Tuhuma dhidi ya JK zaikoroga CCM

- ....... nina wasi wasi sana na amani ya taifa letu mbele ya safari!
FMEs!

Wala usiwe na wasiwasi. Amani mbele ya safari itakuwa ndio hii hii na wala haitopungua. Hapatatokea chochote, kwasababu sisi Watanzania ni BONGO na ni watu wenye kuabudu mizimu!!!!
 
Wala usiwe na wasiwasi. Amani mbele ya safari itakuwa ndio hii hii na wala haitopungua. Hapatatokea chochote, kwasababu sisi Watanzania ni BONGO na ni watu wenye kuabudu mizimu!!!!

- Hapana mkuu wangu, haya yanayosemwa sasa kwa kawaida huwa hayasemwi na viongozi, hii ni kwa mara ya kwanza Tanzania yanaanza kusemwa na wakulu, impact ni kubwa sana kwa wananchi, ndiio maaana siamini kwamba kina Makamba wanaweza kuyachukulia kama ni ya Yanga na Simba, alitakiwa kuyachukulia serious japo kidogo!

Respect.


FMEs!
 
Makamba yale si maneno yake ila ya Tambwe na yule jamaa aliyetoka CUF vichwa hivyo vumeisha oza .

Point!! Hato ni maneno ya mtu anayetegemea kufa hivi karibuni(kama alivyodai mwenhyewe) Hao uliowataja cheki matumbo yao, halafu uwaze wanachotafuta ni nini!!
 
Ukweli ni kwamba Makamba ni mteule wa huyo nanii anayemtetea, sasa lazima apigane manake hata mshahara wake uko juu. Sasa ni kibaraka kwa lugha yetu ya shule ya msingi, lakini kumbuka wanaolalamika nao wamelambwa mkono sasa nao wanahaha tu kiukweli sasa.

Siku zilishaanza kuhesabika kwa hawa mambwa wakubwa wanaoliendesha gurudumu hili muda wowote kinaweza kueleweka ushauri kwa wanaowania ku take cover wasogee kwa umakini bila papara watashinda
 
Point!! Hato ni maneno ya mtu anayetegemea kufa hivi karibuni(kama alivyodai mwenhyewe) Hao uliowataja cheki matumbo yao, halafu uwaze wanachotafuta ni nini!!
Duh! ama kweli duniani kuna mambo!
 
Aliyosema Makamba ni vituko kwa mtu maarufu kama yeye. Ingekuwa nchi hii ina watu makini na hasa wanachama wa CCM , kwa kusema hivyo tu mgosi Makamba angekuwa nje, sijui jeuri ya kusema mtu mmoja ni maarufu kuliko chama ina lengo gani, kwa kuwa CCM ndio chama tawala ina maana Kikwete ni zaidi ya Watanzania wote huo ni upuuzi Kikwete atatoka na TZ itabaki alikuwepo Nyerere sembuse Kikwete?

Na Nyerere hajawahi kusifiwa misifa ya ujinga namna hii
 
Mini naona Makamba atakiwa ashauriwe kupumzika kwani wakimuacha aendelee na huo wadhifa wake 2010 CCM watakuwa na wakati mgumu sana! hao matajiri anaosema wako wangapi? je masikini wanao changia kuku wakigoma kuchagua CCM huyo muhuza sura wake (Kikwete) atarudi ikuru? Labda huyu Ndugu Makamba anataka kutuambia kwamba nchi inaendeshwa kwa mtu kuuza sura na kutalii huku umaliza akiba yetu ya nchi ilihali wananchi wako wanakufa kwa njaa.
 
Moto wa akina Qares wazidi kuichoma CCM


MAKAMBA ANUKUHU BIBLIA, QU'RAAN KUMTETEA KIKWETE

Salim Said

MOTO uliowashwa kwenye kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere dhidi ya Rais Jakaya Kikwete umezidi kuiumiza CCM kiasi cha katibu mkuu wa chama hicho tawala kulazimika kuitisha mkutano mwingine na waandishi kutolea kujibu baadhi ya makombora.

Katika kongamano hilo, wachangiaji walimlaumu Rais Kikwete kwa kusita kufanya maamuzi magumu, huku waziri katika serikali ya awamu ya tatu, Matheo Qares akitaka CCM imtose iwapo atashindwa kufumba macho na kuwashughulikia watuhumiwa wa ufisadi kabla ya mwakani na waziri wa serikali ya awamu ya pili, Musa Nkangaa akieleza bayana kwamba chama kimepoteza mwelekeo.

