Mimi ni mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri. Pia ni mshauri wa biashara, ninatoa ushauri wa biashara na kuendesha mafunzo ya ujasiriamali, kuandaa michanganuo kuombea mikopo benki na misaada kutoka kwa wafadhili. Mwaka 2009 niliwezesha wateja wangu kupata mikopo ya Tshs. milioni 300 toka mabenki mbali mbali, niliendesha mafunzo na kutoa ushauri kwa watu mbali mbali, Kati ya mafunzo ambayo niliyafanya na yakafana ni yale ambayo yaliandaliwa na Mwang'amba Communication na kufanyika Millenium tower, ambapo wawezeshaji tulikuwa mimi( Charles Nazi) James Mwangamba, Eric Shigongo, Martin Kaswahili, Mr Msemwa na Chris Mauki.
Utafiti nilioufanya nimegundua kwamba watu wengi wanakwama kuendesha biashara zao au kupata maendeleo ya kiuchumi kwa sababu ya kukosa maarifa ya ujasiriamali.Kwa hiyo nimeamua kuwa lengo langu ni kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watanzania wote. Kutokana na wito wa mwenzetu natoa ofa kwa Wana JF ambao wako Dar kuwa niko tayali kutoa mafunzo ya ujasiriamali bila malipo yoyote. Nauomba uongozi wa JF usaidie kutafuta ukumbi. Kwa mawasiliano zaidi kwa wanaohitaji kupata mafunzo hayo na uongozi wa JF wanaweza kunipigia simu namba 0755394701. Pia kama una kikundi cha watu ambao wanahitaji kupata mafunzo mnaweza kuniita niko tayali kutoa mafunzo bila malipo mradi mniandalie mahali pa kukutana na muwe idadi isiyokuwa chini ya watu 10.
CHARLES NAZI
Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara