BAADA ya wananchi wa kata ya Ruaha katika Halmashauri ya manispaa ya Iringa kumtuhumu kwa ufisadi wa shilingi milioni 24 .6 za maendeleo afisa mtendaji wa kata hiyo Nuhu Feruzi ameamua kujiua kwa kunywa sumu.
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mashaka Luhamba alimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa kifo cha mtendaji huyo kimeacha simanzi kubwa kwa Halmashauri hiyo na kuwa kifo chake kimekuja ikiwa ni siku tano toka uongozi wa halmashauri hiyo kufika katika kata hiyo kushughulikia malumbano kati ya wananchi wa kata hiyo na mtendaji huyo.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita Wananchi wa mitaa mbali mbali ya kata ya Ruaha, walivamia ofisi ya mtendaji huyo wakitaka kusomewa mapato na matumizi ya kata yao, jambo ambalo liliwafanya mtendaji wa kata huyo na yo Nuhu Feruzi na Diwani Alphonse Mlagala , kuondoka ofisini pasipo kuwapa taarifa hiyo.
Wiki iliyopita wananchi wa kata hiyo waliamua kuifunga ofisi ya Afisa mtendaji huyo wakishinikiza kusomewa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za maendeleo huku wakimtuhumu kuwa amefanya ufisadi wa shilingi mil 24.6 za ruzuku, na kodi ya minara ya simu katika kata hiyo
Hata hivyo ndugu wa marehemu huyo walipofuatwa na mwandishi wa habari hizi ili kuelezea mazingira ya kifo hicho waligoma kuzungumza chochote kwa madai kuwa si wasemaji wa kifo hicho .
Kaimu afisa mnadhimu wa jeshi la Polisi Mkoani Iringa, Hamfrey Saganya alisema kuwa afisa mtendaji huyo, alikutwa akiwa amekufa chumbani kwake, baada ya kunywa sumu ambayo haijajulikana aina yake, katika maeneo ya Mwangata, Manispaa ya Iringa.(Imeandikwa naFrancis Godwin)
Source:francisgodwi.blogspot.com na Mjengwa.blogspot.com