hakuna haja ya kumlaumu kijana mwita au kumhukumu kwa kigezo cha aliyofanya akiwa daruso, kwa sasa ameonyesha njia, ni nani huko ccm ukiacha nape, aloyce kimaro, ana kilango anaweza kuwakemea akina lowasa na mafisadi wengine?
kwa kuwa huyu naye ameungana na kundi lilo jema ni vema aktuzwa kwa ushujaa wake, na kwa kusahau yaliyopita, je kama ameamua kuongoka kama Mtume Paul je?
First LADY NANI ASIYEJUA KUWA WEWE KIBARAKA WA NCHIMBI, HEBU TUTAJIE HUO UFISADI WA WAITARA, WEWE NI MMOJA WA WALE WANAO PINGANA NA VITA DHIDI YA UFISADI, WAITARA SONGA MBELE HIYO NDIYO NJIA HUKO KWINGINE ULIPOTEAHumjui MWITA!Huyo ndo fisadi kabisa anajua aliyoyafanya alivyokuwa Raisi wa DARUSO pale mlimani!hapo anatapatapa tu!lakini kutapatapa kwake at least kunasaidia kukosoa chama chake!ila na yeye ni walewale nakuambia asingehamishwa kutoka Dar kwenda kuwa katibu wa UV-CCM Tanga wala asingemtetea Nape!Na sasa anasema hayo kutokana na hasira ya kurudishwa tena Dar kuwa katibu msaidizi wa Nchimbi
...No First Lady hapo si uchu wa madaraka kama umesoma hiyo habari anachopinga Mwita ni kupelekwa Makao makuu ma kuwa msaidizi wa Nchimbi....Unadhani angebaki Tanga na wadhifa wake aliokuwa nao angelalamika?Huyu ex Raisi wa DARUSO hana jipya kakosa vyeo alivyovitaka ndo maana!kwa nini wakati kampeni zinaaanza hakusema hayo?hamna kitu wewe MWITA MWIKWABE!uchu wa madaraka ndo unakufanya ulielie!
....Karibu sana mkuu. Lakini kwa hilo napenda kutofautiana na wewe. Mbona habari inajieleza wandugu nyie mnakazania kumtoa Mwita kwenye mstari?? Haya kwa nyie mnaomfahamu mimi nimekutana nae magazetini tu lakini maelezo yake yanajitosheleza kabisa juu ya msimamo wake....Habari wana Jamii.
nakaribia katika jamvi baada ya kua msomaji kwa muda mrefu nimeona nami nipate fursa ya kua mchangiaji.
Mwita kwa alichofanya si jambo la ajabu kwani wanomfahamu ajali alopata mwaka jana ya pikipiki mpaka akalazwa muhimbili kwa miezi mitatu wanaweza kuelewa kua ajali ile ilimsababishia tatizo la akili so anayoya sema na kutenda naamini ni matokeo ya kuchanganyikiwa kwakwe baada ya ajali ile.
...No First Lady hapo si uchu wa madaraka kama umesoma hiyo habari anachopinga Mwita ni kupelekwa Makao makuu ma kuwa msaidizi wa Nchimbi....Unadhani angebaki Tanga na wadhifa wake aliokuwa nao angelalamika?
Bravo Mwitra enzi za kunyenyekea vivuli vya binadamu wenzetu hazipo tena.
...Fisrt Lady read between lines please...katika katiba ya Umoja wa vijana CCM hakuna huo wadhifa aliotakiwa kwenda kutumikia Mwita makao makuu. Na sitaki kuamini kuwa ukipewa demotion basi unatengenezewa tu nafasi fulani ili uwepo wepo tu. Jamani si unaanza sergent ndio unakuwa staff sergent hata ukiteremshwa cheo utarudi chini through same channel...Anaposema akawe mtenga cha wa Nchimbi anamaanisha nini?Kweli kama ameamua kukitumikia Chama yeye akishushwa cheo mbona ananuna?
...Fisrt Lady read between lines please...katika katiba ya Umoja wa vijana CCM hakuna huo wadhifa aliotakiwa kwenda kutumikia Mwita makao makuu. Na sitaki kuamini kuwa ukipewa demotion basi unatengenezewa tu nafasi fulani ili uwepo wepo tu. Jamani si unaanza sergent ndio unakuwa staff sergent hata ukiteremshwa cheo utarudi chini through same channel...
Hata kama ni demotion are you sure kuwa alielezwa kosa lake na kupewa nafasi ya kujitetea hatimaye kuonekana mkosefu na kuwa adhibiwe?
Sasa hapo ndo amekosea amepewa hiyo barua akiwa huko Tarime sasa angetumia busara na kuongea na chama chake!sio kupayuka kwa waandishi wa habari na kusema maneno kama aliyosema!Hapo amekosea sana na atajutia sana huo uropokaji wake!
