Tufundishane Ujasiriamali

Hii imekaa vizuri... Nakubaliana kabisa na "who care?" kuwa mjasirimali lazima asiwe mwoga na awe nauwezo wa kufikiri. Ni lazima uweze ku-connect the dots hakuna ubabaishaji.

"An enterpreneur is a person who WORK ON a business NOT in it". (Michael Gerber)

Mfano kama wewe biashara yao ya kuuza chumvi gengeni itasimama endapo utashindwa kuisimamia (mf ukiwa mgonjwa) basi hiyo siyo biashara ya mjasirimali bali ni JOB.

Biashara ya mjasirimali ina endeshwa kwa mfumo (system) ambao hautegemei mtu fulani bali mfumo wenye kufuata kanuni.

Mimi binafsi biashara zangu zamtandao (intenert business) zina cashflow hata kama mimi nikiwa nimelala usiku. Nimetengeneza mfumo ambao hautegemei msimamizi wala sehemu ninayo ishi, hata kama nikifa leo hii cashflow itaendelea.

Jamiiforum ni mfano mzuri wa mfumo was kijasirimali ambao unaingiza pesa kwa kutumia matangazo (contextual advertising) ambapo ukibonyeza tuu hilo tangazo pesa inaingia JF hata kama admin yupo mars.

Biashara ya mjasirimali lazima iwe scalable ie lazima uweze kuipanua. Fikiria biashara yako kama vie prototype ya nyingi kama hiyo. kwa mfano kama nimefanya research na nimeona kwamba "weightloss" ni niche nzuri na yenye faida basi nitatafuta sub niches nyingi za kuambatanisha main product, mfano losing weight for middle age executives, weight loss for fat husbands, weight loss for women who just had a baby n.k

Biashara ya mjasirimali inamtengenezea maisha (kiswahili kitamu LOL) huyo anaye miliki siyo kumuibia muda wake kwa kuutumia kuiendesha.

Just my 2 cents
 
Nashukuru kwa wale wote wanaoendelea kuchangia mada.
Kwa mfano mtu mmoja ana kiwanja maeneo ya Bunju na hana uwezo wa kujenga kwa sasa kutokana na ufinyu wa mshahara anaolipwa lakini benki ana shilingi milioni moja. Amekaa na kufikiria kuwa ni bora akafungua kituo cha kufyetulia tofali na kuuza sementi hapo lakini ukumbuke benki ana shilingi milioni moja tu na kazini kwake hawadhamini wafanyakazi kuchukua mikopo benki kwa kutumia jina la kampuni. Na ukumbuke kuwa kuna mahitaji mengi ili kuweza kuanzisha kituo hicho cha kufyetulia tofali mbali na kiwanja ambacho tayari kipo. Mahitaji mengine yanayotakiwa na yeye hana ni kama vile kontena au servant quatre, materials kama sementi, mapipa ya maji, pamoja na wafyetua matofali ambao watahitaji fedha za kuwalipa wakati kazi inaanza pamoja na mahitaji mengine madogo madogo.

Je hii ni biashara au ujasiriamali kwa mujibu wa maelezo ya Who Cares?
Je atafanyaje hili aweze kuianzisha kazi hii anayotaka kuanza kuifanya?
 
Am a farmer cum civil servant . Nafuga nguruwe kwa kwenda mbele, Kuku wa kienyeji, migomba ya kisasa etc. Then nimeajiriwa, nalipwa sh. 280,000 kwa mwezi mzima. Nikiuza mayai napata 300,000. Nikiuza Kitimoto moja tu kwa mwezi napata 200,000-300,000 kuendana na uzito.
Nikiuza kuku 50 tu kwa mwezi napata 200,000.00. Nyumbani nina mahindi gunia 5 , mchele , na maharage. Mama analima mboga mboga ,na midizi. So cost of foods kwangu ni negligible.
Nina watoto wawili wa primary school na madogo wawili relatives secondary ya private.
Ninaendesha pickup na starlet. Ila nina mpango wa kununua lililobora zaidi kifamilia.

Jumla minimum ni napata 700,000. mazimum 1,500,000.
Zile 280,000 nawalipa wafanyakazi wawili kila m2 140,000 na wako very happy. Shamba nilinunua eka moja u nusu miaka hiyooo na ndipo nimejenga ikulu yangu. Here I am . Mjasiriamali/ civil servant.
 
Ubarikiwe sana, naamini wengi tutafaidika nimechukua namba, wanajamii Forum jamani si tungechagua mmoja wetu awe coordinator hapa tujiorodheshe na tuanze darasa mara moja?
 
Ubarikiwe sana, naamini wengi tutafaidika nimechukua namba, wanajamii Forum jamani si tungechagua mmoja wetu awe coordinator hapa tujiorodheshe na tuanze darasa mara moja?
Ningekuwa DSM ningefanya hii kazi lakini kwa sasa niko nje ya jiji. Ambaye anafikiri anaweza kufanya hili please ajitokeze na kutoa mrejesho hapa na kuwa anawasiliana na Babalao moja kwa moja kwa namba ya simu aliyotoa.

Lakini pia namuomba Babalao kama ana literatures ambazo zinahusiana na mada hii atuorodheshee hapa ili tuweze kuzisoma na kujenga uelewa zaidi.
 
Wazo ni zuri sana.
Ila napendekeza kwa wale watu ambao wako tayari kutoa mada mbali mbali kuhusu ujasiriamali ni vyema tukakubaliana kwamba wapewe muda wa kutosha na kuwe na siku maalum ya kuwasilisha ili wadau wote tuweze kujua kwama leo kuna somo ukumbini.
 

