Tufute ruzuku kwa vyama na badala yake iende kwa wakulima na wafanyakazi

Tufute ruzuku kwa vyama na badala yake iende kwa wakulima na wafanyakazi

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Huwa najiuliza mantiki ya kuvipa vyama vya siasa ruzuku kila mwezi. Zaidi ya makelele, migogoro, kelele, na usanii vinazalisha nini ikilinganishwa na wakulima na wafugani kwanza, na pili wafanyakazi?

Kwanini hii ruzuku ya kila mwezi kwanza, isiende kwa wakulima na itakayobaki iende kwa wafanyakazi kama vile walimu, madaktari, wazoa taka, madereva na wengine?
 
Vyama vyote vilivyosajiliwa ofisi ya mtungi kikiwemo na chama tawala hawawezi ruhusu hili litokee
 
..CCM inapokea 3.2 Billion kila mwezi kama ruzuku.

..sasa hawa wataishi vipi ikiwa ruzuku itafutwa?

..CCM wanavyovuruga uchaguzi lengo lao ni wasikose hilo donge nono la ruzuku.
 
CCM kwa nini wanapokea ruzuku wakati wao wenyewe si walipa Kodi wazuri?

Majengo na viwanja vya Mpira walivyopora toka kwa umma, Kodi zake na fedha zinazoingia kutokana na majengo na viwanja hivyo, wanalipa Kodi?

Kama CCM wengekuwa wanalipa Kodi, kila mwaka wangekuwa ni miongoni mwa walipa Kodi wakubwa.

Hivi CCM ni kwa nini wanapewa ruzuku? Wanaendesha nchi hovyo ufisadi umetapakaa Kila mahali halafu bado wanapewa ruzuku?

Hiki chama kinachowatia umaskini watanzania ni kwa nini wanapewa ruzuku. Hawa watu wanaovuruga uchaguzi kila wakati wa chaguzi kwa nini wapewe ruzuku?
 
Back
Top Bottom