Tuheshimiane

Kitty Galore

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2011
Posts
345
Reaction score
100
Wewe tumefahamiana katika mazingira ya kistaarabu, tumezoeana kama binadamu wengine bila kuvuka mipaka, najua umeoa ila mimi hujui status yangu kama nimeolewa au niko single, kutokana na kwamba haikuhusu, sasa kinachokufanya unipigie simu saa 5 kasoro 7 usiku ni nini? wakati hata huo mchana huna la maana la kuniambia? Najuta kukupa namba yangu, kama matumizi yako ya simu ndo haya. Wanaume wengine mnakera sana
 
Usiku ndo akili zinakuja baada ya kupigwa baridi.
 
Reactions: Mbu
Wasilianeni kwa pm. Habari za kupeana namba zinaleta uzushi uzushi tu.
 
jf is never boring lol

duh............kavulana gani hako jamani?

mchana 'kanashindwa kuzungumza'
halafu usiku ndo 'kanaanza utundu?????

si bora kangekuwa kavulana kangeeleweka
 
alikuwa anakusalimia tu jamani!..kwa hiyo kama hukataka akupigie simu umempa namba ya nini?acha hizo bana.au kosa hakutuma ile vocha(natania).mia
 
Haujui siku hizi kuanzia 4-1 asubuhi tigo-tigo ni bure kuanzia dk ya 3.

Hiyo inaitwa bana matumizi.
 
hayupo humu JF, hii ni kero nimeona ngoja nije kuitolea JF angalau moyo wangu utulie, nimekwazika sana

kama hayuko Jf ina maana hataupata ujumbe wako na ataendelea kukusumbua.

Mimi huwa msichana akinipa huwa namuuliza masharti ya kumpigia simu. Kwanza simu za usiku ni za kitoto.
 
hayupo humu JF, hii ni kero nimeona ngoja nije kuitolea JF angalau moyo wangu utulie, nimekwazika sana

sijui ulikutana wapi na jamaa ingawa huwa kuna mazingira unalazimika kutoa namba bila kupenda ila kama ni mambo ya kimtandaoni usirudie.
 
Hapo palipokolezwa.Hukupaswa kumpa namba wakati hata mchana hana la kukwambia.kwa akili zake chafu alifikiri unampa ili akupigie wakati ana la kukwambia(usiku) kwa kuwa anajua kuwa unajua mchana hana la kukwambia.
 

Ndio mkome kutoa namba kwa vinega
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…