Kuna rafiki yangu alikua anaongoza kwa mdomo anasema kwenye mbio watu wanaenda kudanga. Kuna siku nimekutana nae kwenye starehe huko akaanza nisifia nimepungua blah blah nikamwambia sababu nakimbia nikamkaribisha na yeye kwenye programs zetu za Goba kila Jumanne na Alhamisi.
After two weeks zikaja tena hizi discussion za marathon na umalaya kwenye group yetu ya chuo. Akasema yeye hawezi kukimbia kwanza mbio ni umalaya na hawezi kukimbia hata km 1 sio mambo yake.
Tukaonana tena mwezi wa kwanza mwanzoni akaona nilivyopungua tena.
Sasa hivi nakimbia nae kila siku. Tena siku nyingine nikitoka ofisini nimevurugwa sitaki kukimbia anaenda mwenyewe kukimbia.
Last week anasema boyfriend wake kamsifia alivyopungua na akanishukuru nimemsaidia kuweza kukimbia na kumfutia mentality ya kujudge wengine kwa kitu ambacho wachache wanakifanya.
Haya mambo ni akili yako maana hata iweje hayakwepeki kunapokua na jinsia mbili tofauti
Sent using
Jamii Forums mobile app