SoC02 Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa

Stories of Change - 2022 Competition

Kahumbi Lumola

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2012
Posts
359
Reaction score
2,569
Andiko hili lina sehemu kuu nne; Utangulizi, Mada, Mapendekezo na Hitimisho.

SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina J. Mohamed kwenye Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani ya Tarehe 20 Mei 2019 alisema "Mchango wa nyuki ni muhimu sana katika juhudi za Dunia za kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu...". Nimechagua maneno haya katika Utangulizi wa Andiko langu kwa Dhumuni la kuonyesha umuhimu wa Nyuki katika kuiwezesha Dunia kutimiza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.

Na kwa umuhimu zaidi ni vema wasomaji wangu wakafahamu kwamba Viumbe Hai vyote Duniani kwa mjumuiko wetu ili tuweze kuendelea kuishi tunahitaji Usawa wa Kiikolojia na ili tupate Usawa wa Kiikolojia, mimea na maua ni sehemu muhimu ya kutimiza Usawa huo na Nyuki amethibitika kuwa ndiye Mchavushaji Bora zaidi wa mimea na maua ambapo huchangia Uchavushaji kwa asilimia 90 ya mimea na maua yote Duniani.

Kabla ya kuingia kwenye Kiini cha Mada ni vema wasomaji wote wakafahamu maana ya neno Uchavushaji (Pollination).

Ni nini maana ya Uchavushaji? Uchavushaji ni uhamishaji wa chavua kutoka kwenye (sehemu ya kiume) ya mmea hadi kwenye unyanyapaa (sehemu ya kike) ya mmea, baadaye kuwezesha kurutubisha na kuzalisha mbegu zaidi za mimea au maua husika.

SEHEMU YA PILI: MADA
Katika sehemu hii ya Kiini cha Mada nitaelezea Kazi za Nyuki na faida zake katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo;
(I) KAZI ZA NYUKI NJE YA MZINGA.
Nyuki hufanya Uchavushaji wa Mazao ya Chakula kwa Theluthi moja ya Mazao yote ya Chakula cha Binadamu. Bila ya Nyuki Binadamu tutapoteza Theluthi moja ya Mazao tunayoyategemea kwa chakula Mfano; alizeti, mboga za majani na baadhi ya matunda kwa mfano Parachichi Tikiti Maji n.k.

(II) KAZI ZA NYUKI NDANI YA MZINGA
Nyuki ndani ya Mzinga huzalisha bidhaa sita kama ifuatavyo; Asali (Honey), Nta (Beeswax), Gundi (Propolis), Chavua (Pollen), Maziwa ya Kifalme ya Nyuki (Royal Jelly) na Sumu ya Nyuki (Bee Venom). Bidhaa ambazo hutumika kwa matumizi mengi ya Binadamu kama vile; chakula na Dawa.

Nyuki huchangia Dola za Marekani Bilioni 160 kila Mwaka kwenye Uchumi wa Dunia kutokana na kazi zao Ndani na Nje ya Mzinga kama nilivyoeleza hapo juu.

SEHEMU YA TATU: MAPENDEKEZO
Kama tulivyoona umuhimu wa Nyuki kwenye Utangulizi na Kiini cha Mada ninapendekeza mambo yafuatayo ili tuzalishe Nyuki kwa wingi zaidi na Jamii iwathamini kwa kuwalinda.

(i) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lifanye marekebisho ya Sheria ya Nyuki ya Mwaka 2002.

Ninapendekeza kwenye Sheria hii yafanyike marekebisho katika maeneo mawili mahsusi; mosi katika Adhabu na pili katika Zawadi kwenye Vifungu vifuatavyo;

-Mosi Vifungu vya Adhabu
• Kifungu cha 43, Kifungu cha 44(1) a-f pamoja na Kifungu cha 44(2) vifungu ambavyo Adhabu ya Faini haizidi milioni 1 na Kifungo hakizidi mwaka mmoja. Ninapendekeza marekebisho ya Sheria hii yafanyike ili Adhabu zilizotajwa kwenye kila kifungu ziwe angalau mara 3 ya zilivyo sasa.

