Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona hakuna waliojibu, mimi nasisitiza Kwa waliopo Mwanza, Geita na Simiyu wanaweza kuja kwangu Mwanza kujifunza Ufugaji Nyuki na uzalishaji mazao Sita.Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano.
Leo napenda kuleta uzi wa utofauti kidogo kwa ajili ya kukumbushana mambo madogo yenye mchango mkubwa katika hatua za kuyasaka mafanikio.
Ni dhahiri kuwa kila mmoja anatamani kupiga hatua moja au zaidi kutoka pale alipo. Na kwa bahati nzuri zaidi wapo watu waliopiga hatua mbele ya pale tulipo.
Point ni kuwa tunaweza kujifunza jambo kutoka kwa baadhi ya watu waliothubutu kufanya kile ambacho kwetu bado kipo ideal.
Ni vyema sana kuhusisha survey kwa watu binafsi, taasisi au hata makampuni yanayofanya mradi flan ambao umekuwa ukitamani kuufanya. Hii itakusaidia kujifunza namna sahii ya kuuendeasha mradi husika, kujua ni changamoto zipi zinaukabili mradi na hata njia za kutatua changamoto hizo.
Wengi tumekuwa tukitumia zaidi mitandao ya kijamii katika kutafuta threads za jinsi ya kufuga kuku, kufanya kilimo, na mambo mengine ya uzalishaji mali, tukisahau kuwa miongozo tutakayoipata humu ni nadharia tupu.
Itafaa zaidi kama utapata mtu anayefanya kile unachowish kukifanya, ukamtembelea na kujifunza mambo mbalimbali katika uhalisia, ili utakapoanza uwe na maarifa ya kutosha kutoka kwa mtu mwenye uzoefu na jambo husika.
Kwa mfano, kwa waliopo Dodoma, mnaweza kuunda kikundi cha watu 10 na kuendelea, mkatuma maombi kwa mh. Mizengo pinda ya kutaka kutembelea miradi yake iliyopo kijiji cha ZUZU. Huko mtajifunza ufugaji wa kuku wa kienyeji, nyuki, ng'ombe wa kisasa wa maziwa, ufugaji wa samaki, nguruwe. Pia kilimo cha zabibu.
Kwa idadi iliyopo ya wataalamu waliopo pale, hakika utapata lecture itakayokupa mwongozo katika hayo nliyataja hapo awali.
Vivyo hivyo hata kwa wanaowish kufanya biashara, better upate details kutoka kwa mfanyabiashara mwenyewe, na si kuyaamini mawazo ya watu wa humu kwa 100%, maana kuna fake details nyingi sana nlizokutana nazo humu.
Nawatakia kila lililo jema katika harakati za kuyasaka mavumba.
#ghosts never die.
Wanapitia na wanakuja sana PM, baadhi nimewakumbusha kuchukua hio namba wakutafute mkuu.Naona hakuna waliojibu, mimi nasisitiza Kwa waliopo Mwanza, Geita na Simiyu wanaweza kuja kwangu Mwanza kujifunza Ufugaji Nyuki na uzalishaji mazao Sita.
Navuna Asali, Nta, Pollen, Propolis na Sumu ya Nyuki. Karibuni.
Call +255622 642620
WakaribieWanapitia na wanakuja sana PM, baadhi nimewakumbusha kuchukua hio namba wakutafute mkuu.
Asante kwa ushirikiano