Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Walinda legacy bado wapo katika msiba, wanatukana kila kiongozi wa nchi hii aliyepita. Hawana staha hata kwa baba wa Taifa, wanasema eti hata yeye hajafanya kitu isipokuwa ni Magufuli tu ndo kafanya yote.
Walinda Legacy wanahoji kuwa kwa miaka yote 50 iliyopita mbona ikulu haikujengwa ila ikajengwa na Magufuli? Kwao miaka 12 ya Hayati baba wa Taifa kutojenga Ikulu Dodoma tangu uamuzi wa serikali mwaka 1972 ni kama uzembe hivi wa Mwalimu. Hapo sijasema kuhusu maraisi waliofuata, hao ndo wanawaona hamna kitu kabisaa!
Sisi wengine huwa tunaheshimu kauli za Marehemu. Marehemu alisema hana shida za sifa kutoka kwa watu, bali akisifiwa na mkewe mama Janeti inamtosha!. Sasa nashangaa walinda legacy badala ya kuheshimu wosia huu muhimu sana wa mtu wao, wanataka kila mmoja asimame kwenye podium aimbe sifa za Magufuli. Hebu kuweni na heshima kidogo basi kwa marehemu.
kitu kingine walinda Legacy huwa wanapenda kutukumbusha kuwa tumuache Marehemu apumzike. Sasa hapa mnatuchanganya kidogo. Asiposemwa mnalalamika, Akisemwa mnalalamika. Sasa chagueni moja tuendelee kumzungumzia au tumwache apumzike Chato?
Nataka niwakumbushe tu, Shule ya msingi ambayo Magufuli alisoma, Ilijengwa na baba wa Taifa, Chuo kikuu alichosoma kilijengwa na baba wa Taifa, Hospitali ya Mzena aliyofia ilijengwa na baba wa Taifa. Hata hospitali ya Miembe alipokuwa na file lake ilijengwa na baba wa Taifa.
Kwa hiyo mnaposema kuwa nchi hii Maraisi waliopita hawakufanya kitu, basi angalau kuweni na heshima kidogo kwa baba wa Taifa mwalimu Julius kambarage Nyerere!