-Pili Kifungu cha Zawadi
• Vilevile Kifungu cha 50 katika Sheria hii kinachotaja kiwango cha zawadi endapo Mtuhumiwa atakutwa na Hatia ya akahukumiwa kulipa Faini aliyetoa Taarifa kuhusu Uhalifu dhidi ya Nyuki hupewa zawadi. Hivyo ninapendekeza marekebisho ya Kifungu hiki na zawadi iwe sawa na Faini iliyotolewa na aliyehukumiwa. Kwa lengo la kuhamasisha zaidi Jamii katika kutoa Taarifa za Uhalifu dhidi ya Nyuki.

(ii) Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wadau wa Sanaa itengeneze Matangazo kwenye Luninga na Radio ya Kutaja Faida za Nyuki na kusisitiza Jamii nzima kuwalinda kwa lengo la kuongeza Elimu kwa Jamii kuhusu Nyuki. Hii iende sambamba na kuweka mabango makubwa na madogo.

(iii) Ninapendekeza Marekebisho ya Mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari.
•Lianzishwe Somo rasmi kwa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Nyuki.
•Vilevile Wanafunzi wa Kidato cha 3 waongezewe Option ya kuchagua Mchepuo wa Kilimo na Mifugo ambapo ndani yake wajifunze kuhusu Nyuki. Tofauti na sasa Kidato cha 3 huchagua michepuo ya sayansi, arts na Biashara.
•Na somo la Nyuki (Beekeeping Study) liendelee na kwa Kidato cha 5 na cha 6 liingizwe kama General Study.

(iv) Natambua kwa sasa kuna Vyuo viwili Nchini; UDSM na SUA ambavyo vinatoa Shahada za masomo ya Nyuki. Ninapendekeza Serikali iwape kipaumbele Wanafunzi watakaochagua Kozi za Shahada ya Nyuki kupata Mikopo kupitia HESLB kwa asilimia 100. Hii iende sambamba kwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii wawawezeshe Wanafunzi wa Stashahada Chakula na Fedha ya Mafunzo kwa Vitendo kama inavyofanya kwa Wanafunzi wa Stashahada katika Vyuo vya DIT, MUST na ATC Na kwa baadae Serikali ianzishe Taasisi ya Elimu ya juu ya masomo ya Nyuki katika Stashahada na Shahada mbalimbali.

(v) Kwa kuwa Nyuki ni Mchavushaji Bora zaidi kwenye zao la Alizeti. Ninapendekeza kwa Mwaka ujao wa Fedha Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii iwawezeshe wakulima wa Alizeti kuweka Mizinga ya Nyuki kwenye mashamba yao ili Uchavushaji ufanyike kwa wingi zaidi na mavuno ya Alizeti yaongezeke. Serikali iwatumie Wahitimu wa Shahada na Stashahada za Masomo ya Nyuki kutoka SUA na UDSM kwa ajili ya kuwapa ujuzi zaidi wakulima wa Alizeti jinsi ya kufuga Nyuki kwenye mashamba yao kwa Tija zaidi.

SEHEMU YA NNE: HITIMISHO
Wakati mtazamo wa Dunia kwa ujumla unamuona Nyuki kama mdudu muhimu kusaidia kutimiza Malengo Na. 14 na Na.15 ya Maendeleo Endelevu.

Ninahitimisha kwa kutoa Maoni yangu kwamba kwa Nchi zote zinazoendelea hususani Tanzania, Nyuki anaweza kusaidia kutimiza Malengo mengine ya Maendeleo Endelevu ambayo ni Na.1 Kuondoa Umaskini, Na. 2 Kutokomeza Njaa na Na.8 Kazi zenye Staha na Ukuaji wa Uchumi. Mtazamo huu utaleta muelekeo Mpya ambapo Serikali iandae Sera na Sheria Rafiki zaidi kwa Nyuki kwenye mipango yake ya Mwaka ujao wa Fedha. Ni matumani yangu endapo Serikali itashika haya mpaka kufikia Mwaka 2030 (The UN 2030 Agenda) sisi Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika Vita dhidi ya Ujinga, Umaskini, Maradhi na Ukosefu wa Ajira.

