SoC02 Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa

Stories of Change - 2022 Competition

Kahumbi Lumola

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2012
Posts
359
Reaction score
2,569
Andiko hili lina sehemu kuu nne; Utangulizi, Mada, Mapendekezo na Hitimisho.

SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina J. Mohamed kwenye Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani ya Tarehe 20 Mei 2019 alisema "Mchango wa nyuki ni muhimu sana katika juhudi za Dunia za kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu...". Nimechagua maneno haya katika Utangulizi wa Andiko langu kwa Dhumuni la kuonyesha umuhimu wa Nyuki katika kuiwezesha Dunia kutimiza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.

Na kwa umuhimu zaidi ni vema wasomaji wangu wakafahamu kwamba Viumbe Hai vyote Duniani kwa mjumuiko wetu ili tuweze kuendelea kuishi tunahitaji Usawa wa Kiikolojia na ili tupate Usawa wa Kiikolojia, mimea na maua ni sehemu muhimu ya kutimiza Usawa huo na Nyuki amethibitika kuwa ndiye Mchavushaji Bora zaidi wa mimea na maua ambapo huchangia Uchavushaji kwa asilimia 90 ya mimea na maua yote Duniani.

Kabla ya kuingia kwenye Kiini cha Mada ni vema wasomaji wote wakafahamu maana ya neno Uchavushaji (Pollination).

Ni nini maana ya Uchavushaji? Uchavushaji ni uhamishaji wa chavua kutoka kwenye (sehemu ya kiume) ya mmea hadi kwenye unyanyapaa (sehemu ya kike) ya mmea, baadaye kuwezesha kurutubisha na kuzalisha mbegu zaidi za mimea au maua husika.

SEHEMU YA PILI: MADA
Katika sehemu hii ya Kiini cha Mada nitaelezea Kazi za Nyuki na faida zake katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo;
(I) KAZI ZA NYUKI NJE YA MZINGA.
Nyuki hufanya Uchavushaji wa Mazao ya Chakula kwa Theluthi moja ya Mazao yote ya Chakula cha Binadamu. Bila ya Nyuki Binadamu tutapoteza Theluthi moja ya Mazao tunayoyategemea kwa chakula Mfano; alizeti, mboga za majani na baadhi ya matunda kwa mfano Parachichi Tikiti Maji n.k.

(II) KAZI ZA NYUKI NDANI YA MZINGA
Nyuki ndani ya Mzinga huzalisha bidhaa sita kama ifuatavyo; Asali (Honey), Nta (Beeswax), Gundi (Propolis), Chavua (Pollen), Maziwa ya Kifalme ya Nyuki (Royal Jelly) na Sumu ya Nyuki (Bee Venom). Bidhaa ambazo hutumika kwa matumizi mengi ya Binadamu kama vile; chakula na Dawa.

Nyuki huchangia Dola za Marekani Bilioni 160 kila Mwaka kwenye Uchumi wa Dunia kutokana na kazi zao Ndani na Nje ya Mzinga kama nilivyoeleza hapo juu.

SEHEMU YA TATU: MAPENDEKEZO
Kama tulivyoona umuhimu wa Nyuki kwenye Utangulizi na Kiini cha Mada ninapendekeza mambo yafuatayo ili tuzalishe Nyuki kwa wingi zaidi na Jamii iwathamini kwa kuwalinda.

(i) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lifanye marekebisho ya Sheria ya Nyuki ya Mwaka 2002.

Ninapendekeza kwenye Sheria hii yafanyike marekebisho katika maeneo mawili mahsusi; mosi katika Adhabu na pili katika Zawadi kwenye Vifungu vifuatavyo;

-Mosi Vifungu vya Adhabu
• Kifungu cha 43, Kifungu cha 44(1) a-f pamoja na Kifungu cha 44(2) vifungu ambavyo Adhabu ya Faini haizidi milioni 1 na Kifungo hakizidi mwaka mmoja. Ninapendekeza marekebisho ya Sheria hii yafanyike ili Adhabu zilizotajwa kwenye kila kifungu ziwe angalau mara 3 ya zilivyo sasa.

-Pili Kifungu cha Zawadi
• Vilevile Kifungu cha 50 katika Sheria hii kinachotaja kiwango cha zawadi endapo Mtuhumiwa atakutwa na Hatia ya akahukumiwa kulipa Faini aliyetoa Taarifa kuhusu Uhalifu dhidi ya Nyuki hupewa zawadi. Hivyo ninapendekeza marekebisho ya Kifungu hiki na zawadi iwe sawa na Faini iliyotolewa na aliyehukumiwa. Kwa lengo la kuhamasisha zaidi Jamii katika kutoa Taarifa za Uhalifu dhidi ya Nyuki.

(ii) Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wadau wa Sanaa itengeneze Matangazo kwenye Luninga na Radio ya Kutaja Faida za Nyuki na kusisitiza Jamii nzima kuwalinda kwa lengo la kuongeza Elimu kwa Jamii kuhusu Nyuki. Hii iende sambamba na kuweka mabango makubwa na madogo.

(iii) Ninapendekeza Marekebisho ya Mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari.
•Lianzishwe Somo rasmi kwa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Nyuki.
•Vilevile Wanafunzi wa Kidato cha 3 waongezewe Option ya kuchagua Mchepuo wa Kilimo na Mifugo ambapo ndani yake wajifunze kuhusu Nyuki. Tofauti na sasa Kidato cha 3 huchagua michepuo ya sayansi, arts na Biashara.
•Na somo la Nyuki (Beekeeping Study) liendelee na kwa Kidato cha 5 na cha 6 liingizwe kama General Study.

(iv) Natambua kwa sasa kuna Vyuo viwili Nchini; UDSM na SUA ambavyo vinatoa Shahada za masomo ya Nyuki. Ninapendekeza Serikali iwape kipaumbele Wanafunzi watakaochagua Kozi za Shahada ya Nyuki kupata Mikopo kupitia HESLB kwa asilimia 100. Hii iende sambamba kwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii wawawezeshe Wanafunzi wa Stashahada Chakula na Fedha ya Mafunzo kwa Vitendo kama inavyofanya kwa Wanafunzi wa Stashahada katika Vyuo vya DIT, MUST na ATC Na kwa baadae Serikali ianzishe Taasisi ya Elimu ya juu ya masomo ya Nyuki katika Stashahada na Shahada mbalimbali.

(v) Kwa kuwa Nyuki ni Mchavushaji Bora zaidi kwenye zao la Alizeti. Ninapendekeza kwa Mwaka ujao wa Fedha Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii iwawezeshe wakulima wa Alizeti kuweka Mizinga ya Nyuki kwenye mashamba yao ili Uchavushaji ufanyike kwa wingi zaidi na mavuno ya Alizeti yaongezeke. Serikali iwatumie Wahitimu wa Shahada na Stashahada za Masomo ya Nyuki kutoka SUA na UDSM kwa ajili ya kuwapa ujuzi zaidi wakulima wa Alizeti jinsi ya kufuga Nyuki kwenye mashamba yao kwa Tija zaidi.

SEHEMU YA NNE: HITIMISHO
Wakati mtazamo wa Dunia kwa ujumla unamuona Nyuki kama mdudu muhimu kusaidia kutimiza Malengo Na. 14 na Na.15 ya Maendeleo Endelevu.

Ninahitimisha kwa kutoa Maoni yangu kwamba kwa Nchi zote zinazoendelea hususani Tanzania, Nyuki anaweza kusaidia kutimiza Malengo mengine ya Maendeleo Endelevu ambayo ni Na.1 Kuondoa Umaskini, Na. 2 Kutokomeza Njaa na Na.8 Kazi zenye Staha na Ukuaji wa Uchumi. Mtazamo huu utaleta muelekeo Mpya ambapo Serikali iandae Sera na Sheria Rafiki zaidi kwa Nyuki kwenye mipango yake ya Mwaka ujao wa Fedha. Ni matumani yangu endapo Serikali itashika haya mpaka kufikia Mwaka 2030 (The UN 2030 Agenda) sisi Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika Vita dhidi ya Ujinga, Umaskini, Maradhi na Ukosefu wa Ajira.

Ahsante sana nawasilisha.
 
