Tufanyeje kurejesha uzalendo Tanzania?

Tufanyeje kurejesha uzalendo Tanzania?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Uzalendo tafsiri yake nyepesi ni kutokuvunja sheria za nchi yako.

Chanzo cha uzalendo kutoweka ni umasikini ambao unatia watu tamaa siyo tu ya kulimbikiza mali kwa wastani na ziada, bali kutafuta chochote cha kuokoa roho/uhai kwa maana ya mahitaji ya msingi ya chakula, malazi na mavazi ambayo haya nayo yamekuja kuwa changamoto kwenye jamii pasina ufumbuzi kupatikana.

Nchi zote zilizoendelea duniani zilitanguliza na kulinda uzalendo.

Tufanyeje kurejesha uzalendo Tanzania?

Toa ushauri wako ukijuwa kwamba kutoweka kwa uzalendo nchini/kwenye jamii kunakuathiri na kizazi chako.

1653144822644.png
1653144855582.png

Taswira zote kwa hisani ya google.
 
View attachment 2233208 View attachment 2233211
Taswira zote kwa hisani ya google.
Uzalendo (kwa Kiingereza patriotism[1]) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia. Inakaribiana sana na utaifa.[2][3][4] Uzalendo ukizidi kiasi cha kulitetea taifa huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.
 
Fanya utafiti kabla ya kuandika unapotosha maana nzima ya uzalendo
 
You have said it all Yoda.

Ila hata hii ya sasa nayo ikipata msimamizi na mtekelezaji mzuri huenda uzalendo ukarejea. Mwl alitumia hii hii.
Katiba hii haiwezi kukifaa kizazi cha leo ambapo nafasi za sensa 200k wanaomba 600k
Wakati enzi zile drs la 8 wanatafutwa ofisi ziko wazi.
Wabishi mtapasuka soon
 
Chanzo cha uzalendo kutoweka ni umasikini ambao unatia watu tamaa siyo tu ya kulimbikiza mali kwa wastani na ziada, bali kutafuta chochote cha kuokoa roho/uhai kwa maana ya mahitaji ya msingi ya chakula, malazi na mavazi ambayo haya nayo yamekuja kuwa changamoto kwenye jamii pasina ufumbuzi kupatikana.
Nina mashaka makubwa sana hii sababu yako ya chanzo cha kutoweka kwa uzalendo.
Hao unaowaita maskini wakihaha kujitafutia mahitaji yao ya lazima wanaweza kuwa ni wazalendo zaidi kwa nchi yao kuliko nyie mlioko maofisini mkilipwa mishahara minono na marupurupu kibao, lakini ndio mnaongoza kwa kuiibia hii nchi.
Unadhani Kikwete alipokuwa anasaini mikataba ya kifisadi alikuwa anatafuta kujipatia chakula, malazi na mavazi?
 
Uzalendo (kwa Kiingereza patriotism[1]) ni hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake kwa msingi wa kabila, utamaduni, siasa au historia. Inakaribiana sana na utaifa.[2][3][4] Uzalendo ukizidi kiasi cha kulitetea taifa huitwa uzalendo kipofu au uzalendo bubu.
Misingi ya ukabila na utamaduni ya kuudhihirisha uzalendo huzaa hisia za ukanda kwenye mfumo wa siasa, ajira, teuzi, elimu, ulinzi na usalama, fursa za umiliki wa uchumi nk.

Excerpt from JK Nyerere's oratory.
‘I’m a good Mzanaki, but I won’t advocate a Kizanaki-based political party. ... So I’m a Tanzanian, and of course I am Mzanaki; politically I’m a Tanzanian, culturally I’m Mzanaki.’ (Sandbrook & Halfani eds. 1993: 31-32).

Kwa maoni yangu, uzalendo unatakiwa kutafsiriwa kwenye misingi ya kitaifa tu zaidi ya ile ya kikabila, kitamaduni, kidini, kikanda nk.
 
Nina mashaka makubwa sana hii sababu yako ya chanzo cha kutoweka kwa uzalendo.
Hao unaowaita maskini wakihaha kujitafutia mahitaji yao ya lazima wanaweza kuwa ni wazalendo zaidi kwa nchi yao kuliko nyie mlioko maofisini mkilipwa mishahara minono na marupurupu kibao, lakini ndio mnaongoza kwa kuiibia hii nchi.
Unadhani Kikwete alipokuwa anasaini mikataba ya kifisadi alikuwa anatafuta kujipatia chakula, malazi na mavazi?
Spear of the nation (Umkhonto we Sizwe),

Ni hivi, kupata elimu ili kuwa na fursa ya kufaidi hivyo vinono maofisini ni njia mojawapo ya kuondokana na umaskini, yaani elimu/maarifa huondoa umaskini. Umaskini wa msomi na umaskini wa mjinga vina utofauti mkubwa sana. Maskini hawezi kuwa na uzalendo fursa ya kuiba mali ya umma inapojitokeza kwake. Hawezi kwenda kulala njaa ilhali ameona mwanya wa kuipiga serikali/umma.
 
Uzalendo tafsiri yake nyepesi ni kutokuvunja sheria za nchi yako.

Chanzo cha uzalendo kutoweka ni umasikini ambao unatia watu tamaa siyo tu ya kulimbikiza mali kwa wastani na ziada, bali kutafuta chochote cha kuokoa roho/uhai kwa maana ya mahitaji ya msingi ya chakula, malazi na mavazi ambayo haya nayo yamekuja kuwa changamoto kwenye jamii pasina ufumbuzi kupatikana.

Nchi zote zilizoendelea duniani zilitanguliza na kulinda uzalendo.

Tufanyeje kurejesha uzalendo Tanzania?

Toa ushauri wako ukijuwa kwamba kutoweka kwa uzalendo nchini/kwenye jamii kunakuathiri na kizazi chako.

View attachment 2233208 View attachment 2233211
Taswira zote kwa hisani ya google.
Njia pekee fupi na ya halali ni kuleta KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI .
 
Uzalendo kwa itikadi ya ccm ni kisifia viongozi wakuu hasahsa rais. Kwa itikadi yetu sisi wengine huo ni unyumbu
 
Njia pekee fupi na ya halali ni kuleta KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI .
Nakubaliana na wewe kabisa, ila hofu yangu ni hii:-

Katiba na Tume ya Uchaguzi ni taasisi/vyombo vya warasimu (bureaucrats/elites).

Mkerewe na Mkara wa kule visiwani wasio elites watachelewa kuathiriwa (impacts) maisha yao na taasisi/vyombo hivi.

Constitution and Free Electoral Commission are the tools of the bureaucrats/elites for they benefit first-consideration documented in these tools.

Mungu atusaidie!
 
Hivi Uzalendo huo wa ' "...Kutovunja sheria za nchi yako..." ni Upi haswa?

ni nchi gani inaongoza Duniani kuwa na sifa hizo?
 
Back
Top Bottom