"Hii biashara ngumu sana Tanzania"Namimi nashika nafasi ili nipate notification nione mawazo ya wadau kabla ya kuchangia hii biashara ngumu sana Tanzania.
Rebeca 83 jambo kubwa na la msingi kwanza ni utayari, pili changamoto za mitaji kwa vikundi ama mtu mmoja mmoja maana taasisi zetu za fedha masharti yake si rafiki especial kwa vijana ambao ni beginner.
Sekta ya kilimo tukiikalia serious ni sekta inayoweza kuajiri watu wengi sana tokea wataalamu wa vipimo/udongo,wataalamu wa mbegu na pembejeo, wakulima shambani,nguvu kazi shambani,wauzaji wa mashine za shamba,mafundi kwa maana ya kutengeneza miundombinu ya uhifadhi mazao,secta ya usafirishaji,wafanyabiashara, watu wa masoko till tumfikie final consumer.
We ushawahi kufanya kilimo?Mkuu ni kweli kuna employment opportunities nyingi kwenye Kilimo, kwenye proposal yangu iliyoibiwa Na Stellian Russu 😉[emoji1787][emoji1787]nili identify we have 44 Million hectares of Arable Land in Tanzania;but only 33% of this is put into effective use,Imagine tuki exploit fully this land,si uchumi wetu watanzania utapanda?
Kuhusu Beginners, ingependeza kupewa mkopo wa Kilimo but kuwe na Mentors wanao wa coach as they progress...
Mimi si mtaalamu wa fedha ila kama niwazavyo ni sahihi nadhani mabenki na taasisi za fedha na mikopo badala ya kukaa ofisini kusubiri wafanyabiashara wakubwa kuwafuata kuchukua mikopo mikubwa mikubwa kwenda nje ya nchi kuagiza vyakula ambavyo wanakuja kustore kwenye magodown basi wafanye yafuatayo.
- Mosi zifanyike semina za kuwahusisha vijana kila mikoa/kanda kama itakavyoonekana inafaa kutokana na tabia nchi na aina ya kilimo kitakacholeta tija kwa kanda husika.
- Viundwe vikundi tofauti tofauti baada ya zoezi la semina na vikundi hivi kila kimoja kichague aina ya kilimo/zao watakalokua wanadeal nalo.
- Watafutiwe ardhi ya kutosha ambayo kwa ajili ya kuiplement aina ya zao watakalokua wamechagua kila kundi.
- Wawekewe miundombinu wa maji na barabara za kuwawezesha kufika maeneo ya uzalishaji/mashamba husika.
- Kwakuwa tayari vikundi husika vitakuwa vimeshatambulika basi vitafanya chaguzi ambazo pamoja na mambo mengine vitasajiliwa kisheria ili viweze kukopesheka.
- Hatua itakayofuata ni kutafutiwa wataalamu wa kilimo kwa kila kundi hapa nikilenga kwa wenye aina inayofanana ya kilimo awepo mtaalamu wa kilimo husika ili aweze kuapply utaalamu wake kwenye mambo ya soil ,mabadiliko ya tabia nchi na mbegu bora.
- Wakati vikundi hivi zikiwa kwenye shughuli za uzalishaji basi kazi ya maafisa wa taasisi hizi za fedha ni kutafuta masoko na bei ya mazao ili mkulima atakapotoka shamba akute soko la bidhaa yake ,aweze kuuza ,kurejesha mkopo na kuendelea na process nyingine za kufanya maandalizi ya mzunguko mwingine wa uzalishaji.
Kwanini uogope?No, lol, naogopa sana ku invest huko, ni kama ku bet vilee.. [emoji1787]
Point yangu namba sita nimetaja wataalamu wa kilimo nikijumuisha watafiti ama researchers wako kama ulivyotaka.Asante kwa maelezo mazuri,Ardhi tunayo kubwa tu, ni jinsi ya kuitumia ndio tatizo....i guess wale wote uliowataja ambao wanaweza kuwa employed kwenye kilimo ungeongeza na RESEARCHERS!.. hawa wata continuously identify maeneo mbali mbali yenye potential ambayo watu tunaweza kulima ambayo ita improve our living standards.
Boda boda sita watamletea 10,000 kila mmoja, kila siku . Hii ni hela ya kuwalipa vibarua wanaotaarisha shamba. Kwakifupi huyo ameshauwaga umasikini.Huu uzi nimeuona usiku huu,
Ni masaa kadhaa toka mchana wa leo Jamaa yangu Niliyesoma naye primary akazingua,
KAINGIZA MJINI FUSO ZA VIAZI MBILI kutoka lushoto,
Sijawahi kuamini katika kilimo, ila huyu mwamba kanifanya nijifikirie upya, sio kama naona hakilipi, la hasha ila nimekua niki calculate risk zake sana, hasa nikikumbuka mzee alivyochezea za uso Ifakara, Mbeya na Huko lushoto japo Alikua akikiotea basi ni hela ya kusimamisha nyumba.
Japo pia inapaswa kuelewa HUPASWI kufanya eti kisa yeye katusua, maana pia kwa madai yake hakuanza leo...
Elimu mda mwingine inatudanganya sanaaaaaaa, huyu mwamba hata hakuwazia hasara, Sema Nilipopata ukakasi ni kwamba anasema hela almost yote anataka anunue boda akazijaze Kijijini, hapa kidogo nikashtuka manake hii biashara nayo sijawahi kuiamini, lakini nikakumbuka hata hiki kilimo sikua nikikiamini, leo ndio kimempa hela ya kununua boda 6, Nikaona Sina confidence ya kumshauri, zaidi ya kimoja ambacho amekiitikia kwa moyo wote nimemwambia abakize pesa ya kuandalia shamba tena maana ndio wanaanza taena Asubiri December.
Siandiki futuhi hapa, huyu Millionaire nimelala naye hapa, Asubuhi Nampeleka Mjini akanunue vyake apandishe kwenye Tandamu Aliyokuja nayo Arudi Kijijini,
Sasa uliza kazi yake Kubwa.....?
Kuendesha Magari ya Magogo ya kuchana mbao.
Yaaaps, Katika kutafuta pesa ukijifanya unawaza mbali sanaa, mda mwingine ndio unaharibu.Boda boda sita watamletea 10,000 kila mmoja . Hii ni hela ya kuwalipa vibarua wanaotaarisha shamba. Kwakifupi huyo ameshauwaga umasikini.