Upvote 102
Kamati ya kitaifa ya ushauri wa ufugaji nyuki ni kamati maalumu inayoundwa na wadau wa sekta ya nyuki ikiwa na majukumu yafuatayo.
1.Kutoa ushauri kwa waziri wa maliasili na utalii juu maswala yanayohusu sekta ndogo ya nyuki
2.Kutunga sera na marekebisho ya sheria za sekta ya ufugaji nyuki nchini.
Asante kwa ufafanuzi
 
Ahsante sana Mkuu naomba nipate mawasiliano yako tafadhali
 
Kamati ya kitaifa ya ushauri wa ufugaji nyuki ni kamati maalumu inayoundwa na wadau wa sekta ya nyuki ikiwa na majukumu yafuatayo.
1.Kutoa ushauri kwa waziri wa maliasili na utalii juu maswala yanayohusu sekta ndogo ya nyuki
2.Kutunga sera na marekebisho ya sheria za sekta ya ufugaji nyuki nchini.
Wajumbe wa hiyo kmt wanakuwa wanalipwa au ndio kamat tu ya kujitolea?
 
Kamati ya kitaifa ya ushauri wa ufugaji nyuki ni kamati maalumu inayoundwa na wadau wa sekta ya nyuki ikiwa na majukumu yafuatayo.
1.Kutoa ushauri kwa waziri wa maliasili na utalii juu maswala yanayohusu sekta ndogo ya nyuki
2.Kutunga sera na marekebisho ya sheria za sekta ya ufugaji nyuki nchini.
Wajumbe wa hiyo kamat ya nyuk wanateuliwa na nani na vigezo gani vinahitajika.
 
Kwa MUHUTASARI [emoji116]

Sumu ya nyuki huongeza usambazaji damu ndani ya mwili, na kuruhusu damu ipite kwa urahisi katika mipaka ya
kila chembe chembe hai za mwili. Mshipa inayosafirisha damu
mwilini hupanuliwa, na msukumo wa damu huteremka. Sumu ya
nyuki vile vile hulegeza misuli na huweza kupunguza maumivu ya
misuli.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, wafugaji nyuki wanaepushwa
kuugua maradhi kadhaa kutokana na kudungwa miiba ya nyuki hivyo
kuingiziwa mwilini sumu ya nyuki, mfululizo. Maradhi
wanayoepushwa nayo ni kwa mfano baridi yabisi, maumivu ya viungo
na saratani/kansa.

Soma zaidi kwenye Kitabu Cha Mazao ya Nyuki kilichoandikwa na Marieke na wenzake
Unatema madini sana mkuu. Kusema za ukweli andiko lako limekuwa na faida sana. Yaani sijaona tena mkuu. Mimi Binafsi nimefaidika sana na nimejifunza sana kupitia andiko lako
 
Wajumbe wa hiyo kamat ya nyuk wanateuliwa na nani na vigezo gani vinahitajika.
Wajumbe wanateuliwa na waziri na kigezo kikubwa ni kuwa mdau ambae umetoa mchango mkubwa sana kwenye sekta ya nyuki. Mfano kipindi ilipozindulia mwaka 2019 na waziri Kingwangala, Mwenyekiti wake alikuwa ni Mkurugenzi wa Asali ya bibi(Jina limenitoka) na wadau wengineo
 
Ahsante sana kaka kwa Taarifa. Ubarikiwe sana
 
Andiko hili lina sehemu kuu nne; Utangulizi, Mada, Mapendekezo na Hitimisho.

SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina J. Mohamed kwenye Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani ya Tarehe 20 Mei 2019 alisema "Mchango wa nyuki ni muhimu sana katika juhudi za Dunia za kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu...". Nimechagua maneno haya katika Utangulizi wa Andiko langu kwa Dhumuni la kuonyesha umuhimu wa Nyuki katika kuiwezesha Dunia kutimiza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.

Na kwa umuhimu zaidi ni vema wasomaji wangu wakafahamu kwamba Viumbe Hai vyote Duniani kwa mjumuiko wetu ili tuweze kuendelea kuishi tunahitaji Usawa wa Kiikolojia na ili tupate Usawa wa Kiikolojia, mimea na maua ni sehemu muhimu ya kutimiza Usawa huo na Nyuki amethibitika kuwa ndiye Mchavushaji Bora zaidi wa mimea na maua ambapo huchangia Uchavushaji kwa asilimia 90 ya mimea na maua yote Duniani.

Kabla ya kuingia kwenye Kiini cha Mada ni vema wasomaji wote wakafahamu maana ya neno Uchavushaji (Pollination).