Ahsante sana nawasilisha.
 
Upvote 102
Adhabu zipo mkuu!!
Ukikamatwa na mkaa ambao hauna kibali chombo kilichosafirisha mkaa kinakamatwa na mkaa pia.
Wakala wa huduma za misitu(TFS) ndio wanahusika kwenye hili eneo.
Mimi shida yangu ipo hapo kwanini Serikali wanatoa vibali kwenye mkaa? Hivi kwann Binadamu tunakosa akili? Tunajua tunahitaji miti ili tuweze kuishi kwanini mkaa usipigwe marufuku? Mimi ndio maana nachukia wanasiasa. Ni lazima tuyatunze Mazingira yetu. No way tunapoendea tutakuwa pabaya Sana. Hizi hatua zichukuliwe mapema sana. Tupikie gesi Serikali waweke ruzuku kila mtu apate jiko la gesi mpk Vijijini Zaid ya hapo hakuna namna
 
Hata wewe pia unaweza kutengeneza mafuta ya nta ukiwa nyumbani kwako mkuu!!!
Faida zilizopo kwenye nta ukiitumia katika vipodozi kama sabuni na mafuta ni faida za kiafya kama ilivyo kwenye muarobaini au alovera, na ukiweza kuchanganya hivyo huleta matokeo mazuri zaidi katika ngozi.
Nta ina vitu ambayo ni anti-inflamatory na anti-bacteria ikitumiwa katika ngozi pia hutunza unyevunyevu zaidi kwenye ngozi na huondoa seli zilizokufa katika ngozi kwa urahisi zaidi.
This is very interesting, sikuwahi kujua kama nyuki ana faida nyingi kiasi hiki.
 
Mimi shida yangu ipo hapo kwanini Serikali wanatoa vibali kwenye mkaa? Hivi kwann Binadamu tunakosa akili? Tunajua tunahitaji miti ili tuweze kuishi kwanini mkaa usipigwe marufuku? Mimi ndio maana nachukia wanasiasa. Ni lazima tuyatunze Mazingira yetu. No way tunapoendea tutakuwa pabaya Sana. Hizi hatua zichukuliwe mapema sana. Tupikie gesi Serikali waweke ruzuku kila mtu apate jiko la gesi mpk Vijijini Zaid ya hapo hakuna namna
Upo sahihi mkuu mimi nakuunga mkono
 
Adhabu zipo mkuu!!
Ukikamatwa na mkaa ambao hauna kibali chombo kilichosafirisha mkaa kinakamatwa na mkaa pia.
Wakala wa huduma za misitu(TFS) ndio wanahusika kwenye hili eneo.
Adhabu zipo lkn Hali ni mby sana Mimi nazani ni bora kuwe na mabalozi kwenye jamii yaani isiwe tu maafisa misitu. Au wewe unaonaje kaka. Mimi ni Mgeni kwenye hii field ila kupitia makala hii nimejua mengi sana kuhusu nyuki. Nitakutafuta nataka nifuge nyuki wadogo
 
Karibu sana Bagamoyo Tufuge Nyuki
 
Andiko hili lina sehemu kuu nne; Utangulizi, Mada, Mapendekezo na Hitimisho.

SEHEMU YA KWANZA: UTANGULIZI
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi Amina J. Mohamed kwenye Maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani ya Tarehe 20 Mei 2019 alisema "Mchango wa nyuki ni muhimu sana katika juhudi za Dunia za kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu...". Nimechagua maneno haya katika Utangulizi wa Andiko langu kwa Dhumuni la kuonyesha umuhimu wa Nyuki katika kuiwezesha Dunia kutimiza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.