Katibu huyo, Yusuf Makamba juzi alijibu tuhuma za mawaziri hao wawili akisema kuwa wanaotaka Kikwete atoswe na CCM kwenye urais mwaka 2010 ni wehu, lakini jana akaitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtetea mwenyekiti wake akitumia maandiko ya vitabu vitakatifu vya Msaafu na Biblia.

Makamba aliwaambia waandishi wa habari jana akisema: "Kama ilivyoandikwa na Warumi 13:1 'Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu na wao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu; pia katika Korani, Mwenyezi Mungu anasema 'mtiini Mungu na Mtume wake (S.A.W) na wale wenye mamlaka miongoni mwenu.'

Rais Kikwete ana mamlaka miongoni mwetu, kwa nini tunamvunjia heshima?"Nkangaa na Qares walikuwa wakuu wa mikoa na mimi pia nilikuwa mkuu wa mkoa, tunajuana vizuri.

"Wameyasema haya kwa sababu walikuwa na watu wao katika uchaguzi wa 2005, lakini hawakupita ndio maana wanakuja na madai haya. Hapa hatoswi mtu, watajiju."

Alisisitiza kuwa makada hao ni wehu na kwamba CCM haiwezi kukaa na kuwajadili ili kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa kuwa inatambua kuwa ni wehu.

"Tunajuana Qares aligombea ubunge Singida Mjini, lakini akakataliwa, amepauka kama shati na ndio mana labda ana chuki kwa sababu alishindwa na Mohammed Dewji,"alisema Makamba.

"Afadhali wale wehu wa barabarani, maana utamwona mwehu barabarani anatembea bila ya nguo, lakini akiiona CCM au msafara wa rais Kikwete husema 'CCM oyee…..JK oyeee," alisisitiza Makamba.

Makamba alisema CCM haiwezi kumtosa Rais Kikwete kama makada hao wanavyotaka kwa kuwa ni mtaji wake kisiasa.

"Kwa nini nasema ni mtaji wa CCM; moja ni kwamba Redet ilifanya utafiti Novemba 2008 na ikasema umaarufu wa Rais Kikwete ulikuwa asilimia 78.5, Sinovet Tanzania nao walifanya utafiti Julai 2009, walibaini pia kuwa umaarufu wa Rais Kikwete ni asilimia 86," alisema Makamba.

"Redet ikasema umaarufu wa CCM ni asilimia 72.8 wakati Sinovet Tanzania ikabaini asilimia 62.9 umaarufu wa CCM, kwa hiyo hapa tukiangalia Rais Kikwete amekizidi hata chama chake kwa umaarufu, hivyo huu ndio mtaji wetu," aliongeza.

Makamba alisisitiza kuwa "kutokana na hali hiyo, anayetaka JK atoswe 2010, huyo ni mwehu, asiyeitakia mema CCM na hawezi kusikilizwa ndani ya chama".

"Nani kama Kikwete ndani ya CCM? Hamna kwa sasa, yeye ndiye daraja letu tunamtegemea ili atuvushe 2010."

Alifafanua kuwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, CCM ilishinda kwa asilimia 93 kazi ambayo haikuwa ya katibu mkuu wake Yusuf Makamba wala mweka hazina wake, (Amosi) Makalla, bali ilikuwa kazi ya Rais Kikwete kutokana na kukubalika kwake.

Kuhusu madai kwamba rais hajachukua maamuzi mazito, Makamba alihoji: "Ni maamuzi gani hayo mazito wanayotaka rais achukue zaidi ya haya aliyochukua?

"Unamchukua rafiki yako, kiongozi mwenzako, uliyekuwa naye katika vikao vya baraza la mawaziri na bunge, unampeleka mahakamani, hayo hayajawa maamuzi mazito? Je, ni maamuzi gani mazito wanayoyataka?

"Lakini hata hao ambao wanatuhumiwa ni hadi uchunguzi ufanyike. Hivi kwa mfano ukisikia Makamba amefumaniwa utaandika tu, si mpaka ufanye uchunguzi?