Ni nini maana ya Uchavushaji? Uchavushaji ni uhamishaji wa chavua kutoka kwenye (sehemu ya kiume) ya mmea hadi kwenye unyanyapaa (sehemu ya kike) ya mmea, baadaye kuwezesha kurutubisha na kuzalisha mbegu zaidi za mimea au maua husika.

SEHEMU YA PILI: MADA
Katika sehemu hii ya Kiini cha Mada nitaelezea Kazi za Nyuki na faida zake katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo;
(I) KAZI ZA NYUKI NJE YA MZINGA.
Nyuki hufanya Uchavushaji wa Mazao ya Chakula kwa Theluthi moja ya Mazao yote ya Chakula cha Binadamu. Bila ya Nyuki Binadamu tutapoteza Theluthi moja ya Mazao tunayoyategemea kwa chakula Mfano; alizeti, mboga za majani na baadhi ya matunda kwa mfano Parachichi Tikiti Maji n.k.

(II) KAZI ZA NYUKI NDANI YA MZINGA
Nyuki ndani ya Mzinga huzalisha bidhaa sita kama ifuatavyo; Asali (Honey), Nta (Beeswax), Gundi (Propolis), Chavua (Pollen), Maziwa ya Kifalme ya Nyuki (Royal Jelly) na Sumu ya Nyuki (Bee Venom). Bidhaa ambazo hutumika kwa matumizi mengi ya Binadamu kama vile; chakula na Dawa.

Nyuki huchangia Dola za Marekani Bilioni 160 kila Mwaka kwenye Uchumi wa Dunia kutokana na kazi zao Ndani na Nje ya Mzinga kama nilivyoeleza hapo juu.

SEHEMU YA TATU: MAPENDEKEZO
Kama tulivyoona umuhimu wa Nyuki kwenye Utangulizi na Kiini cha Mada ninapendekeza mambo yafuatayo ili tuzalishe Nyuki kwa wingi zaidi na Jamii iwathamini kwa kuwalinda.

(i) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lifanye marekebisho ya Sheria ya Nyuki ya Mwaka 2002.

Ninapendekeza kwenye Sheria hii yafanyike marekebisho katika maeneo mawili mahsusi; mosi katika Adhabu na pili katika Zawadi kwenye Vifungu vifuatavyo;

-Mosi Vifungu vya Adhabu
• Kifungu cha 43, Kifungu cha 44(1) a-f pamoja na Kifungu cha 44(2) vifungu ambavyo Adhabu ya Faini haizidi milioni 1 na Kifungo hakizidi mwaka mmoja. Ninapendekeza marekebisho ya Sheria hii yafanyike ili Adhabu zilizotajwa kwenye kila kifungu ziwe angalau mara 3 ya zilivyo sasa.

-Pili Kifungu cha Zawadi
• Vilevile Kifungu cha 50 katika Sheria hii kinachotaja kiwango cha zawadi endapo Mtuhumiwa atakutwa na Hatia ya akahukumiwa kulipa Faini aliyetoa Taarifa kuhusu Uhalifu dhidi ya Nyuki hupewa zawadi. Hivyo ninapendekeza marekebisho ya Kifungu hiki na zawadi iwe sawa na Faini iliyotolewa na aliyehukumiwa. Kwa lengo la kuhamasisha zaidi Jamii katika kutoa Taarifa za Uhalifu dhidi ya Nyuki.

(ii) Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wadau wa Sanaa itengeneze Matangazo kwenye Luninga na Radio ya Kutaja Faida za Nyuki na kusisitiza Jamii nzima kuwalinda kwa lengo la kuongeza Elimu kwa Jamii kuhusu Nyuki. Hii iende sambamba na kuweka mabango makubwa na madogo.

(iii) Ninapendekeza Marekebisho ya Mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari.
•Lianzishwe Somo rasmi kwa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Nyuki.
•Vilevile Wanafunzi wa Kidato cha 3 waongezewe Option ya kuchagua Mchepuo wa Kilimo na Mifugo ambapo ndani yake wajifunze kuhusu Nyuki. Tofauti na sasa Kidato cha 3 huchagua michepuo ya sayansi, arts na Biashara.
•Na somo la Nyuki (Beekeeping Study) liendelee na kwa Kidato cha 5 na cha 6 liingizwe kama General Study.