Na kwa umuhimu zaidi ni vema wasomaji wangu wakafahamu kwamba Viumbe Hai vyote Duniani kwa mjumuiko wetu ili tuweze kuendelea kuishi tunahitaji Usawa wa Kiikolojia na ili tupate Usawa wa Kiikolojia, mimea na maua ni sehemu muhimu ya kutimiza Usawa huo na Nyuki amethibitika kuwa ndiye Mchavushaji Bora zaidi wa mimea na maua ambapo huchangia Uchavushaji kwa asilimia 90 ya mimea na maua yote Duniani.

Kabla ya kuingia kwenye Kiini cha Mada ni vema wasomaji wote wakafahamu maana ya neno Uchavushaji (Pollination).

Ni nini maana ya Uchavushaji? Uchavushaji ni uhamishaji wa chavua kutoka kwenye (sehemu ya kiume) ya mmea hadi kwenye unyanyapaa (sehemu ya kike) ya mmea, baadaye kuwezesha kurutubisha na kuzalisha mbegu zaidi za mimea au maua husika.

SEHEMU YA PILI: MADA
Katika sehemu hii ya Kiini cha Mada nitaelezea Kazi za Nyuki na faida zake katika sehemu kuu mbili kama ifuatavyo;
(I) KAZI ZA NYUKI NJE YA MZINGA.
Nyuki hufanya Uchavushaji wa Mazao ya Chakula kwa Theluthi moja ya Mazao yote ya Chakula cha Binadamu. Bila ya Nyuki Binadamu tutapoteza Theluthi moja ya Mazao tunayoyategemea kwa chakula Mfano; alizeti, mboga za majani na baadhi ya matunda kwa mfano Parachichi Tikiti Maji n.k.

(II) KAZI ZA NYUKI NDANI YA MZINGA
Nyuki ndani ya Mzinga huzalisha bidhaa sita kama ifuatavyo; Asali (Honey), Nta (Beeswax), Gundi (Propolis), Chavua (Pollen), Maziwa ya Kifalme ya Nyuki (Royal Jelly) na Sumu ya Nyuki (Bee Venom). Bidhaa ambazo hutumika kwa matumizi mengi ya Binadamu kama vile; chakula na Dawa.

Nyuki huchangia Dola za Marekani Bilioni 160 kila Mwaka kwenye Uchumi wa Dunia kutokana na kazi zao Ndani na Nje ya Mzinga kama nilivyoeleza hapo juu.

SEHEMU YA TATU: MAPENDEKEZO
Kama tulivyoona umuhimu wa Nyuki kwenye Utangulizi na Kiini cha Mada ninapendekeza mambo yafuatayo ili tuzalishe Nyuki kwa wingi zaidi na Jamii iwathamini kwa kuwalinda.

(i) Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lifanye marekebisho ya Sheria ya Nyuki ya Mwaka 2002.

Ninapendekeza kwenye Sheria hii yafanyike marekebisho katika maeneo mawili mahsusi; mosi katika Adhabu na pili katika Zawadi kwenye Vifungu vifuatavyo;

-Mosi Vifungu vya Adhabu
• Kifungu cha 43, Kifungu cha 44(1) a-f pamoja na Kifungu cha 44(2) vifungu ambavyo Adhabu ya Faini haizidi milioni 1 na Kifungo hakizidi mwaka mmoja. Ninapendekeza marekebisho ya Sheria hii yafanyike ili Adhabu zilizotajwa kwenye kila kifungu ziwe angalau mara 3 ya zilivyo sasa.

