Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,557
- 8,673
Nakosa la kusema. Hivi hawa watu ambao wanajitokeza sasa na kusema hayo yote walikuwa wapi siku zote hizo tangia JK aingie madarakani mpaka sasa?
Naona hawa pia walikuwa sehemu ya kusebabisha matatizo hayo yote, na sasa sijui wameitilafiana wapi tena mpaka imefikia hatua ya kuanikana hadharani.
Yawezekana ni mbinu pia ya ccm kujipanga kwa 2010.
"MADHAMBI YAO YANAWATAFUNA, WATATAJANA WOTE NA MAKOSA WALIYOTENDA KILA MMOJA" Tutaona na kusikia mengi kuelekea 2010
Lakini kwa huyu bwana yamezidi.....na kuombwa kuishawishi Marekani eti kuwaondolea vizuizi Cuba, nguvu hiyo hana....fuatilia uone...
Mkuu, kauli zinazotolewa na viongozi kote duniani hufika kwenye audience wanazotarajia mapema sana. Kiongozi huyo wa CUBA alitumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe wake kwa Rais wa Marekani. Vile vile, anaamini kuwa JK ana uhusiano mzuri tu na Rais Obama na hivyo anaweza kusaidia kufikisha ombi hilo kwa urahisi zaidi. Hii yote haimaanishi kuwa JK ni kiongozi mahiri, hodari au mwenye kuchukua hatua sahihi kwa ajili ya utawala alioomba watu wake.
Unaweza kupendwa na mtu mwenye hadhi kubwa na akakusikiliza maombi yako kwa kuwa tu una udhaifu mkubwa na hivyo anakuonea huruma. Lakini pia tunajua interest za mataifa kama Marekani kwa nchi kama zetu huwa si zenye manufaa makubwa kwetu. Hivyo inawezekana kabisa kuwa Rais huyo wa CUBA anajua kuwa JK anaweza kutoa fadhila zaidi kwa Marekani na yeye akafaidika. Yote yanawezekana.
Sijui unahitaji uthibitisho gani kuwa JK ameshindwa mara nyingi kufanya maamuzi magumu. Ila kuna taarifa za kutosha sana kuhusiana na hilo.
Usemi wa wahenga (busara zisizopinda) ni zaidi ya urithi, hivyo mjinga mmoja kama huyu hawezi na wala asepewe nafasi ya kuwafanya wazee wote waonekane mbumbumbu. Hivyo inabidi tumchukulie kama wale wazee wanaobaka watoto wadogo, kitendo hiki kimetokea mara nyingi lakini sio kibali cha wazee wote kudharaulika.Wahenga walisema uzee dawa. Lakini ukifuatilia hoja na maneno ya baadhi ya wazee wetu kama Makamba unajiuliza kama kweli bado huu usemi wa wahenga unaendelea kuwa na maana iliyotarajiwa.
ikitokea kaweza kuishawishi? Maana yeye ni rais wa kwanza kuarikwa white house na obama hivi obama anaarika marais wadhaifu?
Kwa kiasi fulani wazee wetu hawa wanafanya hivyo sio kwa kuipenda NCHI yao. Wanafanya hivyo kwa kuwa utawala wa sasa umewatupa nje. Hawana ushawishi tena. Wengine kwa kuwa "mgombea wao" hakufanikiwa. Vinginevyo kuukosoa uongozi ulioko madarakani huku uking'ang'ania kuwa mwanachama wa chama hichohicho ni kichekesho.Kuna 'mentality' ambayo naamini si nzuri, tunayo Watanzania. Hata kama mtu alikuwa kiongozi huko nyuma, akapigwa chini (kufulia), haruhusiwi kutoa maoni yake? Kuna watu wanaamini kabisa kwamba, Malecela, Mkapa, Sumaye, Salim, Warioba, Salimin, Jumbe, na wengineo wote waliowahi kushika madaraka huko nyuma, hawaruhusiwa kuukosoa uongozi uliopo madarakani. Ni kweli hivi ndivyo inavyotakiwa?
Siamini kama ni rais dhaifu Tanzania na Africa,hayo ni maono na fikra binafsi ambazo ni ruhusa mtu kutoa maoni kikatiba.
Kam kunauthibithisho wa udhaifu wa Rais JK basi uelezwe ili tuone ukweli wa habari hizi.