(iv) Natambua kwa sasa kuna Vyuo viwili Nchini; UDSM na SUA ambavyo vinatoa Shahada za masomo ya Nyuki. Ninapendekeza Serikali iwape kipaumbele Wanafunzi watakaochagua Kozi za Shahada ya Nyuki kupata Mikopo kupitia HESLB kwa asilimia 100. Hii iende sambamba kwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii wawawezeshe Wanafunzi wa Stashahada Chakula na Fedha ya Mafunzo kwa Vitendo kama inavyofanya kwa Wanafunzi wa Stashahada katika Vyuo vya DIT, MUST na ATC Na kwa baadae Serikali ianzishe Taasisi ya Elimu ya juu ya masomo ya Nyuki katika Stashahada na Shahada mbalimbali.

(v) Kwa kuwa Nyuki ni Mchavushaji Bora zaidi kwenye zao la Alizeti. Ninapendekeza kwa Mwaka ujao wa Fedha Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii iwawezeshe wakulima wa Alizeti kuweka Mizinga ya Nyuki kwenye mashamba yao ili Uchavushaji ufanyike kwa wingi zaidi na mavuno ya Alizeti yaongezeke. Serikali iwatumie Wahitimu wa Shahada na Stashahada za Masomo ya Nyuki kutoka SUA na UDSM kwa ajili ya kuwapa ujuzi zaidi wakulima wa Alizeti jinsi ya kufuga Nyuki kwenye mashamba yao kwa Tija zaidi.

SEHEMU YA NNE: HITIMISHO
Wakati mtazamo wa Dunia kwa ujumla unamuona Nyuki kama mdudu muhimu kusaidia kutimiza Malengo Na. 14 na Na.15 ya Maendeleo Endelevu.

Ninahitimisha kwa kutoa Maoni yangu kwamba kwa Nchi zote zinazoendelea hususani Tanzania, Nyuki anaweza kusaidia kutimiza Malengo mengine ya Maendeleo Endelevu ambayo ni Na.1 Kuondoa Umaskini, Na. 2 Kutokomeza Njaa na Na.8 Kazi zenye Staha na Ukuaji wa Uchumi. Mtazamo huu utaleta muelekeo Mpya ambapo Serikali iandae Sera na Sheria Rafiki zaidi kwa Nyuki kwenye mipango yake ya Mwaka ujao wa Fedha. Ni matumani yangu endapo Serikali itashika haya mpaka kufikia Mwaka 2030 (The UN 2030 Agenda) sisi Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika Vita dhidi ya Ujinga, Umaskini, Maradhi na Ukosefu wa Ajira.

Ahsante sana nawasilisha.
Kwa yeyote anayefahamu naomba kuuliza juu ya faida ya Maziwa ya nyuki ile wanaita jelli ya Kifalme chakula cha malkia
 
Jeli ya kifalme ni tiba ya tumbo, ini, na matatizo ya
uyeyushaji chakula tumboni,

Husaidia msukumo mwingi wa damu, huongezahamu ya chakula,

Vilevile Husaidia watu wenye upungufu wa uzito, uchovu, kukosa utulivu, kukosa
usingizi, ujauzito wenye matatizo, adha ya kusimama hedhi.

Hii ni kwa uchache lakini faida zake ni nyingi sana
 
Naweza kufuga maeneo ya nyumbani wasilete madhara kwa watoto na wapita njia?

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Ufugaji wenye Tija pamoja na mambo mengine ni ule ambao hufanyika katika mashamba Maalumu.

Ni ngumu kuzuia madhara ya Nyuki kwa watoto kwasababu watoto wenyewe ndio wanaweza kuwachokoza Nyuki na
 
Jeli ya kifalme ni tiba ya tumbo, ini, na matatizo ya
uyeyushaji chakula tumboni,

Husaidia msukumo mwingi wa damu, huongezahamu ya chakula,

Vilevile Husaidia watu wenye upungufu wa uzito, uchovu, kukosa utulivu, kukosa
usingizi, ujauzito wenye matatizo, adha ya kusimama hedhi.

Hii ni kwa uchache lakini faida zake ni nyingi sana
Pia nataka kuongezea hapo Mr. Lumola faida za Maziwa ya nyuki
kufanya mtu awe mkakamavu, mwenye afya na asiyechoka. Huweza
kuliwa katika hali ya asili, au baada ya kuchanganywa na asali.
 
Ahsante sana

Your additional points are very useful

[emoji1374] [emoji1374] [emoji1374] [emoji1374]
 
Back
Top Bottom