Tuhuma za rushwa TFF

Joined
Sep 17, 2021
Posts
39
Reaction score
84
Mbunge wa Misungwi, mmiliki wa timu ya Gwambina Alexander Mnyeti ameibua hoja zinazoonesha kuwa na rushwa katika mpira wa Tanzania.

"Wale watu wanataka uje kwenye mpira kwa ubabaishaji wakikuomba hela utoe,l a sivyo utapangiwa ratiba ngumu hadi uchukie. Unapangiwa kwenda Mbeya unacheza unarudi misungwi tena unarudishwa mbeya.

"Uwanja wangu unafungiwa una kila kitu napelekwa Nyamagana ambayo Kapeti limeshachubuka na choo hakuna cha Wageni wananitoa Kwangu ambapo hata mechi za CAF zinaweza kuchezwa hapo.

"Tatizo kuu lilianzia nlipokataa mechi ziende CCM Kirumba za Simba na Yanga wao wanataka hvyo ili wapige hela tu. Nmeamua kuona kuwa nimefaeli uwekezaji wa soka kwa sasa nasubiri hao mabwana najua hawatakaa Milele hapo TFF ndo nitarudi na mimi.

"Nimeshavunja timu na vijana nmeshawaruhusu waende makwao nashangaa TFF wanajitekenya na kucheka mara ooh tuipokonya Point Gwambina na Faini. Sasa wanawapokonya watu ambao hawapo?

"Lengo lao kuu lilikuwa Gwambina ashuke na Apotee na mimi nasema heri nishuke kabisa kuliko nina uwanja mzuri tena niwe nawalipa hela watu burebure."

Alisema Mbunge wa Misungwi Mnyeti kupitia Clouds FM.

 
Sasa ule uwanja utatumika kwa shughuli gani? Ila hela za dhuluma bhana!! Yaani hufanyii hata kitu cha maana.
Haishangazi kuona hata wale jamaa zetu wa barabarani nao kuishia tu kunywea pombe na kuhongea zile hela za manung'uniko.
 
Nilishaongoza timu iliyocheza michuano ya kitaifa. Analosema ni sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…