata faida katika huu mradi kwaajiri ya matumizi yake binafsi......!

Hujamuelewa mleta mada
 
Kwanza kusanya hao vijana,wape somo waelewe be a leader,watie moyo,waeleweshe kuwa kazi yenyewe ni ngumu inataka muda,moyo,uvumilivu,nia thabiti na kuaminiana kwa hali ya juu. Sasa pendekezeni mawazo,yajadiliwe muone ni kipi mnapenda na kipi mnaweza,.
Halafu mnaangalia kile mlichonacho kama kianzio,inaweza kuwa nguvu au ujuzi.
Baada ya hapo fikirieni jinsi ya kupata pesa japo kidogo. Hatua inayofuata ni kuchagua saiti ya kazi..na mkaisavei.
Mwisho ni kuwaona wenye mamlaka. Hapo mko tayari kwa kuomba vibali na kuanza shughuli.
 
Hujamuelewa mleta mada
Umesoma alichosema pale juu?! Hadi ameamua kutumia neno social entrepreneurship it means alitaka ujumbe ufike vile namna nimekufafanulia, otherwise angetumia tu neno entrepreneurs basi.....

Sasa sijui mimi na wewe hapa hatuelewani eneo gani?!

Kwa kifupi hapa ni sawa sawa na wafamasia wawili wamekutana na wametambua ajenda inayozungumziwa kwa jinsi terminology na maneno yaliyotumika yanatanabaisha watu wa field gani. Sasa wewe ninakufafanulia kuwa jamaa alichosema nimemnyaka vema sana, ila wewe umekwenda chaka tena tunaanza kubishana.

Wewe una taaluma gani labda tuanzie hapo ndugu maana tusipishane kauli halafu kumbe unadegree ya Economics , Banking, au Accounting, then unabishana na mimi ambaye nakuelekeza kitu ambacho nimekisoma na nimejaza material yake kwenye library yangu.
 
Back
Top Bottom