tafsiri ya ya chama mmeipoteza na nani? Ulitakiwa kusema wewe pekeyako na mafisadi umepoteza tafsiri ya ccm kwa kusema kidumu chama cha mapinduzi badala ya kigumu chama cha mafisadi hiyo ndiyo tafsiri harisi ya ccm. Halafu sioni ajabu unapo sema waitare si kiongozi maana kwenu yeyote anaye gusa ufisadi si kiongozi anaye faa ndani ccm chama cha mafisadi kiongozi ndani ya chama chenu ni yule anaye utetea ufisadi kwa nguvu zake zote. Hapo umechemkahata kama jamii inaona anachosema ni kweli basi nadhani yeye na wengine humu tumepoteza tafsiri ya chama na sasa tunamfanya mtu kuwa na wasifu wa chama. Ninampinga yeye binafsi kwani njia aliyoitumia haimjengi yeye kama mwita lakini kibaya zaidi anathibitisha kuwa yeye si mtu wa utaratibu na asiye tayari kukosolewa na kwa maelezo yake ameonyesha wazi yeye anatawaliwa na mob saikoloji. Ni hatari kuwa na kiongozi anayesukumwa na hadhira baadala ya yeye ku study hadhira na kuiongoza ktk dira sahihi na siyo kukurupuka, ufisadi ni agenda ya dunia hivyo inataka hekima unapoijadili mbele ya familia yako maana unaweza ukajikuta unamtukana babako tena hadharani.
Ccm na jumuiya zake wana utaratibu wa kuhojiana, kutofautiana na mwisho muafaka kwa maslahi ya chama na nchi, iweje kada kama mwita ajiondoe ktk mstari huo na kuitumia tarime kama mahala pa kugomea nafasi yake mpya ya usaidizi wa m/kiti eti kwa njozi za kuwepo kwa mazingira ya kutimuliwa baadaye?!!!!!
Hapa hatuna kiongozi ndani ya mwita zaidi ya upayukaji usio na tija wala kuheshimu mipaka.
Kidumu chama cha mapinduzi.
wakuu
siku zote nimekuwa nikiitetea CCM,najua mapungufu yao ila huu ni uzugaji ambao watanzania wanataka kuingia mkenge.Mwanakiji alishaonya kwamba mwaka huu watuzuge tukazugika ila mmeshakubali kufungwa bao lingine la kisigino.
connecting to the Dot is Mwita liingizwa kwenye Siasa na Mzee Kngunge who also recomend Makamba to be CCM General Secreatary which implies that they know each others.
Hii ni mbinu ya kupunguza nguvu ya Upinzani Tarime.Sijaipenda hii njia waliyoitumia kwa wiki hii.Najua CCM itashinda ili kwa njia hii walipotoka na nawasikitikia wale ambao wmechukulia kweli.
ila ole wenu CHADEMA kama mkiamua kumchukua huyu kijana ambaye wakati akiwa Rais amewaongoza baadhi ya vijana wa CHADEMA,hivyo kama mko tayari kumchukua msubiri yale yale ya kina Hizza.ni watu wa aina ya kina hizza na akwilombe.
i!kama ngeleja anaacha kushughulikia suala la kitaifa baada ya tanesco kutangaza mgao wa umeme, badala yake anaklwenda nyamongo kwenye kampeni unategemea nini?.
.
Ninampinga yeye binafsi kwani njia aliyoitumia haimjengi yeye kama Mwita
Ni hatari kuwa na kiongozi anayesukumwa na hadhira baadala ya yeye ku study hadhira
CCM na Jumuiya zake wana utaratibu wa kuhojiana, kutofautiana na mwisho muafaka kwa maslahi ya chama
mkulu kwakweli hapo umeyumba sana.
ni ukweli ulio wazi kuwa njia aliyoitumia inamjenga sana yeye binafsi kuliko kukijenga ccm,kwakuwa ccm haitaki wajenzi sasahivi bali inakumbatia wale wanaoitumia kuendesha ufisadi.
haiwezi kuwa hatari kwa kiongozi kusukumwa na hadhira.Hujawahi kusikia kuwa Bill Clintin wakati akiwa rais wa marekani alikuwa akiacha kusoma hotuba aliyoandaliwa na badala yake anatoa hotuba kutokana na namna anavyoisoma hadhira?ndugu yangu ni muhimu sana kuzungumza na hadhira inayokuelewa.Kila siku hapa tunawawashauri viongozi kuwa wawe wanasoma alama za nyakati.
ccm na jumuiya zake hawana utaratibu wowote wa maana zaidi ya kuitana wendawazimu na kufukuzana uanachma pale wanapoambiwa ukweli.
.
Ninampinga yeye binafsi kwani njia aliyoitumia haimjengi yeye kama Mwita
Ni hatari kuwa na kiongozi anayesukumwa na hadhira baadala ya yeye ku study hadhira
CCM na Jumuiya zake wana utaratibu wa kuhojiana, kutofautiana na mwisho muafaka kwa maslahi ya chama
mkulu kwakweli hapo umeyumba sana.
ni ukweli ulio wazi kuwa njia aliyoitumia inamjenga sana yeye binafsi kuliko kukijenga ccm,kwakuwa ccm haitaki wajenzi sasahivi bali inakumbatia wale wanaoitumia kuendesha ufisadi.
haiwezi kuwa hatari kwa kiongozi kusukumwa na hadhira.Hujawahi kusikia kuwa Bill Clintin wakati akiwa rais wa marekani alikuwa akiacha kusoma hotuba aliyoandaliwa na badala yake anatoa hotuba kutokana na namna anavyoisoma hadhira?ndugu yangu ni muhimu sana kuzungumza na hadhira inayokuelewa.Kila siku hapa tunawawashauri viongozi kuwa wawe wanasoma alama za nyakati.
ccm na jumuiya zake hawana utaratibu wowote wa maana zaidi ya kuitana wendawazimu na kufukuzana uanachma pale wanapoambiwa ukweli.
Kama CHADEMA WALIVUMSIMAMISHA WANGWE alipowaambia ukweli!