-Pili Kifungu cha Zawadi
• Vilevile Kifungu cha 50 katika Sheria hii kinachotaja kiwango cha zawadi endapo Mtuhumiwa atakutwa na Hatia ya akahukumiwa kulipa Faini aliyetoa Taarifa kuhusu Uhalifu dhidi ya Nyuki hupewa zawadi. Hivyo ninapendekeza marekebisho ya Kifungu hiki na zawadi iwe sawa na Faini iliyotolewa na aliyehukumiwa. Kwa lengo la kuhamasisha zaidi Jamii katika kutoa Taarifa za Uhalifu dhidi ya Nyuki.

(ii) Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wadau wa Sanaa itengeneze Matangazo kwenye Luninga na Radio ya Kutaja Faida za Nyuki na kusisitiza Jamii nzima kuwalinda kwa lengo la kuongeza Elimu kwa Jamii kuhusu Nyuki. Hii iende sambamba na kuweka mabango makubwa na madogo.

(iii) Ninapendekeza Marekebisho ya Mitaala kwa Shule za Msingi na Sekondari.
•Lianzishwe Somo rasmi kwa Shule za Msingi na Sekondari kuhusu Nyuki.
•Vilevile Wanafunzi wa Kidato cha 3 waongezewe Option ya kuchagua Mchepuo wa Kilimo na Mifugo ambapo ndani yake wajifunze kuhusu Nyuki. Tofauti na sasa Kidato cha 3 huchagua michepuo ya sayansi, arts na Biashara.
•Na somo la Nyuki (Beekeeping Study) liendelee na kwa Kidato cha 5 na cha 6 liingizwe kama General Study.

(iv) Natambua kwa sasa kuna Vyuo viwili Nchini; UDSM na SUA ambavyo vinatoa Shahada za masomo ya Nyuki. Ninapendekeza Serikali iwape kipaumbele Wanafunzi watakaochagua Kozi za Shahada ya Nyuki kupata Mikopo kupitia HESLB kwa asilimia 100. Hii iende sambamba kwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii wawawezeshe Wanafunzi wa Stashahada Chakula na Fedha ya Mafunzo kwa Vitendo kama inavyofanya kwa Wanafunzi wa Stashahada katika Vyuo vya DIT, MUST na ATC Na kwa baadae Serikali ianzishe Taasisi ya Elimu ya juu ya masomo ya Nyuki katika Stashahada na Shahada mbalimbali.

(v) Kwa kuwa Nyuki ni Mchavushaji Bora zaidi kwenye zao la Alizeti. Ninapendekeza kwa Mwaka ujao wa Fedha Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii iwawezeshe wakulima wa Alizeti kuweka Mizinga ya Nyuki kwenye mashamba yao ili Uchavushaji ufanyike kwa wingi zaidi na mavuno ya Alizeti yaongezeke. Serikali iwatumie Wahitimu wa Shahada na Stashahada za Masomo ya Nyuki kutoka SUA na UDSM kwa ajili ya kuwapa ujuzi zaidi wakulima wa Alizeti jinsi ya kufuga Nyuki kwenye mashamba yao kwa Tija zaidi.

SEHEMU YA NNE: HITIMISHO
Wakati mtazamo wa Dunia kwa ujumla unamuona Nyuki kama mdudu muhimu kusaidia kutimiza Malengo Na. 14 na Na.15 ya Maendeleo Endelevu.

Ninahitimisha kwa kutoa Maoni yangu kwamba kwa Nchi zote zinazoendelea hususani Tanzania, Nyuki anaweza kusaidia kutimiza Malengo mengine ya Maendeleo Endelevu ambayo ni Na.1 Kuondoa Umaskini, Na. 2 Kutokomeza Njaa na Na.8 Kazi zenye Staha na Ukuaji wa Uchumi. Mtazamo huu utaleta muelekeo Mpya ambapo Serikali iandae Sera na Sheria Rafiki zaidi kwa Nyuki kwenye mipango yake ya Mwaka ujao wa Fedha. Ni matumani yangu endapo Serikali itashika haya mpaka kufikia Mwaka 2030 (The UN 2030 Agenda) sisi Tanzania tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika Vita dhidi ya Ujinga, Umaskini, Maradhi na Ukosefu wa Ajira.