"Pengine alikuwa na bukta yake anatoka mazoezi watu wanafukuza mwizi wakamwona yeye wakasema ametoka kwa mke wa mtu, hiyo haitakuwa haki hadi uchunguzi ufanyike. Kwa hiyo hawa watuhumiwa ni binadamu nao tuwatendee haki, tuwaonee huruma."

Moja ya mambo ambayo Kikwete amekuwa akilaumiwa kuwa anasita kuchukua hatua ni suala la kuwawajibisha watumishi walio chini ya mamlaka yake ambao Bunge liliazimia wachukuliwe hatua, akiwemo mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah kutokana na kutowajibika ipasavyo katika kashfa ya Richmond.

Alisema CCM iliunda chombo cha maadili ambacho kazi yake kubwa ni kuchunguza tuhuma za wanachama na kuchukua hatua kwa sababu haina utamaduni wa kutimuana kwa tuhuma.

Kuhusu madai kuwa chama hicho kimetekwa na matajiri na kwamba viongozi wanashindana kujilimbikizia mali, Makamba alisema CCM si chama cha matajiri, bali ina wanachama matajiri hivyo kitendo cha watu kusema ni chama cha matajiri sio sahihi.

"Philemon Ndesamburo ni tajiri ndani ya Chadema, lakini hiyo haimaanishi kuwa Chadema ni chama cha matajiri. Kwa hiyo wanapaswa wajue kuwa CCM, NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema si vyama vya matajiri bali vina wanachama matajiri ambao ni waaminifu kwa vyama vyao," alisema Makamba.

"Hawa wehu wanapiga kelele CCM chama cha matajiri, CCM chama cha mafisadi baadhi yao wanachukua posho na mishahara yao hukohuko kwa matajiri," aliongeza.

Alisema yuko tayari kutetea kauli na msimamo huo popote hata ikibidi kufungwa au kufa akimtetea Rais Kikwete.

"Kwanza wakishtaki huyo hakimu mwenyewe atashangaa. Watu wanamvunjia heshima rais halafu anatokea mtu anawaita wehu wanaenda kushtaki, hata huyo hakimu atacheka," alisema Makamba.

Kuhusu hoja kwamba CCM imepoteza mwelekeo, Makamba alisema kabla ya uhuru wakati chama cha Tanganyika African National Union (Tanu) kinaundwa, lengo lilikuwa ni kuwaandaa Watanganyika kujitawala, lakini sasa kila chama cha siasa lengo lake ni kushinda uchaguzi na kushika dola.

Alisema kukubalika kwa chama kunaonekana katika matokeo ya tafiti na chaguzi mbalimbali zinazofanyika mara kwa mara nchini.

“Tumeshinda Tunduru, Kiteto, Busanda, Mbeya Vijijini, Magogoni Zanzibar na tumekomboa jimbo letu la Biharamulo, lakini pia tumeshinda kwa asilimia 93 serikali za mitaa," alisema Makamba.

Alisema kuwa chama bado hakijapata maazimio ya kongamano la taasisi hiyo hawajayapata, lakini watakapoyapata watayajadili katika vikao vya juu vya CCM
 
Unategemea makamba seme nini jamani! kama sio mnamuonea bure , yeye ndiyo yuko hivyo JK wakati anampa ukatibu alijua yuko hivyo na utendaji wake uko hivyo!

Sipati picha hivi kweli CCM yoote mlikosa katibu mkamweka huyu?

Qares wewe na wenzako ebu ondokeni kwenye hicho chama , pumzikeni kama alama ya kutokukubaliana nao.



mwangalie komba!

Makamba yuko radhi hata akiambiwa afue sox za JK atafua tu, usibishe!
 

Sisi tulio wanachama wa chama tawala tunalilia utekelezaji sahihi wa Itikadi ya chama , ambacho ni cha Mkulima na Mfanyakazi.
Kunukuu vitabu vya dini ni kujitayarishia MOTO mkubwa wa kisiasa hapo baadaye.
 


mkulu you are right........hata wakati ule wa mwinyi ambaye tulifikiri he was liberal president ever ...hapakuwa na mtu mwenye balls za kumsema isipokuwa mwalimu peke yake....wengine walikuwa wakisemea vyooni ,au chumbani na wake zao...ukiachilia watu kama kina mtikila na wanafunzi wa chuo kikuu....

lakini hali ya sasa ...tukubali tukatae ni kwamba ma comrade ndani ya ccm wameshindwa kuwa contained na uvumilivu umewaisha sasa wanaongea kwa hasira hadharani...