Huyo ni mjasiriamali. Kitendo cha kugundua kwamba kiwanja ambacho hawezi kukiendeleza kwa sasa kwa kukosa fedha bali anaweza kukitumia kupata fedha kinamweka kwenye kundi la wajasiliamari.

Mjasiliamari ni mtu anayeweza kuona fursa za kutengeneza pesa pale ambapo wengine hawaoni. Na ndio maana mfano Dar kuna biashara nyingi sana za kuigana. Wafanyabiasha wengi wa Dar (sio wajasiliamari) wana madala dala, hair saloon za kike na kiume (barber shop), baa za kitimoto na bia na migahawa!

Huyo mwenye kiwanja cha kwake, na mtaji wa shilingi milioni moja tayari ana mtaji mkubwa kuliko anavyofikiria. Tatizo lake anaona kwamba hizo milioni moja ni kidogo sana kwa hiyo hawezi kuanzisha hiyo biashara. Pia ana mawazo ya kwenda kukopa benki.

Mjasiliamari halisi huwa anaanza na mtaji sifuri na haendekezi mambo ya mikopo. Kama ameweza kujikusanyia shilingi milioni moja kama ''saving'' pamoja na kiwanja bila kukopa, ipo siku atajikuta ana Shs. milioni mia moja na kiwanda cha simenti bila mkopo! Achotakiwa kufanya kuendeleza kanuni zake za kujikusanyia mapato, kujiwekea akiba na kufirikia fursa nyingine za kujiongezea kipato.

Looser always say it is possible but it is very difficult, where as winners always say it is difficult but it is possible.
 

keep it up nakuombea uzidi kufanikiwa zaidi
 

Kaka asante sana!

Safari tumeianza na niseme umeianzisha hapa kwa kutupa changamoto na fikra!

Usichoke mkuu unatufaa wengi!
 
ukweli hii mada imenivutia sana wandugu, kwani mimi binafsi ninataka kuwa mjasiliamali bt cjui wapi pa kuanzia hivyo nadhani hiyo elimu itatusaidia sana endapo itapata nafasi hapa jamvini na mada mbali mbali zikatolewa na wawezeshaji.
 

Hapo pekundu ndo hasa kwa wajasiriamali kupaangalia sana, chukua senks
 
If you can't make money without money, you can't make money with money. Period!
 
Tunashukuru kwa mada nzuri! jamani tupeni upeo wa kuwa wajasiriamali itatudaidia sana cha msingi ni kuwa na moyo wa kujifunza ujasiriamali. Mimi nilifungua mashine za kusaga na kukoboa Tandale lakini biashara ilinishinda nadhani ni elimu duni ambayo sikuwa nayo kwa kweli usimamizi nao ulikuwa mbovu mpaka ninavyoongea mashine ya kusaga na moja ya kukoboa zipo na nitatafuta mtu wa kuzinunua...kama kuna mtu yuko interested tunaweza kuwasiliana kwa bethmsk@yahoo.com akaenda kuziona tukaongea biashara..
 
Mimi nilikuwa na wazo ambalo nahisi litatusaidia wote sisi tulio nje ya DSM na nyie mlio DSM. Wazo hili ni la kumuomba babalao pamoja na kutoa offer ya kutoa mafunzo kwa watu kumi (10) nilikuwa namuomba awe anatoa mada hapa kwenye thread hii kwani inaonekana ndio sehemu ambayo watu walioko sehemu mbalimbali wanaweza kufaidika zaidi. Sijapinga wazo la kutoa elimu kwa wale walioko DSM ila nimejaribu kuangalia jinsi ambavyo huyu mtaalamu wa masuala ya ujasiriamali anaweza kusaidia watu wengi zaidi. Sijui wezangu mnaonaje wazo hili. Kama limekaa vizuri tumsisitizie babalao hta kwa PM
 
please naomba hili wazo/ombi liende hata kwa mwingine yeyote mwenye kuweza kutoa elimu hii hapa hapa JF
 
If you can't make money without money, you can't make money with money. Period!

You are right. You can read a book Rich Daddy Poor Daddy. Kinapatikana Novel Idea. Ni kizuri sana kwa kujifunza ujasiriamali.
 
jamaniiiiii...mjasiriamali haitaji MTAJI....kwa maana ya PESA...mjasiriamali anaitaji MTAJI WA AKILI NA UBUNIFU ULIO TOFAUTI NA WENGI KATIKA MAZINGIRA YALIYOMZUNGUKA...
1-akili/wazo
2-Ubunifu tofauti
3-Mazingira yaliyomzunguka

Hivi ni vitu muhimu sana kwa mjasiriamali wa kweli..baada ya hapo...vitu kama PESA ndipo hufuata ili kuliwezesha (lile wazo lilojaa ubunifu tofauti katika mazingira yalokuzunguka)liwe la kweli...
Natoa changamoto kwa wadau..jaribu kujiba mazoezi ya say unaishi sinza..kila nyumba imejaa baa na guest house na kitimoto, fastfood, boutique etc...jiulize unachoweza kufanya katika hizo biashara wanazoigana ukaweza KUSIMAMA kidedea na tofauti na wao then ukaouza au kuingiza pesa kuliko wao...hapa ndipo napoongelea mtaji wa AKILI...sio pesa
 
Heshima sana mkuu, hili nalo neno. Lakini pia wadau wanasema vitu ambavyo wewe ni mteja (ambavyo hutumia sehemu kubwa ya kipato chako) yaweza kuwa sehemu ya ubunifu unapofikiria kuanzisha biashara. Kielelezo ukiwa wewe mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…