Rais kupunguziwa madaraka hasahasa ya uteuziTusaidie mbinu za kutoka kwenye unyumbu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Rais kupunguziwa madaraka hasahasa ya uteuziTusaidie mbinu za kutoka kwenye unyumbu.
Ni tafsiri (coined by the political bureaucrats) na kuwekwa kwenye mtaala ili tufunzwe kwenye somo la siasa, practically baada ya kuhitimu shule inadhihiri kwamba tulikuwa brainwashed, kwa sababu inathibitika kwamba keki ya taifa kumbe hainaga mgawanyo sawia kwa wana wa nchi na hii inastawisha umaskini ambao ukikomaa hupoteza uzalendo.Hivi Uzalendo huo wa ' "...Kutovunja sheria za nchi yako..." ni Upi haswa?
ni nchi gani inaongoza Duniani kuwa na sifa hizo?
Good, hizo zita-rollback poverty.Haki sawa na Fursa sawa
Hii ni tafsiri ya kijinga kabisa kuwahi kuisoma. Uzalendo ni kuipenda nchi yako na watu wake, nukta!Uzalendo tafsiri yake nyepesi ni kutokuvunja sheria za nchi yako.
Hawa "political bureaucrats" wa nchi gani mahususi?Ni tafsiri (coined by the political bureaucrats)
Ili nielewe, hao political bureaucrats waliweka tafsiri inayosema...au kwa lugha nyepesi...waliobambika tafsiri ya kuwa "kutovunja sheria ya nchi yako" ...ni Uzalendo na wamefanya hivyo kwa kuweka kwenye mitaala ya shule?na kuwekwa kwenye mtaala ili tufunzwe kwenye somo la siasa,
lbda najixnganya. Huu Uzalendo na mashaka nao...practically baada ya kuhitimu shule inadhihiri kwamba tulikuwa brainwashed, kwa sababu inathibitika kwamba keki ya taifa kumbe hainaga mgawanyo sawia kwa wana wa nchi na hii inastawisha umaskini ambao ukikomaa hupoteza uzalendo.
Kamaradi Stefano,Hii ni tafsiri ya kijinga kabisa kuwahi kuisoma. Uzalendo ni kuipenda nchi yako na watu wake, nukta!
Kurudisha uzalendo ni rahisi sana. Wanasiasa na vyama vyao na nchi na vyombo vyake vianze kuwa wazalendo kwanza. Wananchi watafuata mkondo naturally!
Umeweka picha ya Mwalimu hapo, aliipenda nchi yake na watu wake na ndio maana wananchi wakafuata mkondo.
Tanzania ilijifunza ubinafsi kwa njia mbaya, ndiyo maana uzalendo ukavunjika. Kabla ya Utawala wa Mwinyi, nchi ilikuwa na uzalendo sana, ila hali ya uchumi aliyokuta Mwinyi ikamlazimisha kukubaliana masharti ya IMF na World bank, ambayo yalitaka kubinfsisha mashirika yote. Sasa kuanzia pale ndipo ubinafsi ukaanza, na hivyo ni ubinafsi ulioanza kwa njia mbaya sana iliyosukumwa ya shida. Ubinafsi huo ndio umeondoa uzalendo kabisa nchini.Uzalendo tafsiri yake nyepesi ni kutokuvunja sheria za nchi yako.
Chanzo cha uzalendo kutoweka ni umasikini ambao unatia watu tamaa siyo tu ya kulimbikiza mali kwa wastani na ziada, bali kutafuta chochote cha kuokoa roho/uhai kwa maana ya mahitaji ya msingi ya chakula, malazi na mavazi ambayo haya nayo yamekuja kuwa changamoto kwenye jamii pasina ufumbuzi kupatikana.
Nchi zote zilizoendelea duniani zilitanguliza na kulinda uzalendo.
Tufanyeje kurejesha uzalendo Tanzania?
Toa ushauri wako ukijuwa kwamba kutoweka kwa uzalendo nchini/kwenye jamii kunakuathiri na kizazi chako.
View attachment 2233208 View attachment 2233211
Taswira zote kwa hisani ya google.
