Serikali ilianzisha uzalishaji wa ngano toka mashamba ya Hanang' Complex Mkoani Manyara na uzalishaji ulikuwa mkubwa sana. Serikali ilipoanza ubinafsishaji mashamba haya yaliuzwa kwa bei ya kutupwa.
Wengi wa wafanyabiashara waliouziwa mashamba haya hawayaendelezi na mengi yamebaki kama mahame. Ninaishauri Serikali kufikiria upya kuyarudisha mashamba haya Serikalini kwa wale ambao wamekataa kuyaendeleza na kuwapa wafanyabiashara wenye nia ya kulima ngano.
Ni vema Serikali ikakaa chini na Bakressa ili apewe mashamba haya kwa ajili ya kulima ngano kuliko kuagiza ngano toka nje ya nchi kitu ambacho kinaigharimu Serikali kutumia fedha nyingi za kigeni.