Tufanye nini tupate utajiri?

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,363
Reaction score
1,431
Habari za jioni wakuu. Nijielekeze Moja kwa moja kwenye topic.

Haiitaji kuwa msomi kuelewa ukifanikiwa kipesa maishani ni jambo litakalokusaidia kufurahia maisha na kupunguza sana stress za maisha, hivyo kuwa tajiri ni ndoto ya watu wengi.

Lakini pamoja na kufahamu ukweli huu, hali halisi ni kuwa watu wengi hasa tunaoishi dunia ya tatu bado tunaishi maisha ya umasikini sana, yaliyojaa karaha na stress kibao tunapokuwa tunapambanakupata human basic needs yaani chakula malazi na mavazi bila kusahau sex.

Paradox hii inaibua tafakuri juu ya nini hasa Siri ya kuwa tajiri?

Makundi mbalimbali kama wachumi, wanasiasa, wapigania haki za kimatabaka, taasisi za kijamii na kimataifa hutoa nadharia ambazo uamini zikitekelezwa vyema zaweza kukutoa kwenye dimbwi la ukata.

Mbinu hizo na kanuni ni Kama kufanya kazi kwa bidii, maarifa na ujuzi, kuwekeza na nidhamu ya pesa. Mambo mengine ni kuondoa rushwa, kukuza uwazi na uwajibikaji na kujenga mifumo ya usawa katika jamii.

Kwa Karine nyingi, nchi zetu za kiafrika zimejaribu mbinu hizo japo kwa kusuasua ila matokeo yake kiujumla sio yenye tija sana.

Nikiwa naamini JF ni familia kubwa ya watu wenye kila uzoefu na mazingira tofauti ebu tushilikieni nini kifanyike tupate utajiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu kina masikio, na ili fedha ije kwako lazima iamuliwe ndipo ije.

Zab 24:1. Nchi na vyote viijasavyo ni mali ya Bwana. Hivyo basi kama vitu vyote ni mali ya Mungu basi jua yeye ndiye pekee mwenye kutajirisha au kumfukarisha mtu kwa kadri ya uamuzi wake. Juhudi, nidhamu ya fedha n.k wameviongezea watu tu, tena walioandika vitabu vya jinsi ya kuwa tajiri ni watu wa kawaida tu.

Shetani hutoa utajiri pia wa hapa duniani ila hatajirishi, kuna mkwamo mbele unapotumia mali zake.
 
So mkuu, Mungu anafurahia tuwe masikini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alipo mkabidhi shetani, hapo ndio kila kitu kilipoharibika, shetani anatunyoosha kwelikweli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…