mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,188
- 1,090
Watoto wa taifa hili ni vijana wa kesho hivyo vijana wa leo ni viongozi wa leo na kesho..Tutafakari hulka Za vijana wa kesho je pasipo kufinyangwa vema wataweza kumlea vema mama Tanzania?
Pamoja na uwepo wa mifumo mbali mbali ya kufunda wataalaamu na viongozi bado kama taifa tuna ombwe la kuibua viongozi madhubuti wenye uzalendo usio na shaka..
Ni ukweli usiopingingika wana siasa wana nguvu kubwa sana ktk kufanya maamuzi ya kulididimiza taifa au kuliendeleza na kulikuza..Ili kujenga taifa lolote maono thabiti yanapaswa kuwepo ndani ya viongozi tunaowafinyanga. Nini kiu,nia,matamanio, maono, Uwezo wa ya yeyote mwenye nia ya kuomba ridhaa ya ujumbe, Uenyekiti, Ukatibu, udiwani, Ubunge, Uwaziri, Urais n.k.
Nini kiu ya wanaopigana vikumbo kutaka kupewa mamlaka au madaraka?Ni utukufu? Uzalendo?Vipawa?Utajiri?Ukwasi?Sifa na Heshima?Urithi?…
Lazima tufinyange na kurutubisha viongozi ktk uzalendo usio na mashaka,Uadirifu mkuu,Utakatifu kisiasa,Usafi wa nia/Nafsi/Mioyo na Ufahamu. Na hili lifanyike pasipo kujali itikadi Kwa Maana ya yeyote mwenye matamanio ya kuwa kiongozi sharti afinyangwe na kufanyika mhitimu Kwa maslahi mapana ya taifa kimaendeleo,Kiusalama na mengineo.