Ahsante sana nawasilisha.
Tuongeze ufahamu kuhusu bidhaa za Nyuki watu wengi wanauliza

1. Maziwa ya Kifalme

Huzalishwa na nyuki vibarua wachanga ambao hula asali na chavua nyingi ili kutengeneza chakula chenye virutubisho vingi ambacho kwa kimombo hujulikana kama (royal jelly).

Chakula hiki hulishwa mabuu wachanga ili waweze kukua haraka na malkia aweze kutaga mayai na asizeeke haraka.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba wazee watumiapo chakula hiki huwafanya kuonekana bado vijana na huwaongezea nguvu za kiume.

Wadau wengine wanaweza kuongezea faida zingine za Royal Jelly.

PIRO tycoon4
 
Napata faida nyingi sana kuhusu nyuki. Endelea kutupa madini mdogo wangu
 
Tuongeze ufahamu kuhusu bidhaa za Nyuki watu wengi wanauliza

1. Maziwa ya Kifalme

Huzalishwa na nyuki vibarua wachanga ambao hula asali na chavua nyingi ili kutengeneza chakula chenye virutubisho vingi ambacho kwa kimombo hujulikana kama (royal jelly).

Chakula hiki hulishwa mabuu wachanga ili waweze kukua haraka na malkia aweze kutaga mayai na asizeeke haraka.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba wazee watumiapo chakula hiki huwafanya kuonekana bado vijana na huwaongezea nguvu za kiume.

Wadau wengine wanaweza kuongezea faida zingine za Royal Jelly.

PIRO tycoon4
Royal jelly (Maziwa ya kifalme).
Inaimarisha sana mfumo wa kinga ya mwili,pia nzuri kwa ngozi na nywele!! Kiufupi mungu aliweka maajabu mengi sana apa,ndio sababu mtu umri umeenda lakini ngozi bado ya under-17.
Royal jelly ni "super food" katika koloni la nyuki, yenye virutubisho vingi ambavyo vinaongeza nguvu nyingi kwa malkia na kumfanya atage kwa wingi,faida kwa mwanadamu ni nyingi ila faida na sifa kubwa ni kufanya usionekane mzee mapema.
Bahati mbaya ni kati ya zao ambalo sio rahisi kuonekana mara kwa mara ndani ya mzinga.
 
Ahsante kwa kuweka ufafanuzi zaidi[emoji1374]
 
Ubarikiwe [emoji8]
 
Tuongeze ufahamu kuhusu bidhaa za Nyuki watu wengi wanauliza

1. Maziwa ya Kifalme

Huzalishwa na nyuki vibarua wachanga ambao hula asali na chavua nyingi ili kutengeneza chakula chenye virutubisho vingi ambacho kwa kimombo hujulikana kama (royal jelly).

Chakula hiki hulishwa mabuu wachanga ili waweze kukua haraka na malkia aweze kutaga mayai na asizeeke haraka.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha kwamba wazee watumiapo chakula hiki huwafanya kuonekana bado vijana na huwaongezea nguvu za kiume.

Wadau wengine wanaweza kuongezea faida zingine za Royal Jelly.

PIRO tycoon4
Salute kwako andiko lako limetufungua wengi
 
Hata wewe pia unaweza kutengeneza mafuta ya nta ukiwa nyumbani kwako mkuu!!!
Faida zilizopo kwenye nta ukiitumia katika vipodozi kama sabuni na mafuta ni faida za kiafya kama ilivyo kwenye muarobaini au alovera, na ukiweza kuchanganya hivyo huleta matokeo mazuri zaidi katika ngozi.
Nta ina vitu ambayo ni anti-inflamatory na anti-bacteria ikitumiwa katika ngozi pia hutunza unyevunyevu zaidi kwenye ngozi na huondoa seli zilizokufa katika ngozi kwa urahisi zaidi.
Fantastic
 
Back
Top Bottom