na mkuuu FM hii ilianza taratibu ..ilipofika watu wa usalama wakiingilia italeta fujo zaidi ...na ndio udhaifu wa system tunaoongelea siku zote.....kila uhuru una mipaka na rais hawezi kujisifu kwa hili....wana ccm wengi waandamizi tunakaa nao na walianza kunungunika chini chini au kwenye vikao vya confidants vya ulabu....lakini system ikifahamishwa wanasiasa wanasema ...achaneni nao...hao walishindwa mwaka 2005...wamekuwa wakiwadharau wale wote ambao hawakumuunga mkono jk 2005...na matokeo ya kutosikilizwa kwao ndio haya kusema hadharani.....
 
Mzee Makamba amefanya kazi yake vizuri ya kupiga porojo nafikiri nafasi yake kubwa kabisa ya utumishi wa umma angestahili kuishia kwenye ukuu wa mkoa. Baada ya kustaafu kumpa kitu cha kufanya labda angejiunga na TOT pale na akina John Komba wakaimba nyimbo za kuhamasisha wananchi kuunga mkono CCM. Nafasi ya ukatibu mkuu wa chama ni kiatu kikubwa sana kwake. Tanzania ya leo si ile ya mwaka 1947 watu sasa wameamka.

Mzee Makamba hawezi kuzuia mto uliofurika maana ukiziba sehemu moja utapata nyingine. Chama chetu sasa kimekuwa kama bendi ya taarabu kila mtu akiamka na wimbo wake wa mipasho. Tutaenda hivi mpaka lini? Wanadhani itakuwa hivi siku zote. My friends I am afraid this time around it is not.
 
makamba ni fisadi mkubwa,hajui tanzania ya leo wala inayokuja....huyo jk wake na ccm yake itaikumbuka itakapo meguka nakuwa ccm na ccmi.....ccm impact hii itakuwa ya watu safi na vijana.
 

Safi.

Nadhani pia makamba hajelewa kwanini watu wanapigia kelele matajiri kwenye CCM, ni kuwa wamekishika chama na wamepewa nguvu ndani ya chama hilo ndilo tatizo.

Pili enzi za Mwl.JKN matajiri walikuwepo wakina Mzee Rupia(Paul Rupia's Father) na wengine ila hao matajiri wa enzi izo walikuwa hawana nguvu ndani ya chama na walikuwa wanakichangia chama na kukitumikia chama na wakati huo Mwl.JKN alikuwa anajenga hoja nzito ambazo matajiri walikuwepo na walikuwa hawakimbili kujinyakulia nafasi ndani ya chama.

Sasa Mzee makamba atujeengee hoja hapa na tujue hao matajiri kwanini wananguvu sana na nafasikubwa na wanasikilizwa sana ndani ya chama? ni utumwa au umaskini kwakuwa tajiri anapesa basi yeye tumsikilize? chama chaongozwa hivyo??? ni heri maskini anaye toa kuku kuliko tajili kutoa mang'ombe na kumtukuza maana atatufanya sie vijakazi wake. Ni heli ngamia kupita tundu la sindano kuliko Tajiri kuingia ufalme wa Mungu. mwazania hapo ni mchezo matajiri wana mambo yahoo bwana let no entertain them ndani ya vyama wata wanyanyasa sana wasiokuwa na uwezo.

Maskini tuchangieni vyama vyetu ili kuwepo na kauli ya vilio vya mnyonge na itasikilizwa

 
Makamba anajua vizuri udhaifu ulipo na pia yeye ndio maana amewekwa hapo maana hata alipochanguliwa watu walipiga sana kelele na pia ilikuwa na vile amelishwa ndimu vile, Sasa ndio siasa hizi zetu za ajabu na watu wa ajabu sana
 
- Tunajaribu kujadili hoja yake on masilahi ya taifa, tukiamini kwamba maneno yake ni yana baraka ya Rais wetu, na pia ni masimamo wa CCM pia!

es!
True FMES!!
Watu hawaichukii CCM kama chama bali yale matendo yasiyokidhi matakwa ya wananchi.
Bila itikadi inayoeleweka kwa wananchi,viongozi wa sasa wanakiweka Chama katika njia panda.
Maadui wa waTanzania bado ni umaskini, ujinga na maradhi,lazima turudie siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.
 

SAFI na SAWA

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…