Hivi juzi Rais wa CUBA amekaririwa akimuomba Rais JK amsaidia kuishawishi Marekani kuondoa vizuizi iliyoiwekea CUBA.Sasa najiuliza hivi unawexza kwenda kumuomba usaidizi wowote ule kwa mtu aliyedhaifu?
Uozo wote tunaouona sana sidhani kama umetokea kwa awamu hii ya nne pekee,kwa awamu zote zilizopita kulikuwa na mapungufu mengi sana.
Kwa kiasi fulani wazee wetu hawa wanafanya hivyo sio kwa kuipenda NCHI yao. Wanafanya hivyo kwa kuwa utawala wa sasa umewatupa nje. Hawana ushawishi tena. Wengine kwa kuwa "mgombea wao" hakufanikiwa. Vinginevyo kuukosoa uongozi ulioko madarakani huku uking'ang'ania kuwa mwanachama wa chama hichohicho ni kichekesho.
Kuna 'mentality' ambayo naamini si nzuri, tunayo Watanzania. Hata kama mtu alikuwa kiongozi huko nyuma, akapigwa chini (kufulia), haruhusiwi kutoa maoni yake? Kuna watu wanaamini kabisa kwamba, Malecela, Mkapa, Sumaye, Salim, Warioba, Salimin, Jumbe, na wengineo wote waliowahi kushika madaraka huko nyuma, hawaruhusiwa kuukosoa uongozi uliopo madarakani. Ni kweli hivi ndivyo inavyotakiwa?
Mkuu si siri mtu mwenye "mentality" ya jinsi hii ana kasoro au ameathirika physiologically , na anajaribu kuwashawishi watu wenye upeo wa kuchambua mambo waamini ule ujinga wake..!
Kama hututokubali kukosolewa basi hatutoweza kubadirika hata kidogo..!! Mzee Makamba lazima akubaliane na hali kwamba wakati wa porojo porojo na kunukuu mistari ya Bibilia na Miswafu ulishapitwa na wakati.
Huwezi kulazimisha picha ya kibakuli kuwa picha ya sahani japo zote ni picha za vyote vyombo vya kulia chakula ..!!
Kzi ipo mwaka huu...JK will be among the weakest president this country has in its history
Unajua Mkuu hata Mangula na marehemu Kolimba walipokuwa madarakani hawakuoni ubovu wa chama chao lakini walipokuwa nje waliona kasoro zote. Kumbuka Kolimba alivyosema kuwa CCM imekosa dira jinsi alivyoshukiwa na hata kufa!! leo hii Mangula naye ameona haya.. Usishangae Makamba akitoka ndio ataona kuwa alikuwa anatetea pumba!!
Wahenga walisema uzee dawa. Lakini ukifuatilia hoja na maneno ya baadhi ya wazee wetu kama Makamba unajiuliza kama kweli bado huu usemi wa wahenga unaendelea kuwa na maana iliyotarajiwa.
Udhaifu wake unatokana na kutothubutu kutoa maamuzi. Kila kitu kinaenda shaghala baghala. Hamna control ya mawaziri, watumishi, huoni kama huo ni udhaifu?]Nyuki;686174]Siamini kama ni rais dhaifu Tanzania na Africa,hayo ni maono na fikra binafsi ambazo ni ruhusa mtu kutoa maoni kikatiba.
Kam kunauthibithisho wa udhaifu wa Rais JK basi uelezwe ili tuone ukweli wa habari hizi.
Raisi wa CUBA hana data za utendaji wa JK. Inawezekana amechukua reference ya number of trips za Marekani alizofanya JK au pengine alikua anamkejeli. Angekua anamuheshimu angemtumia naibu waziri kumpokea?Hivi juzi Rais wa CUBA amekaririwa akimuomba Rais JK amsaidia kuishawishi Marekani kuondoa vizuizi iliyoiwekea CUBA.Sasa najiuliza hivi unawexza kwenda kumuomba usaidizi wowote ule kwa mtu aliyedhaifu?
Bado unabakia kuwa ni uozo na wala haijustify uzaifu wake mkuu wangu.Uozo wote tunaouona sana sidhani kama umetokea kwa awamu hii ya nne pekee,kwa awamu zote zilizopita kulikuwa na mapungufu mengi sana.