Kamaradi Kichuguu,Tanzania ilijifunza ubinafsi kwa njia mbaya, ndiyo maana uzalendo ukavunjika. Kabla ya Utawala wa Mwinyi, nchi ilikuwa na uzalendo sana, ila hali ya uchumi aliyokuta Mwinyi ikamlazimisha kukubaliana masharti ya IMF na World bank, ambayo yalitaka kubinfsisha mashirika yote. Sasa kuanzia pale ndipo ubinafsi ukaanza, na hivyo ni ubinafsi ulioanza kwa njia mbaya sana. Ubinafsi huo ndio umeondoa uzalendo kabisa nchini.
Mtanzania akiambiwa ahujumu nchi ili apate pesa, atafanya hivyo. Unaona kuwa kuna watanzania waliokuwa wanahsbaikia ndege za ATCL kukamatwa nje ya nchi, na kuna watanzania waliokuwa wakishiriki katika sakata hilo ili wapate hela. Kuna watanzania walioshirikiana na makampuni ya madini kuihujumu serikali mapato yake mradi wao wapate kityu fulani. Maafisa wa kodi walikuwa mbele sana kuhujumu mapato ya serikali ili wazipate wao. Mifano ni mingi san.
Utashangaa nchi kama Kenya pamoja na kwamba wana matatizo ya Ukabila kwa muda mrefu, lakini linapokuja swala la uzalendo kwa nchi yao, wako juu sana na wanakuwa kitu kimoja. Wote wanajivunia na kulinda kilicho cha Kenya bila kujali itikidai na makabila yao.
Tuko tayari hata kuvunja viti vya Uwanja wa Taifa kwa sababu za kibinafsi bila kujua kuwa hiyo ni mali ya walipakodi wa Tanzania.Kamaradi Kichuguu,
Umeongea kitu real!
Kwenye mauaji ya Kenya 2007-2008, Wakenya waliheshimu mitaji iliyowekezwa bila kuihujumu wakijuwa baada ya vita watataka kurudi kwenye ajira zao ili maisha yaendelee na vizazi vyao (uzalendo wa kutovunja sheria huu) ndiyo maana baada ya machafuko yale Kenya haikushuka kwenye FDI wala uchumi haukuyumba. Waliuana kikabila kati ya staff na staff lakini hawakuchoma wala kuiba kiwanda, unique!
Hapa Tz tunahujumu mali za umma (kama ulivyosema) hata bila nchi kuwa vitani.
You have said it all Yoda.
Ila hata hii ya sasa nayo ikipata msimamizi na mtekelezaji mzuri huenda uzalendo ukarejea. Mwl alitumia hii hii.
Uzalendo kwa itikadi ya ccm ni kisifia viongozi wakuu hasahsa rais. Kwa itikadi yetu sisi wengine huo ni unyumbu
Ngoswe penzi kitovu cha uzembe na Edwin Semzaba, ni kitabu kilichoandikwa miaka mingi lakini kumbe kilikuwa kinaona leo!Tuko tayari hata kuvunja viti vya Uwanja wa Taifa kwa sababu za kibinafsi bila kujua kuwa hiyo ni mali ya walipakodi wa Tanzania.
Majina ya Kikomunisti haya siyapendi kama nini 😉Kamaradi Stefano,
Sheria yoyote inayoumiza nchi au wananchi haina uzalendo ndani yake na wazalendo wanajua cha kufanya.Tuelimishe zaidi kwenye haya:-
Vipi ukiipenda nchi yako lakini unavunja sheria zake huo ni uzalendo?
Huyo Pita ni raia wa Bongo?Vipi Peter Greenberg anayeipenda nchi limbwende Tz ni mzalendo?
Kwani Tanzania ni nchi yao?Wawekezaji wa kigeni wanaoipenda nchi ni wazalendo (kama pia hawavunji sheria zake)?
Duh!Wakurugenzi wa makampuni ya kigeni yaliyoingia mikataba tata na taifa ni wazalendo?
Wewe ni mzalendo wa Marekani? UK? uganda? Malawi?Hivi uzalendo unahusu uraia?
GTHKwenye mchango wako aya ya pili na tatu umenishawishi kwa ziada Kamaradi Stefano.
Katiba mpya ndio inaleta uzalendo au sio?🤔🙌KATIBA MPYA
Mwalimu aliongoza maiti hai. Siku CCM itaacha kutawala nchi hii kwa shuruti uzalendo utakuwepo.